Mohamed Dewji (MO) aliyepotea, apatikana. Amerudi nyumbani akiwa salama

Yajayo yanafraisha mkuu,, Ni kuumbuka kwa kwenda mbaliiii zaidi Unajuwa kila kitu kina mwanzo na kati then mwisho
Waswahili husema ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka, Huenda wasiojulikana wako mbioni kujianika
 
Polisi bora mngebaki na hekaya hiyo hiyo ametupwa JIMKANA ila mlivyongezea amerudishwa na gari lile lile ndio mmezidi kuharibu,GYMKHANA kuna ulinzi wa kutosha pale na kuna Temporary kituo cha polisi inakuwaje TOYOTA SURF yenye WATEKAJI WAZUNGU WANAONGEA KIZULU wapite bila kusimamishwa? Hiyo TOYOTA SURF IMEPITA Hapo hapo kituo cha SALENDA? Au ilipita WIZARA YA MAMBO YA NDANI KWENDA GYMKHANA?
Bora ingekuwa Vitz,hilo Toyota picha yake ilikuwa mtandaoni na linatafutwa
 
Tumezoea kumuona Humphrey Polepole akiitisha press conference kufafanua jambo hata kwa issue ndogo ndogo tu, lkn tangu Mohammed Dewji atekwe takribani siku kumi, si Polepole wala Bashiru wala Mwenyekiti wa chama aliyejitokeza kuzungumzia tukio hili.

Tulitegemea CCM kama chama kongwe ionyeshe mfano kwa vyama vingine jinsi ya kuwa karibu na wanachama wake pindi wanapopata matatizo lkn imekuwa ndivyo sivyo.

Leo mtaenda kumwambia nini Dewji, mtaiambia nini familia yake na mtawaambia nini wanachama wenu na watanzania kwa ujumla.

Mmekosea, mtaonyesha ukomavu wa kisiasa kama chama kikikiri kuwa kimekosea, kukiri kosa siyo unyonge bali ni ujasiri.
 
Hii inaonyesha familia wamelipa ransom!

Moja ya masharti ya ransom ni kutozungumza kuhusu tukio lote!

Kama atazungumza kuhusu yaliyomsibu mpaka akarudi basi hiyo itaonyesha kuwa hakulipa ransom na hakuna makubaliano.

Hoja iliyopo mbele yetu kwa sasa, Je, kama amelipa ransom, nini kwa sasa nafasi ya matajiri nchini kuhusiana na usalama wao kwa sababu kulipa ransom ni kufungua mlango wa biashara ya kidnapping and ransom nchini kwa matajiri.

Kosa la kulipa ransom baada ya kutekwa ambalo nchi za kusini mwa Afrika kama Afrika Kusini na Msumbiji walilianza kwa matajiri ndilo kwa sasa linazidi kuwatafuta kwa kasi zaidi.

Je, kuna uwezekano na Tanzania tukaelekea ambako nchi za kusini mwa Afrika ziliko kwenye biashara ya kidnapping and ransom?
Ina maana unajifanya hujui Mo alitekwa na nani?
Really? Seriously?
 
me naomba kujua jesh la polis alifanyi kaz ipasavyo.. jana igp sirro kaongea sana na gar lilohiska kumteka mo limeonesha mpka plate number na wamedai ni la nchi jiran hapo wamechunguza sna.. mpk hayo majibu tumepewa jana... haya ssa gari lilihusika kumbe sio ni gar la hapa hapa tz.. ndo tunatka kusema jeshi letu bdo sana kwenye uchunguz.. ila igp sirro aje tu tena aite waandsh wa habar ATUOMBE RADH WATANZANIA WOTE KWA KUTUDANGANYA NCHI NZIMA
Hawezi kuja kwani hata yeye mwenyewe alikuwa ameandaliwa cha kutueleza kabla ya kumuachia MO. Hata yale maelezo ktk simu ya MO sio yeye mwenyewe bali walitwit kwa niaba yake. NI AIBU KWA JESHI LA POLISI NA NI AIBU KWA SERIKALI NA NI AIBU KWA NCHI YETU. Mimi ningemshauri Jiwe aachane kabisa na mtoto pendwa kwani tutakuja kuyashuhudia mengi na makubwa zaidi ya haya.
 
Ndugu wanabodi,
Ukiiangalia press ya IGP kisha ukaangalia majigambo ya Mambosasa akinesha gari iliyotajwa na IGP kuwa imepatikana na MO akiwa salama kabisa lazima utagundua kuwa kuna picha imechezwa hapa
Lakini yote kwa yote tumshukuru Mungu MO kapatikana salama
Aksante.
 
kwa mtazamo wangu swala hili litaisha kama la Roma mkatoliki. mo mwenyewe atakavyotoa majibu mtashangaa. subirini..
 
Duh hawa watekaji kiboko wanaroho ngumu sana ...wakamrudisha na gari ile ile mpaka gymkana?!
 
Brother Mo, kama unanisoma ni hivi

ULIFANYA LA MAANA SANA KUWEKEZA KWENYE SIMBA SPORTS CLUB, WANASIMBA WOTE BILA KUJALI VYAMA VYAO TULIKUWA NYUMA YAKO.

Na laiti usingekuwa mmiliki wa Simba, Watu wasingekujua, Wasingefuatilia kutekwa kwako, Wasingepaza sauti waliyopaza!. Yaani nakueleza wazi brother Mo, Kwa mara ya Kwanza wale jamaa hatukwaelewa kabisaaa Stori na Matango Pori waliyotulisha!

SIMBA NGUVU MOJA!!!
Acha utoto Mkubwa, mbona hata Mimi mwana Yanga nilihuzunika na sasa nimefurahi kupatikana kwake? Mamipira yako yasikutoe akili,pale ilikuwa ni ishu ya afya na uhai Wa mtu ndugu. Tajiri Mkubwa kama huyu hata bila simba na Yanga angestua watu na kumbuka aliwahi kuwa MP
 
Back
Top Bottom