Mobile Money Transfer,kuna siku itakula kwetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mobile Money Transfer,kuna siku itakula kwetu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by mfianchi, Feb 9, 2011.

 1. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Kukua kwa teknolojia siku hizi kumerahisisha mambo mengi,moja wapo la hayo mambo ni uwekaji au uhamishaji wa fedha kwa kutumia kampuni zitoazo huduma za simu za mkononi,lakini kila jambo zuri lisipokuwa na uangalizi hatimaya yake ni kuwa kama DECI,karibu kampuni zote kubwa za huduma za simu za mkononi hufanya shughuli za kuhamisha au kuhifadhi fedha,mamilioni ya shilingi hupita katika hayo makampuni kila siku,tatizo langu ni kuwa je hizo shughuli zina sheria yoyote inayoziendesha kwani nilitegemea benki kuu kuwa msimamizi wa hizo shughuli za mamilioni ya pesa yanayopita nje ya utaratibu wa sheria za fedha,na je pale kampuni ya simu ikafilisika au ikafungasha virago je watu walioweka pesa zao watazipata wapi?na wataenda kudai wapi.Maoni yangu ni kuwa benki kuu iiweka utaratibu utakaofuatwa na kampuni zote,kwa benki kuu kukaa kimya na kujifanya hamnazo ni kukaribisha DECI mpya,au mpaka watu waje lizwandio benki kuu itatoka usingizini?
   
 2. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,362
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Mkuu hii ni Bongo.
  our management in public sector are always managing by Fire Fighting .yaani kila atendacho mkuu wa taasisi ya umma huwa ni maelekezo ya dharura.so the tamko la mkuu huwa linashuka hadi chini kwa watendaji kwa mfumo wa kidharura dharura... bongo hamna planing inayofuatwa,kwa kawaida watu wanaenda bagamoyo kuandaa plan yao ya mwaka,then wakirudi hamna hata chembe ya hiyo plan inayofuatwa.

  nikirudi kwenye mada yako ya BOT na pesa za Mobile Transfers i.e ZAP,M-Pesa,Tigo Pesa and Zantel pesa ,hapa BOT wanatakiwa wawe makini,watunge Guide lines ,na kupendekeza sheria ili zipitishwe na bunge kuhusu swala zima la E-commerce .
  tuwe na platform moja ya kutumia e-money.
   
 3. O

  Oshany Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa kuletwa hoja hii, ni jambo la muhimu kuwa na uangalizi kwenye hizi aina mpya ya biashara. Nadhani kwa kuna umuhimu wa BOT kwa kushirikiana na TCRA kuangalia kwa pamoja suala hili. Sababu ya kutoa ushauri huo ni kuwa biashara hii inahusu masuala ya pesa (BOT) na masuala ya mobile communications (TCRA).
   
Loading...