Moja kati usafiri hatari hapa mjini... Boda boda!!!

excel

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
22,463
Reaction score
17,960
Habari zenu wadau... leo naomba tujionee kisa cha huyu jamaa aliyejipatia ajali maeneo fulani hapa jijini, halafu tujadili jinsi tunavyochukulia aina hii ya usafiri...


hii ni gari iliyopata ajali ilikutana na pikipiki uso kwa uso..




gari ikazidi kuibonda zaidi pikipiki namna hii....



na zaidi...




huyo jamaa mwenye helmet ndiye dereva hasa wa boda boda aliyenusurika kutoka ajalini...



hawa ni askari wakisaidiana na raia wakifanya yao 'baada' ya ajali..





jamani suala la msingi hapa... hawa madereva wa pikipiki wamekuwa watu wa ajabu sana.. kwanza wengi wao si wafuataji wa sheria za barabarani kiujumla..

wao wanadhani wana haki ya kufika wanakoenda mapema zaidi kuliko mtu awaye yeyote yule mwenye chombo cha usafiri, hivyo wanapelekea ajali na misongamano isiyo ya lazima....

aina za mwendo kasi wanazoendeshea zimekuwa za juu mno kiasi cha kuwa kero sababu ya kelele na kupelekea ajali...

kwenu wadau, hivi huwa mnajisikiaje hasa mnapokuwa mmekodi pikipiki? suala la usalama wenu huwa mnalizingatia?

je, wao wanapokuwa wanaendesha kwa spidi kubwa, huwa mnachukua hatua gani? ama ninyi ndio mnaowapa amri?
Excel
 
Last edited by a moderator:
Ndiomaana sijawahi kukodi bodaboda, iyo bajaji kwa shida sana
 
Mimi naogopa hata kuziona licha ya kuzipanda. Jana walifakamiana mwenye bodaboda na baiskeli wakaja kuangukia pembeni mwa gari yangu...nashukuru hawakunichubua...ni hatari...unajua kuwa unatoka lakini huna hakika kama utarudi
 
kumbe kuku wanalipa sana mpaka umenunua gari. ngoja na mimi nifuge



Mimi naogopa hata kuziona licha ya kuzipanda. Jana walifakamiana mwenye bodaboda na baiskeli wakaja kuangukia pembeni mwa gari yangu...nashukuru hawakunichubua...ni hatari...unajua kuwa unatoka lakini huna hakika kama utarudi
 
Ni kweli bodaboda wengi hawajui sheria lakini hili nalo limegeuka kuwa kinga kwa madereva wa magari maana wakati mwingine huwafanyia maksudi bodaboda hata pale wanapokuwa kwenye sheria. Na tatizo kubwa ni madereva wa daladala.
 
Mungu mkubwa kapona hapo?,majinga sana madreva wa bodaboda.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…