Monalisa ashinda tuzo Kimataifa ya Emmy Kids 2022

Thus tunasema kupata sio ujanja bali ni wakati ukifika kila unachogusa kina tiki
Na juhudi pia
20230317_081837.jpg
 
hamna mbwembwe ,awalimu ni ajira tu kuna maisha mengi nje ya ualimu, ficha mdomoni kauli zako si kila mwalimu ni fala
Kua Mwalimu wewe unayelia kila siku una maisha magumu (rejea posts zako) unaweza ukamuajiri Monalisa na Ukoo wangu mzima

 
p-1024x819.jpg

MWIGIZAJI Mtanzania Yvonne Cherrie, maarufu kama ‘Monalisa’ ameshinda tuzo ya kimataifa Emmy Kids 2022 katika series ya ‘My Better World Show’ kwa kuingiza sauti kwa lugha ya Kiingereza.

Baada ya ushindi huo, Monalisa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram ameandika “Miaka minne iliyopita, nilikuwa mmoja wa waigizaji tuliochaguliwa kuingiza sauti kwa lugha ya Kiingereza katika series ya My Better World Show ambapo mimi binafsi nilitia sauti ya wahusika watatu.

Napenda kukujulisha kuwa, series hiyo imeshinda moja kati ya tuzo kubwa sana duniani, tuzo za EMMYS 2022, katika Kipengele cha International Emmy Kids: Entertainment and Factual. Na usiku wa jana tulipata wasaa wa kukutana CAST and CREW ili kusherehekea ushindi huo.”ameandika Monalisa.

Amemaliza kwa kuandika “Sio mbaya ukaanza kuniita Emmy award winner voice over artist. Hongera kwa Timu nzima kwakweli, maana ni kazi kubwa iliyoshirikisha watu mbalimbali wa nchi mbalimbali za Afrika.”
Snapinsta.app_1080_332264085_215553984361629_8716069928478680423_n-823x1024.jpg
Nikimpenda tangu kipindi kile yupo Mambo Hayo
 
Back
Top Bottom