kukukakara
JF-Expert Member
- Jul 31, 2012
- 496
- 164
Wanajamvi, hasa waishio Dar,
Naamini kabisa wengi wetu tumekuwa tukisugua vichwa kutafakari nini hasa hakijafanyika katika swala zima la kuboresha mzunguko wa vyombo vya usafiri (Mobility) na hivyo kupunguza adha kubwa ya foleni na karaha zake. Pengine yapo yasiyofanyika kutokana na gharama zake lakini mimi najikita na yale ambayo nadhani gharama ni ndogo na uwezekano (feasibility) ni mkubwa.
1. Magari ya mizigo mikubwa kama vile malori ya makontainer yatemebee usiku tu kuanzia saa tano hadi saa kumi na moja alfajiri. Nimejiridhisha kuanzia saa tano barabara za Bandari -Ubungo huwa kimya kama vile hatuna shida ya foleni Dar. Wadadisi watauliza muda wote huu malori haya yatakuwa wapi yakipakia mizigo bandarini?
Hapo sasa utapata jibu kuwa wataalamu wetu kwa kutokuliona hili mapema wamegawa ardhi yote ya Kurasini kwa wawelkezaji madepo na shughuli kama hizo lakini wakasahau kuwa Malori ya mizigo hayana eneo tengefu la kusuburia kupakia au kuingia bandarini (Truck Holding area).
Wakati shimo udongo inavunjwa wengi tulidhani ni upanuzi wa bandari na moja ya lengo ni kutengeneza 'Truck Holding area'. Leo tunalia foleni zimezidi tunasingizia magari yamezidi eneo barabara ni ndogo. Kupanga ni Kuchagua wacha tubanane nayo na saa nyingine yatuangushie makontena.
2. Kwanini hatuna utaratibu wa kufunga barabara kadhaa na zikawa one way kwa masaa Fulani, hasa rush hours. Sio jambo geni asubuhi kwa muda wa masaa mawili au matatu barabara zote zinaoingia mjini zote ziingie (One way in) na jioni zote zitoke (One way Out). Hii itawezesha kuondoa msongamano na watu watajipanga kutokana na hayo masaa.
Wanaokatiza barabara hizi watajipanga kusubiri masaa haya yapite au wafuate mkondo unaotakiwa. Askari wetu badala ya kuteseka na junctions wangesimamia utaratibu huu kwa muda mufupi na kisha kuondoka kwani idadi kubwa ya magari itakuwa imeondoka au kuingia mjini.
3. Ring Roads: Barabara za pembezoni. Jiji lijikite kwa makusudi kuboresha bara bara za pembezoni na kwa mimi naona kuna mambo mengine ambayo pesa inaenda bure wakati bado kunavipa umbele kama hivi. Kwa mfano kuna repair za lami katikati ya jiji tena lami bado zinaonekana ni nzima inakwanguliwa na kuwekwa nyingine. Hizi pesa zingeenda kumwaga vifusi na kuchonga barabara nyingi mitaani magari yachepukie kuacha main road.
Mapambo kama ya hizo chuma zilizo chimbiwa bustani za baraba kuu zote kutoka Airpoti hadi mjini na kwingineko mimi naona ni kama kupaka wanja uso usionawa. Bora hizo pesa zingeenda kuimarisha Ring roads
4. Usafiri wa umma: Hili limeanza kuleta ufanisi na kama kuna watu wa Ubungo - Kimara bado wantumia magari ya binafsi kuanzia la mama, la baba, na la watoto basi ni utamaduni unaopaswa kukemewa. Kama kuna jirani yako muda huu ana hii tabia hata kama ni tajiri mchekeni.
5. Watu binafsi waruhusiwe kuanzisha daladala na boda boda za majini na watengenezewe miundo mbinu yake na wizara husika. Boat za abiria toka Mbagala hadi Ferry miaka hamsini ya uhuru sasa hakuna. Boat za bairia toka Ferry hadi Kawe na mbele zaidi hadi Bagamoyo sio lazima ziwe za serikali watu wenye pesa zao wahamasisishwe kuwekeza. Maji ya bahari yameka bure.
6. Daladala hazijathibitiwa kuhusu kutanua, kuchomekea na fujo zote hizo barabarani. Mipango ya mbeleni ifikirie kutengeza lane maalumu ya dala dala, japo matarajio yetu usafiri wa umma mathubuti aina ya hii DART kwa sasa ifikie kuua daladala jijini kabisa
7. Traffic waachane na kuingilia kazi ya traffic lights. Wawepo kurekebisha mzunguko tu kama kuna tatizo kama ajali ikitokea au taa zikizima. Wao ni binadamu si rahisi kubalance uwingi wa magari katika njia zote, huweza kuzidisha au kupunguza upande moja na hivyo kusabaisha kero kwa mwingine. JIJI liimarishe TRAFFIC Lights. Ni Dar tu kwa uzoefu wangu Tarffic wanatumika kufanya kazi ya Taa za kuongezea magari wakati wan kazi zao nyingi na muhimu za kufanya.
Ongeza na ya kwako!