Mobisol engie, kampuni ya sola ya kitapeli nchini Tanzania

bukenyaimo

Member
Oct 21, 2021
99
289
Tanzania ni moja ya nchi iilizofungua milango ili Makampuni mengi yaje kuwekeza nchini kwenye Sekta mbalimbali hususani Sekta ya Nishati.

Moja ya Kampuni hizo ni Kampuni ya Sola ya Engie ambayo zamani ilikuwa ikiitwa Mobisol. Kampuni hii yenye Makao Makuu yake Mkoani Arusha ni Kampuni ya Kitapeli iliyojaa wezi ukianzia kwa Mkurugenzi wake Mkuu Bwana Godfrey Mugambi raia wa Kenya.

Ni Kampuni ambayo inauza bidhaa zilizo na kiwango cha chini tena kwa bei ya juu. Mimi ni mmoja wa wateja wa kampuni hii ambapo waliniuzia mtambo wao wa sola na nikautumia kwa wiki moja tu na kuanza kunisumbua.

Jitihada za kupiga simu huduma kwa wateja zimeishia kupigwa danadana tu kwa kuambiwa mafundi watakuja kunirekebishia tatizo langu bila ya mafanikio na miezi mitatu sasa imepita.

Majuzi amekuja mfanyakazi wa Kampuni hiyo nyumbani kwangu eti anauliza kwa nini silipii huduma (natakiwa kila mwezi niwe nalipia Tsh.31,000), kwa kweli kidogo nimkate na panga maana nalipiaje wakati huduma sipati

Ashukuru nilipoingia ndani kufuata panga alikimbia.

Naiomba Serikali yangu tukufu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kwa Waziri wa Nishati Mheshimiwa Makamba kuifurusha nchini Kampuni hii kwani imekuwa ikitunyonya sana sisi wananchi wa kipato cha chini huku vijijini ambao bado huduma ya Umeme haijatufikia.

Watanzania wenzangu hasa wa vijijini tunaotumia Sola TUPAZE SAUTI KUIKATAA KAMPUNI HII YA KITAPELI YA MOBISOLI

Mheshimiwa Rais nakuomba kwa niaba ya Wananchi wanyonge ongeza juhudi ili vijiji vyote nchini vipate umeme wa Gridi ili tuondokane na UNYONYAJI tunaofanyiwa na Kampuni hii ya Mobisoli.
 
upo sahihi kwamba bidhaa zao ni ghali lakini unaongopa kusema ni low quality,mimi ninazo tatu na zote zinapiga kazi,moja imekaa miaka 5.
tatizo la huduma kwa wateja pia huenda upo sahihi,ila kwa gharama wapo juu mno kuna mtambo wa mil 3 na zaidi na ninayo mitambo mitatu ya bei hiyo
 
Kampuni ilikuwa inabidhaa nzuti sana hata mm nilitumia kwa muda mpk nilipolazimika kuhama na kuurudiaha mtambo wao, niliurudiaha ukiwa kama mpya maana mm nilikuwa mtunzji sana,
Ila nahofia huenda kuna mitambo inayorudishwa pia na wateja wengine ambao si watunzaji na inakuwa resold kwa mikataba mipya, sasa tatizo linaweza kuanzia hapo kwa mtazamo wangu,
 
Nimeapa akija ofisa yeyote wa Mobisol nyumbani kwangu kuuliza kwa nini silipii na kujifanya anataka kuondoka na Mtambo lazima mapanga yahusike nikafie Jela nawaonya nyie majizi Mobisol maana naamini uzi huu mnausoma
 
Ndio,huku kwetu Kijijini hakuna umeme hivyo Sola haziepukiki,sasa hii Kampuni ya Mobisol ni majizi na matapeli ya kutupwa,yao yanajua kufuatilia wateja kukumbushia walipie bila kujali wamepata huduma kikamilifu au hawajaipata,ni majizi kama majizi mengine tu
 
Hao jamaa ni wezi wa kutumia janja janja na uzezeta wa raia pamoja na serikali yenu nyinyi wabongo.
Bidhaa ya 40,000/=mnauziwa kwa 290,000 kwa mkopo na ndani ya mwaka muwe mmemaliza deni,mabwege mna miaka milioni mia ya kupigwa,kaeni kwa kutulia kazi bado mnayo.
 
Tunaendekeza anasa sana kwa kutumia solar na umeme wakati mababu zetu karne na karne waliishi kwa kutumia kuni na mbalamwezi na maisha yalienda na walikuwa na furaha sana.
 
Back
Top Bottom