monomotapa
JF-Expert Member
- Oct 30, 2012
- 437
- 325
Mama wa mabomu yote duniani (Bomu ambalo halina mahusiano na nuklia) - Massive Ordinance Air Blast bomb AKA Mother Of All Bombs (MOAB) lenye uzito wa kilogram 10,300, (22,600lb) na ujazo wa tani 11 za milipuko (TNT) lililotengenezwa mwaka 2003 huko Marekani limetumiwa hivi karibuni na kikosi maalum cha wanajeshi wa anga wa Marekani" Special Royal Air Force" huko Aghanistan na kuwaua magaidi zaidi 92 wa kundi la ISIS, Shuhuda wa Kiafghanistan alielezea kuwa mlipuko wa MOAB ilikuwa kama mbingu zinaangukia dunia...(I felt like heavens were falling) Msemaji wa serikali ya Marekani akielezea CNN anasema MOAB imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa na kiwango cha juu cha shabaha (Precision) na kutimiza lengo lililo tarajiwa (Target) mashambulizi ya jeshi la marekani Syria na Afghanistan na kuelekeza manowari zake kwenye ukanda wa ghuba ya Korea ni ujumbe tosha kuwa Marekani imerudi kwenye nafasi yake tena duniani " US is back again"