Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni: PPF yasifiwa na wastaafu kwa kulipa pension ya kila mwezi kwa wakati

HR wangu aliniingiza kwenye hilo jinamizi pasi na matakwa yangu, Yaani Sina hamu nalo hilo lidubwana! Nina mwaka wa 3 sasa hata Forms zao sijajaza!

Hii pressure ya kuunganishwa mifuko ndio itanipeleka nikajaze form za usajili!
 
Sawa mkuu, hii niliyozungumzia ni ya PSPF,sina hakika ya mashirika mengine.
PSPF wako vizuri. Ila mtoa mada alisema PPF ndiyo maana nilidhani unazungumzia hiyo. PSPF lump sum iko poa ila ya kila mwezi si kubwa na ndiyo wanajivunia PPF kuwa wao ya kila mwezi ni kubwa. Bora yaunganishwe tu wote tupate sawa yaani formula moja.
 
HR wangu aliniingiza kwenye hilo jinamizi pasi na matakwa yangu, Yaani Sina hamu nalo hilo lidubwana! Nina mwaka wa 3 sasa hata Forms zao sijajaza!

Hii pressure ya kuunganishwa mifuko ndio itanipeleka nikajaze form za usajili!
Jaza tuu hamna namna ila mimi hao siwataki tena
 
Sasa kama unamuambia asijitumbukize huko, alternative ni nini?Kumbuka itafika mahali ajira itakoma,sasa ajira ikikoma na hana chochote, itakuwaje?Lets share.
Ppf hupati kabisa mafao yako mpaka uzeeni lakini nssf wanakupa ingawa utapitia usumbufu sasa bora wapi ingawa hata hao nssf hawana maana
 
PSPF wako vizuri. Ila mtoa mada alisema PPF ndiyo maana nilidhani unazungumzia hiyo. PSPF lump sum iko poa ila ya kila mwezi si kubwa na ndiyo wanajivunia PPF kuwa wao ya kila mwezi ni kubwa. Bora yaunganishwe tu wote tupate sawa yaani formula moja.
Sawa mkuu.Ila PPF wamesifiwa kwa kutoa mapema pension ya kila mwezi,ila kwa pension ya lumpsum na ya kila mwezi ni kweli sio wazuri sana.

Hata hivyo formula ya kukotoa lumpsum imebadilishwa PSPF kwa mikataba mipya, kwa hiyo take home huko nako inasemekana imeshuka accordingly, kwa pension ya lumpsum na kila mwezi.

Mkuu sijui kama kuunganisha mashirika kutaboresha pension ya lumpsum na ya kila mwezi, ngoja tusubiri March.Hata hivyo haya ndiyo kati ya mambo ambayo wanachama wanapaswa kushirikishwa ku-arrive at,lakini kwa bahati mbaya wamewekwa pembeni kabisa,things are just being imposed on them,pathetic.
 
NSSF walijaa wezi na wapiga deal. Wamekula sana kupitia miradi hewa waliyobuni nchi nzima. Sasa wanachama watawalipaje?
 
Ppf hupati kabisa mafao yako mpaka uzeeni lakini nssf wanakupa ingawa utapitia usumbufu sasa bora wapi ingawa hata hao nssf hawana maana
Mkuu ni sawa kuna wakati mtu unajitoa katika mkataba na shirika lako la jamii kwa sababu zisizoweza kuepukika na labda ungependa upate fao la kujitoa kufuatana na mkataba wako.Kwa bahati mbaya ni kwamba fao hili limetolewa kwenye mashirika mengine na ni kweli inaudhi na inakatisha tamaa.Hata hivyo ni vema tukakumbuka kwamba mziki upo baada ya kustaafu.Mkuu unapokuwa na nguvu zako you can maneuver around ukaishi.Hali ni tofauti kabisa unapokuwa mzee!Ushauri wangu ni kwamba tuangalie zaidi maisha ya uzeeni,hapa katikati sio issue sana.Kwa hiyo pamoja na matatizo mbali mbali yaliyopo kwenye mashirika ya kijamii,ni muhimu tukajiunga nayo and fight for our rights from within.Umoja ni nguvu.
 
tarehe 20 kweli
 
Kabisa mkuu. Walitakiwa watushirikishe wastaafu watarajiwa. Wanapanga tu. Nasikia take home ya lumpsum imepunguzwa to 32% badala ya inayotolewa sasa hivi ya 50%. Yaani tunaibiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…