Mohamed Dewji ni mmoja ya Mabilionea watano Afrika, sijawahi msikia kwenye Kashfa

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
Mohamed Dewji ni kijana Mtanzania mwenye asili ya Asia ambaye amekuwa na Utajiri mkubwa sana. Kijana huyu amekuwa katika 5 Bora ya Matajiri Afrika.

Nimekuwa nikijiuliza Chanzo cha Utajiri wake ni nini. Lakini binafsi sijawah msikia kwenye kashfa kama walivyo akina.... Ambao wamekuwa wakichukua tenda kifisadi na kuwanunua wanasiasa. Kijana huyu sijajua kwa jimboni kwake kuna maendeleo kias gani lakini kama ni mtu ambaye hajahusika na ufujaji katika taifa hili. Yafaa kumsupport kwa kiasi kikubwa.

Alikuwa Mbunge sina uhakika kama alishastaafu au anaendelea.
 
Mohammed Gulam Dewji (born 8 May 1975) is a Tanzanian businessman, entrepreneur, philanthropist, and former politician. He represented the Singida Urban constituency in the National Assembly from 2005 to 2015;[2] when he announced that he was resigning from active politics.[3] He owns 75% of MeTL Group and serves as its Chief Executive Officer.[1]

In March 2015 Forbes magazine named him as the 31st richest person in Africa, with his net worth an estimated US $1.25 billion, having also been the first billionaire in Tanzanian Forbes magazine in 2013.[4][5]
Source: Encyclopedia
 
Huyu makampuni yake ni mabingwa wa kupakia bidhaa zilizopitwa na wakati na kuwekwa kwenye mifuko mipya. Ni mbaya zaidi kuliko hao unaoita mafisadi.

Huyu mtoa mada hajui,na anajua kabisa kama hajui ila hataki kuuliza ili ajue. Bora apige kimya tuu kuliko kusifia asivyovijua.

Mtoa mada hebu ni tajie tajiri mmoja tuu Duniani aliyetajirika bila scandle. Usinitajie inventors.
 
Nenda kawaulize wafanyakazi wake juu ya maslahi na wanavyokuwa treated alafu urudi!
 
Sasa kama hata haujui kama bado ni mbunge au laa? Utawezaje Kujua kashfa zake? Na kama hujui hata jimbo alilokuwa analiongoza kama kuna maendeleo unawezaje kusimama mbele za watu na kusema hujawahi msikia kwenye kashfa? Kiufupi huna habari zake zozote ziwe nzuri au mbaya kwa hiyo huwezi msemea kwa lolote!
 
Mleta post hakuna unachokijua.......kaongee vizuri na wafanyakaxi wake, hasa wale wa viwandani.
 
Mzee gulam baba ake kamwachia mo aongoze kampuni... Baba ni mzima ofisi yake ipo city centre jengo moja refu hapo posta
 
Sasa kama hata haujui kama bado ni mbunge au laa? Utawezaje Kujua kashfa zake? Na kama hujui hata jimbo alilokuwa analiongoza kama kuna maendeleo unawezaje kusimama mbele za watu na kusema hujawahi msikia kwenye kashfa? Kiufupi huna habari zake zozote ziwe nzuri au mbaya kwa hiyo huwezi msemea kwa lolote! Hivi hizi shule mlienda kusomea ujinga au? Au ndio nyie TCU iliwapitisha kimagendo hadi Ndalichako akaja watumbua jipu?
Mkuu, nakuunga mkono; kama eti hajui kama bado mbunge au laa anawezaje kujua mambo yaliofichika ya huyu mtu?
 
Ule mchele mbovu uliosababisha yaliyomkuta Mkemia mkuu wa serikali sijui uliua wangapi na kutupa maradhi ya kudumu wangapi.
Nchi hii ukiona mfanyabiashara anajiingiza kwenye siasa au kuwa mfadhili wa chama tawala mwangalie kwa makini lazima kuna jambo nyuma yake. Tena zito kabisa
 
Back
Top Bottom