Hii nafasi ya Mohamed Dewji huko Afrika Kusini ni kubwa sana

Thadei Ole Mushi

Verified Member
Oct 13, 2018
30
150
HII NAFASI YA MOHAMED DEWJI NI KUBWA SANA.

Na Thadei Ole Mushi.

Kwa Tanzania leo habari kubwa ingetakiwa kila mahali iwe ni Mohamed Dewji kuteuliwa kuingia kwenye Jopo la washauri watano watakaomshauri Rais wa Africa Kusini kuhusu Masuala ya Uwekezaji na Uchumi.

Taifa la Africa kusini ni Mojawapo ya Taifa kubwa kabisa KIUCHUMI Africa. GDP yake ni USD 317.19 bilioni nyuma ya Nigeria. Hivyo Mo anaenda kushauri Taifa la pili kwa Uchumi mkubwa Africa. Hili sio Jambo Dogo kabisa.

Mohamed Dewji (Mo) kwenye Rank ya matajiri Duniani anaingia nafasi 1931 na kwa Africa anashika nafasi ya 13. Kubwa zaidi kwenye nafasi hizo ni kwamba Kwa Africa ndiye bilionea mdogo kuliko wote akiwa na umri wa Miaka 45. Mo kashinda awards nyingi Sana za kibiashara na huenda sifa hizi ndizo zilizomfanya Ramaphosa aone umuhimu wa kumfanyia kuwa mshauri wake.

Nini kinaenda kutokea.

Kwa Sasa hivi Taifa lolote linalotaka kwenda kuwekeza Africa Kusini lazima likutane na Timu hii ya watu watano akiwemo MO. Yaani hata Tanzania ikitaka kwenda kuwekeza Africa Kusini Rais akienda kuongea Hilo dili na delegation yake Basi Mezani watamkuta Mo.

Vivyo hivyo Africa Kusini ikitaka kwenda kuwekeza nje lazima Timu hii ya watu watano akiwemo MO washauri kabla ya Rais Ramaphosa hajaamua.

Si hivyo tu kwa Sasa Mo ataingia vikao vyote vya Serikali ya South Africa ambavyo vinahusu biashara na Uwekezaji.

Vile vile Mo atakuwa na Fursa ya kukutana na VIONGOZI wengi Sana wakiwemo Marais nje na ndani ya Africa. Yaani pale ambapo asingeweza kuingia Kama mfanyabiashara Sasa ataingia Kama msaidizi wa Rais wa Africa Kusini.

Pia Mo anapata Fursa ya kwenda kuwekeza Africa Kusini ni sawa na Kwamba Ramaphosa kamtega Mo kwa nafasi hii.

Hii ni nafasi kubwa Sana kwa mtanzania Mwenzetu huyu. Pia tuna la kujifunza toka kwa Mo kuchukua watu waliofanikiwa na waliopo kwenye Field kushauri mambo yanayowahusu.

Kwa wafanyabiashara wengine Wana la kujifunza hapa kwa Mo.

Akili kubwa ni Mali ya Rais zitumike kwa manufaa ya nchi.

Ole Mushi
0712702602

images.jpeg
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,084
2,000
Wampe na uraia wa huko sisi tuwachwe kama tulivyo. Kama tunateka watu, tunauwa mbona tupo na maisha yanaendelea.

Utajiri wa mtu hautufanyi kudhalilika maana ukizikwa huendi na sanduku la hela, fikiria ujiongeze sio mnapapatikia visheti wakati hata halua ina utamu.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
8,468
2,000
Yaani hapo jamaa anachotaka ni MO kuwekeza south Africa, Sisi watu kama hawa tulikuwa tunawapiga nyundo, kuwateka, na kutaka waishi kama mashetani, Manji kakimbia nchi sababu ya personal issue tu ambazo ni za kawaida, mnakaa meza moja mnasameheana mnajenga Tanzania moja.
Halafu unakuta walio mfanyia hujuma wenyewe mfano yule Daudi Albert Bashite na Mzee wake aliyefariki, ni useless tu!

Mbona Rostam Aziz wamemsafisha! na kumpokea kama mwana mpotevu, na wakati hana tofauti yoyote ile na Yusuph Manji?
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,869
2,000
Mo ana akili nyingi mno, kampuni ya familia toka baba yake amkabidhi u MD kaipaisha kampuni juu hasa.

Baba yake alimwandaa vizuri kwa kumsomesha best schools na vyuo ili arudi kuja kuendesha kampuni na alisoma kweli kweli kwa juhudi ya kufa mtu akafaulu vizuri mno akarudi kuendesha kampuni ya familia na kaipaisha hasa mpaka kuwa na Mo brand.

Mitoto mibwege ya mitajiri ngozi nyeusi hasa ya baadhi ya makabila matajiri kama wachaga na wakinga nk wana cha kujifunza hapa. Mitoto unakuta shule haitaki inadeka deka tu ohhh mzazi tajiri shule inasomea mingine basi tu kinyoge pass za hovyo ipoipo tu.

Mzazi mwenye business akizeeka au kuugua au kufa kampuni linayumba au kufa kabisa wakati mitoto ipo inatoa mimacho tu kama mijusi iliyofiwa na mkwe wao haina msaada wowote kwenye kampuni zaidi ya kusubiri mzazi afe ianze kutwangana kugawana mali badala ya kuiendeleza hiyo business wawe wanagawana faida.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
6,615
2,000
Jamaa anaweza kupata experience huko atakayoileta hapa kwetu naamini hii serikali mpya itakuwa tayari kupokea ushauri wake.
 

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,160
2,000
Yaani hapo jamaa anachotaka ni MO kuwekeza south Africa ,Sisi watu kama hawa tulikuwa tunawapiga nyundo , kuwateka , na kutaka waishi kama mashetani , Manji kakimbia nchi sababu ya personal issue tu ambazo ni za kawaida , mnakaa meza moja mnasameheana mnajenga Tanzania moja ...
Ujumbe mkubwa kuliko wote ni huu.

"AKILI KUBWA NI MALI YA RAIS, ZITUMIKE"

Kwa bahati mbaya sana, mbaya sana yani huku kwetu akili kubwa ni adui
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
47,263
2,000
Yaani hapo jamaa anachotaka ni MO kuwekeza south Africa ,Sisi watu kama hawa tulikuwa tunawapiga nyundo , kuwateka , na kutaka waishi kama mashetani , Manji kakimbia nchi sababu ya personal issue tu ambazo ni za kawaida , mnakaa meza moja mnasameheana mnajenga Tanzania moja ...
Well said
 

Nziiri

JF-Expert Member
Jul 23, 2020
448
500
Ujumbe mkubwa kuliko wote ni huu
"AKILI KUBWA NI MALI YA RAIS,ZITUMIKE"

Kwa bahati mbaya sana,mbaya sana yani huku kwetu akili kubwa ni adui
Sikupingi, ingependeza zaidi kuwa, 'AKILI KUBWA NI MALI YA TAIFA' au ' AKILI KUBWA NI MALI YA JAMII'
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
29,637
2,000
Mo ana akili nyingi mno, kampuni ya familia toka baba yake amkabidhi u MD kaipaisha kampuni juu hasa

Baba yake alimwandaa vizuri kwa kumsomesha best schools na vyuo ili arudi kuja kuendesha kampuni na alisoma kweli kweli kwa juhudi ya kufa mtu alafaulu vizuri mno akarudi kuendesha kampuni ya familia na kaipaisha hasa mpaka kuwa na Mo brand

Mitoto mibwege ya mitajiri ngozi nyeusi hasa ya baadhi ya makabila matajiri kama wachaga na wakinga nk wana cha kujifunza hapa.Mitoto unakuta shule haitaki inadeka deka tu ohhh mzazi tajiri shule i adomea mingine basi.

Mzazi mwenye business akizeeka au kuugua au kufa kampuni linayumba au kufa kabisa wakati mitoto ipo inatoa mimacho tu kama mijusi iliyofiwa na mkwe wao haina msaada wowote kwenye kampuni zaidi ya kusubiri mzazi afe ianze kutwangana kugawana mali badala ya kuiendeleza hiyo business wawe wanagawana faida
Umezunguka kote lakini nia ni kuwa dis Wachaga. Hivi nyie Wasukuma hawa Wachaga wamekukoseeni nini? Hivi ukimchukia tajiri ndiyo umasikini wako utaondoka?
 

Oculus

JF-Expert Member
Apr 21, 2014
915
1,000
Aende tu, hata wakimpa uraia ni sawa kabisa.

Tukija nyumbani, MeTL Group of Company ni wajanja na matapeli wa haki na stahiki za wafanyakazi wao, hivyo CEO naye ni sahihi tukimuita tapeli.
 

NORTHERNIST

JF-Expert Member
Feb 10, 2021
200
250
Nafasi aliopata MO ya kuwa kwenye timu ya kumshauri Raisi wa South Africa kwenye uwekezaji na uchumi ni kubwa sana na pia ni heshima kwa taifa letu tujifunze kuwatumia watu wenye akili kubwa kwa maendeleo yetu sio kukaa tu kuona potentials wanachukuliwa na kwenda kufaidisha mataifa mengine. Naamini Mo ni mzalendo kuwepo kwake kwenye timu kubwa kama ile exposure yake itaongezeka ambapo atatkuja kutumia hapa kwetu. nahitimisha kwa viongozi wetu wachukulie hili jambo kama lesson tuwatumie hawa wenzetu wenye mafanikio kwa maendeleo yetu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom