MOI yapewa saa 48 mashine za MRI na CT-SCAN zifanye kazi

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,738
15,205
Katibu mkuu wa wizara ya afya prof Abel Makubi amefanya ziara ya kushitukiza kwenye hospitali ya taifa ya muhimbili kitengo cha mifupa MOI na kukuta mashine za MRI na CT scan zimeshaharibika na hazifanyi kazi kwa muda mrefu hivyo wagonjwa huelekezwa waende kupata matibabu kwenye hospitali za watu binafsi.

Prof Makubi ametoa masaa 48 kwa uongozi wa hospitali hiyo kuweza kurekebisha hali hiyo na waanze kuhudumia wananchi kama kawaida.

Abel aache u Magufuli wake wa kuharibu chakula cha watu.

Mambo ya mitambo hiyo kuwa mizima muda wote kama ilivyokuwa kwenye Utawala wa JPM yalishapitwa na wakati na sasa tunaharibu mashine makusudi ili wagonjwa waende kwenye hsptl zetu binafsi.
 
Ukija kuugua Utajua kama Umeandika Upumbavu na Ugolo
Vifaa vimeharibika Unaambiwa muda mrefu walifanya nn
Acha kulete utoto na ujinga kwenye Maisha yawatu
 
Abel aache u Magufuli wake wa kuharibu chakula cha watu.

Mambo ya mitambo hiyo kuwa mizima muda wote kama ilivyokuwa kwenye Utawala wa JPM yalishapitwa na wakati na sasa tunaharibu mashine makusudi ili wagonjwa waende kwenye hsptl zetu binafsi.
Kabisa!

Sasa hivi ni wakati wa watu kula!

Huku wakiwakomesha sukuma gang, kufuta legacy na kuwafuta machozi machadema baada ya kuonewa sana kwa miaka 5
 
Lakini huongelei mamia ya makaburi ya Wananchi waliouwawa na Utawala huo uliolaaniwa.
 
Kwa muda mrefu!! Halafu utaambiwa huko mahospitalini kuna wapelelezi!,sijui kazi yao ni udaku. ?
Yani hili taifa ni Kama vile kuna kataifa kadogo ndani yake!
Wapelelezi! Au unamaana wana Usalama?
 
Nasikia wakuu wote wa vitengo ni TISS, je mambo ya "mashine zimeharibika kwa muda mrefu" zinatoka wapi?
Au kuna Tanzania ingine siijui
 
Abel aache u Magufuli wake wa kuharibu chakula cha watu.

Mambo ya mitambo hiyo kuwa mizima muda wote kama ilivyokuwa kwenye Utawala wa JPM yalishapitwa na wakati na sasa tunaharibu mashine makusudi ili wagonjwa waende kwenye hsptl zetu binafsi.
Huwa tunaambiwa kuna mtu wa kitengo.sasa ana ripoti nini kama issue kama hizo hazifanyiwi kazi.Nadhani njaa ndio sababu inafanya mtu anajitambulisha kuwa mtu wa kitengo ili nae apate mgawo.Hiyo idara ingefumuliwa.
 
Katibu mkuu wa wizara ya afya prof Abel Makubi amefanya ziara ya kushitukiza kwenye hospitali ya taifa ya muhimbili kitengo cha mifupa MOI na kukuta mashine za MRI na CT scan zimeshaharibika na hazifanyi kazi kwa muda mrefu hivyo wagonjwa huelekezwa waende kupata matibabu kwenye hospitali za watu binafsi.

Prof Makubi ametoa masaa 48 kwa uongozi wa hospitali hiyo kuweza kurekebisha hali hiyo na waanze kuhudumia wananchi kama kawaida.

🤣🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Nchi hii kwa usanii? Hivi hawajiulizi tu kwa nini mambo hayaendi pamoja na kufanya ziara za kushtukiza, pamoja na kutoa vitisho, pamoja na kutoa muda, pamoja na kila kitu? Huu ni upumbavu nchi yenye watu zaidi ya mil 60 kujaribu kufanya mambo yale yale kwa njia ile ile huku tukitegemea matokeo tofauti! Kwa nini tusikiri kuwa mfumo wetu hautufai na tujaribu kuufumua na kuunda mpya?
 
Nasikia wakuu wote wa vitengo ni TISS, je mambo ya "mashine zimeharibika kwa muda mrefu" zinatoka wapi?
Au kuna Tanzania ingine siijui
Huko unakodhani ni ''malaika'' basi ndiko kwenye ''mashetani''. Tukubali tu kuwa mfumo wetu wa kuongoza nchi haufai na tuufumue na kuunda upya. Uzuri ni kuwa tayari kuna nchi zenye mifumo inayofanya kazi vizuri hivyo tunaweza kuiga na kufanya modification ili iendane na mazingira yetu.
 
Well done prof Makubi ila ningeshauri improvement ya hizi taasisi ifanywe kitaalamu ,maana naona idea unazitoa kichwani plan za maboresho ni.muhimu.zikawa planned na kuwa documented. Prof Makubi naamini ushafanya kazi nje procedures zote ziko researched na kuwa documented ambayo ni rahisi kutrace where something goes wrong .
 
Embu tuma hizo picha za makaburi hayo!! Na tutajia jamii iliyolalamika kupoteza ndugu,!!acha ugaidi kichwani
Tuko kwenye Maridhiano na Mama
Embu tuma hizo picha za makaburi hayo!! Na tutajia jamii iliyolalamika kupoteza ndugu,!!acha ugaidi kichwani
Wengi wamezikwa kwenye mass graves huko Rufiji na wengine walitupwa Mto Ruvu wakiwa ndani ya mifuko ya sandarusi.
 
Back
Top Bottom