Forbes Yatoa orodha ya matajiri wapya Aliko Dangote na Mo Dewji miongoni mwa watu matajiri zaidi barani Afrika 2022

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Licha ya mlipuko wa virusi vya corona , watu matajiri barani Afrika wameongeza utajiri wao zaidi ya walivyokuwa miaka minane iliopita.

Mabilionea wa bara hili kwa jumla walijipatia $84.9 bilioni ikiwa ni asilimia 15 zaidi ya utajiri wao miezi 12 iliopita na kwamba ni dadi kubwa iliojumlishwa tangu 2014 ambapo kulikuwa na mabilionea 28 kulingana na jarida la Forbes.

Kupanda kwa bei za hisa kuanzia Nigeria hadi Zimbabwe kuliongeza utajiri wa wafanyabiashara hawa kutokana na ongezeko la mahitaji ya simiti hadi bidhaa za kujifurahisha.

Jarida la Forbes lilitumia bei za hisa na thamani ya ubadilishanaji wa sarafu kuanzia Januari 19 2022 ili kupima utajiri wao.
Mabilionea kutoka mataifa saba ya Afrika waliorodheshwa katika orodha jiyo.

Afrika Kusini na Misri ndio mataifa yenye mabilionea wengi- nchi zote mbili zikiwa na mabilionea watano kila mmoja zikifuatiwa na Nigeria yenye mabilionea watatu.

Katika Orodha hiyo , bilionea Aliko Dangote aliongoza kwa mara nyengine barani Afrika akiwa na utajiri wa thamani ya $13.9b .

Utajiri wa mtu mwenye utajiri mkubwa zaidi barani Afrika uliongezeka kutoka $12.1 billioni mwaka uliopita hadi kufikia takriban $13.9 billion kulingana na jarida la Forbes.

Forbes imesema ukuwaji huo unatokana na ongezeko la bei za hisa za kampuni ya simiti ya Dangote ambayo ndio mali yake yenye thamani zaidi.

Katika nafasi ya pili ni bilionea wa Afrika kusini Johann Rupert ambaye alipanda kutoka nafasi ya nne mwaka jana.

Asilimia 60 ya hisa zake za kampuni yake inayotengeneza saa za Cartier watches na Montblanc ziliongeza utajiri wake na kufikia $11 billioni kutoka $7.2 billioni mwaka mmoja uliopita akiwa ndiye mfanyabiashara aliyefaidi pakubwa katika orodha hiyo.

Mfanyabiashara wa Afrika Kusini Nick Oppenheimer, ambaye ndiye aliyekuwa mmiliki wa kampuni ya kuchimba madini ya almasi ya DeBeers kabla ya kuiuza kwa kwa kampuni ya Anglo American muongo mmoja uliopita alichukua nafasi ya tatu akiwa na utajiri wenye thamani ya $8.7 billion.

Bilionea aliyefaidika zaidi kwa asilimia kubwa alikuwa Strive Masiyiwa wa Zimbabwe aliyepanda juu kwa asilimia 125. Utajiri wake ulipanda kutoka $1.2bilioni hadi $2.7 bilioni mwaka uliopita.

Hisa zake za kampuni ya Econet Wireless Zimbabwe, ambayo alianzisha zilipanda kwa asilimia 750% katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita , zikimsaidia kuongeza thamani ya utajiri wake .

Mfanyabiashara wa Nigeria Abdulsamad Rabiu, amejiongezea utajiri wa $1.5 billioni baada ya kutangaza hisa za kampuni yake kwa umma.

Mapema mwezi Januari 2022, Rabiu aliweka hisa za kampuni yake ya chakula BUA Foods katika soko la hisa la Nigeria. Yeye na mwanawe waliendelea kumiliki asilimia 96 ya hisa za kmapuni hiyo.
Mohammed Dewji wa Tanzania, ambaye utajiri wake ulipungua hadi wastani wa dola bilioni 1.5 kutoka dola bilioni 1.6 mwaka mmoja uliopita.

Mabilionea wote walikuwa wanaume huku mwanamke wa mwisho kuorodheshwa akiwa Isabel Dos santos wa Angola ambaye aliondolewa katika orodha hiyo ya watu matajiri Januari 2021.

Orodha ya watu matajiri barani Afrika 2022 na thamani yao

1.Aliko Dangote $13.9b

2.Johann Rupert & family $11b

3.Nicky Oppenheimer & family$8.7b

4.Nassef Sawiris $8.6b

5.Abdulsamad Rabiu $7B

6.Mike Adenuga $6.7b

7.Issad Rebrab & family $5.1b

8.Naguib Sawiris $3.4b

9.Patrice Motsepe $3.1b

10.Koos Bekker $2.7b

10.Strive Masiyiwa $2.7b

12.Mohamed Mansour $2.5b

13.Aziz Akhannouch & family $2.2b

14.Michiel Le Roux $1.7b

15.Othman Benjelloun & family $1.5b

15.Mohammed Dewji$1.5b

15.Youssef Mansour$1.5b

18.Yasseen Mansour$1.1b
 
Duh ndugu zake Samia Kikwete Muhamed said na Faiza fox ndug zao kwenye list ya matajiri 18 Afrika wao wametoa 11 duh jamaaa masking Sana hawa
 
Huyo MO DEWJ.. kwani hawezi kugawa buku kumi kumi TANZANIA nzima huyo.. aongeze upendo tu kwa watanzania sio mbaya
 
Dah kwenye iyo list kobaaz wako 11, sisi wagalatia wanne tu. Kobaaz wanachanja mbuga tu.
 
Back
Top Bottom