MOI kufurika abiria wa Mwendo kasi!

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,636
2,725
Jamani hali ni mbaya kwenye peak hours ukitaka kupanda kwenye mwendo kasi.
Ile stampede ya abiria kuwahi siti ni balaa.

Jana katika kuwahi gari za Kimara, nilipigwa push nikabanwa mbavu na mabega yote.
Maumivu niliyoyapata ni zaidi ya ajali ya boda boda.

Hali ikiendelea hivi watu wengi sana watakuwa na majeraha ya ndani hasa kwenye kifua na mbavu.

Jamani abiria kuweni na ustaarabu.

Mwendo kasi sio gari ya kwenda Mbinguni, useme kwamba ukiachwa ndio imetoka. No! Mabasi yako mengi, likijaa moja si utapanda linalofuata?
 
mbagala tushazoea tukibanana kwenye mlango wa dcm hivi ni mdogo halafu tupo watano hapo haingii mtu utakuta mwengine kapitisha kichwa mwengine mguu mwengine mikono mwengine kiwiliwili miguu ipo chini tumeshazoea njoo huju uone na upate darasa jinsi ya kumzuia baunsa mlangoni
 
Kama ingekuwa kugombania gari unaenda MOI wakazi wa Mbagala si wangejaa sana huko MOI..?

Mbagala ni hatari watu wanabanana kuingia kwenye gari kupitia madirishani.Dirisha moja vichwa viwili vinatangulizwa kuingia ndani kupitia dirishani kila kimoja kikipigania kuingia.Vyote vinamudu kuingia ndani ya dirisha kwa wakati mmoja.

Kasheshe sasa inakuwa namna viwiliwili vyao vitakavyoweza kuingia ndani hapo ndipo mtu unabanwa hadi kukaribia kujinyea.Hayo ya kubanana mwendo kasi mbona ni bado LUXURY basi kwa mbagala.

Mbagala nauli unaweka mdomoni SIO MIFUKONI unapoingilia dirishani.Mifuko ya suruali kama mwanaume unaiacha free ili kibaka awe huru ku-search atakavyo maana hujaweka kitu.
 
Ww unayejuwa yako mengi si ungesubiri jingine? Hakuna namna wakubane tyu maana ulitaka mwenyewe
 
Mbagala ni hatari watu wanabanana kuingia kwenye gari kupitia madirishani.Dirisha moja vichwa viwili vinatangulizwa kuingia ndani kupitia dirishani kila kimoja kikipigania kuingia.Vyote vinamudu kuingia ndani ya dirisha kwa wakati mmoja.Kasheshe sasa inakuwa namna viwiliwili vyao vitakavyoweza kuingia ndani hapo ndipo mtu unabanwa hadi kukaribia kujinyea.Hayo ya kubanana mwendo kasi mbona ni bado LUXURY basi kwa mbagala.

Mbagala nauli unaweka mdomoni SIO MIFUKONI unapoingilia dirishani.Mifuko ya suruali kama mwanaume unaiacha free ili kibaka awe huru ku-search atakavyo maana hujaweka kitu.
Dah, hapa nimechoka mwenyewe!
 
Achana na kuingia ndani ya basi pale kimara, kutoka napo ni shida wakati wa peak time, ukiwnda shukia kimara kati ya saa 12 asubuhi na saa 3 asubuhi unaweza ukashindwa kushuka, unarudishwa ndani na abiria wanaogombea kuingia ndani!
Ni kero tupu.
 
Wanajikanda na maji ya moto, maumivu yanapoa. Chezea gharama za matibabu weye? Mimi bora nirudi kwenye treni la Mwakyembe. Mwendokasi, basiii.
ushazoea maisha ya raha endelea kutafuta raha,unafananisha ajali za bodaboda na msukumano wa magari ya mwendokasi kweli???jaribu kutafuta kitu kingine cha kufananisha nacho,moi imejaa vijana wa bodaboda hodi nzima imejaa na hata miaka kumi haijapita toka hiyo biashara iwe rasmi lakini watu tunadandia tunasukumana huu mwaka wa 15 mtoto anazaliwa sasa hivi yupo secondary na hatujawahi gusa moi wewe kidogo tu unalialia humu acha pumba kijana
 
Nahs ww ndo wale waliokuwa wemezoea kunyofoa vinauli vyetu na simu kwenye milango midogo ya costa eicher dcm n.k sasa uko kwa M/kasi milango mikubwa umedoda
 
Back
Top Bottom