Naona kuna kitu ulitaka kusema ukazunguka mwishoe ukasema.kama kitu huna ujuzi nacho basi usikulupuke kukifanya,naona umepata muda wakuandika ila umekosa muda wa sekunde chache hata ku google kupata maana ya hilo neno.
Ndio maana waafrika wengi hatuendelei kwa sababu inaweza tukawa ni wajinga au ni uvivu wa kutotaka kujishughulisha/kuchemsha bongo.
Neno KAFIRI ni nomino,kitenzi chake ni kufuru.mtu yeyote atakaye kufuru anaitwa KAFIRI.Je,kukufuru ni nini? Kukufuru kupo kwa aina nyingi mfano (1) kumfananisha mwenyezi mungu na kiumbe chochote au kuufananisha uwezo wake na kiumbe chochote.
(2)kukataa maamlisho yake. Hiyo ni baazi mifano nimekutolea.
Wengi wana usema uislamu vibaya ila kiukweli hawaujui uislamu wenywe,wengi wamemezeshwa uwongo kuhusu uislam basi wamejaa chuki na waislam na uislam bila sa abu yeyote.
Naomba unipe aya inayo sema KAFIRI NI MASIKINI ndani ya quran.maana uislam unaongozwa na quran.