Mohammed Enterprise Limited ( METL) matatani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mohammed Enterprise Limited ( METL) matatani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bagamoyo, Oct 29, 2012.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,525
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Serikali Mkoani Iringa imeifungia na kuinyanganya kampuni maarufu ya Mohammed Enterprise kufanya biashara ya mbolea mkoani Iringa. Sababu kuu ya serikali ya mkoa kuchukua hatua hiyo dhini ya kampuni ya Mohammed Enterprise ni baada ya kukuta mbolea ktk maghala ya kampuni hiyo ikiwa:


  • Haina viwango vya ubora
  • Mbolea imeganda
  • mifuko haionyeshi expiry date
  • mifuko haina viashiria vya mchanganyiko wa mbolea
  Wakulima mkoani Iringa wameelezea wasiwasi wao wa kupata mazao bora baada ya pembejeo hiyo toka Mohammed Enterprise kukosa viwango na kurudisha nyuma juhudi za kauli-mbiu KILIMO KWANZA.

  Kampuni ya Mohammed Enterprise imeshaandikiwa barua kuhusu hatua hiyo na viongozi wa Mohammed Enterprise wamekubali hatua hiyo ya serikali.

  Source: StarTV habari za jioni 29/10/2012 Radio Free Africa Tanzania*|* STARTV LIVE
   
 2. Mwanahisa

  Mwanahisa JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 1,397
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ipelekwe maabara kabisa kuchunguza ni mchanganyiko wa aina gani kwani hata kuimwaga au uteketezaji wake unaweza leta madhara.Iko kiasi gani na ilipitishwa na mamlaka ipi ya viwango. Wakuwajibika hapo sio MeTL peke yao.
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Wanaandaliwa bahasha zao, business as usual, usipokuwa mkali uletewi fungu lako wanakula wakubwa tu juu kwa juu.
   
Loading...