Jamani kwa nini mawasiliano yako yawe ni siri??? Kuna kitu gani unaficha??? Nafikiri majambazi ndiyo watataka kuficha mawasiliano yao?? I mean jambazi katika nyanja zote (wazinzi, silaha, bila silaha, vibaka, you name all!!!). Unahofia nini kama mambo yako ni safi?? Mtu anaogopa kumpa mke/mume/mtoto simu yake!!!! Aibu hii.
Vipo vingi tu ambavyo haviusiani na uvunjaji wa sheria, ambavyo watu wengine wanavyo nawasingependa ku-share na wengine. Kama wewe huna basi ni vizuri, lakini usi-assume kwa sababu wewe huna basi kila mtu mwingine anatakiwa asiwenavyo.
Kwa mafano uko likizo na mfanyaazi mwenzako anakuomba username na password ya router yenu. Au mawasiliano kati ya whistle blowers na wanaopelekewa taarifa. Ukifikiria nje ya box kuna mifano mingi tu, sema unaona yale ya hovyo tu pengine kwa sababu ndiyo yaliyo kichwani kwako.