Moise Katumbi Sasa Autaka Uraisi

Moise Katumbi Sasa Autaka Uraisi

Ni chotara wa kiisraeli, na kwa kipindi kirefu amekuwa akishirikiana na wafanyabiashara wa Israeli katika utafiti wa mafuta na biashara za uchimbaji madini nchini humo. Kwa hiyo ana ushawishi kiasi fulani ukizingatia siasa za Kongo zinavyokwenda, ambapo hata rais aliyepo madarakani kuna madai ya kuwa ni pandikizi kutoka nchi jirani.

Baada ya kupinduliwa Laurent Kabila, kwa nafasi kubwa serikali ya Kongo inaongozwa na raia wa kigeni kuanzia ikulu hadi kwenye majimbo. Mwanasiasa aliyekuwa na harakati za kuirudisha Kongo kwa wakongomani alikuwa ni Jean-Pierre Pemba, ambaye amefungiwa na mahakama ya ICC kushiriki siasa za Kongo.
Kabila baba pia alikuwa na harakati za kuirudisha CONGO kwa wakongoman na alishaanza kufanya maendeleo lakin hakukaa sana kwenye kiti cha uraisi
 
Haaaa!!! A nation should governed by a greater thinker its imposible to katumbi 2be the predider of congo
 
ila mpaka sasa hivi Katumbi sina uhakika kama yuko Congo maana kuna ponya ponya nyingi za kumkili zimempitia....yapo makampuni mengi ya mining huku yamefunga kupisha uchaguzi kukwepa vurugu halafu Jose K hataki uchaguzi uwepo anadai hana fedha za kuendesha uchaguzi...
 
Ngoja aupate huo urais akutane na wakina kagame na museveni afu ajichanganye kwenye 18 zao, atajua tofaut ya kua rais wa Tp mazembe na kua rais wa nchi
 
ila mpaka sasa hivi Katumbi sina uhakika kama yuko Congo maana kuna ponya ponya nyingi za kumkili zimempitia....yapo makampuni mengi ya mining huku yamefunga kupisha uchaguzi kukwepa vurugu halafu Jose K hataki uchaguzi uwepo anadai hana fedha za kuendesha uchaguzi...
Inawezekana kabisa hayupo Congo mkuu. Jamaa anacheza michezo ya hatari sana kuchezea sharubu za Jöse K. Angejikita kwenye biashara na kuachana na siasa. Mbaya zaidi baada ya kutofautiana na Jöse akaanza kumkandia na kumchalenji hadharani.
 
Hiyo biashara ya samaki ilikuwa ni muendelezo. Lakini jamaa familia yao ilikuwa na uwezo tangu zamani. Majina alibadilisha, anatumia majina ya wajomba zake kwani majina ya upande wa baba ni ya kiisraeli halisi. Hii imemsaidia kushiriki katika siasa za Kongo kikamilifu.

Kama unavyofahamu waisraeli hawaachi damu yao ipotee, wana taarifa za ndugu zao popote pale walipo. Na ndio waliomtumia kuingia Kongo na kufanya utafiti wa mafuta katika ziwa Albert na biashara ya madini katika jimbo la Katanga.
Baba yake Moïse Katumbi alikuwa ni Mgiriki mkuu...jina lake aliitwa NISSIM SORIANO. Fanya utafiti kidogo. Huko Israel walipita na kutengeneza business connections tu Kama alivyopita Zambia na kuwekeza sana huko pia. Alipofika Moero ndio akajikita huko baada ya kuona opportunity ya Uvuvi na Madini..na ndipo alipoamua kuoa (Virginie Katumbi) kabisa ili asipate longolongo kwenye biashara zake.
 
Huyu bwana nadhani angeachana na siasa na ajikite kwenye biashara zake maana uraisi wa Kongo hauna tofauti na hukumu ya kifo.....
Lakini pia kuwa gavana wa Katanga sio kitu kidogo mkuu,utajiri mkubwa wa Kongo umejikita katika jimbo hilo.
 
Lakini pia kuwa gavana wa Katanga sio kitu kidogo mkuu,utajiri mkubwa wa Kongo umejikita katika jimbo hilo.
Jamaa pale alipewa shavu na Jöse K kwa maslahi na kazi maalum. Ndio maana alikuwa hapindui wala humwambii kitu tofauti juu ya Jöse. Alipojikita na kuapata sapoti kutoka kwa wananchi haswa mashabiki wa TP Mazembe, akapata nguvu kwamba ataweza kumchalenji Jöse. Bila kujua ya kwamba alishatengenezewa mitego tokea nyuma ya kwamba Kama akiutaka URAIS wa Congo wataanza kutegua na kuyatoa hadharani madudu aliyokuwa akifanya. Na ndio kinachotokea sasa hivi. Tunavyoongea sidhani Kama jamaa bado yuko Congo kwa sasa.
 
Siasa za Africa ni ngumu sana.Kwa mtindo huo aachane tu na siasa aendelee kutupa burudani na TP Mazembe.
 
Siasa za Africa ni ngumu sana.Kwa mtindo huo aachane tu na siasa aendelee kutupa burudani na TP Mazembe.
Kupita kiasi mkuu. Akifanya mchezo hata TP Mazembe inaweza ikakumbwa na dhoruba. Kuna ule Wimbo unaitwa "Usimchezee Chatu ooh Chatu eeeh...gongo usimtupie utaukosa ushindi" huwa napenda sana kuusikiliza una maneno ya maana sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom