Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake apewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Dec 20, 2011.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Dec 20, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna msemo mmoja wa kiswahili unaosema hakuna marefu yasiyo na ncha.Kila jambo lina wakati wake na wakati ni ukuta ukishindana nao utaumia.Imenilazimu kutumia misemo hii maarufu ya kiswahili nikiwa na maoni na masikitiko yangu juu ya chama hiki cha NCCR MAGEUZI.

  Napata ugumu kuamini kinachajiri na hatima ya chama hiki.sitaki kuamini malengo makuu ya chama hiki ni kusindikiza wenzake katika vinyang'anyiro vya kuwaongoza wananchi wa nchi hii.

  Kila mmoja ni shahidi kwa umaarufu wa chama hiki mwanzo wa mfumo wa mageuzi nchini mwetu.Kilikuwa chama kilchoonekana kuwa chama mbadala chenye uwezo wa kuchukua dola mwaka 1995,kilikuwa ni chama makini na watu makini katika kuapanga mikakati ya kukikuza chama hiki.

  Sitaki kuamini busara za akina Dr.Haider Magutto zilizikwa mara baada ya kufa kwake. Sitaki kuamini nguvu kubwa na hoja madhubuti zilizojengwa na akina Mabere Nyaucho Marando zimepotea.

  Chama hiki cha NCCR MAGEUZI imekuwa taasisi kama ya kifamilia zaidi kuliko nia na madhumuni ya kuanzishwa kwake.Nakumbuka sana matafaruku mkubwa uliotokea kipindi cha Mh. Mrema lakini ulidhibitiwa kwa hekima kubwa,leo hii nini kimewakumba hata kuondokewa na uvumilivu ule? Wananchi waliamini kijana akipewa madaraka anaweza, sasa napata sana taabu kuamini hivyo ikiwa vijana ndo wanatumika kuumizana wao kwa wao ilikodhoofisha harakati za kujenga demokrasi ya kweli ndani ya taifa letu.

  Mh. Kafulila ni kijana mdogo aliyeingia NCCR na kuamsha matumaini mapya kutoka katika usingizi mzito uliokuwa umekikumba chama hicho,lakini leo hii wanathubutu bila haya kumuondoa katika chama katika wakati mgumu wa mapambano dhidi ya haki na batili ndani ya taifa hili.Tuna kwenda wapi ndugu zangu.

  Kafulila na wenzake walitakiwa mawazo yao yaheshimiwe na kufanyiwa uchunguzi wa kina kabla ya kutoa matoke yasiyo na tija zaidi ya kukiangamiza chama.

  Chama kama chama kingepima tuhuma alizotuhumiwa mwenyekiti,ikiwa pamoja na kupima utendaji wa chama na mafanikio ya chama kwa kipindi chake alichokaa madarakani vinaendana na tuhuma hizo?Sitaki kuamini kuwa lile ombwe la fikra limekikumba chama hiki kilichokuwa kipenzi cha wananchi kwenye mika ya tisini.

  Hoja ya kumfukuza mh. kafulila haina mashiko, adhabu aliyopewa ya kumuondoa uenezi ilitosha kabisa kudhibiti nidhamu ya kijana huyu.Nasema haina mashiko na dhaifu kwa kusema amekuwa anatoa maoni yake kupitia vyombo vya habari na kuweka mambo hadharani.Labda niulize!

  Hashimu Rungwe alipotoa tuhuma kuhusu mwenyekiti kumkataza kuzungumzia CCM kwenye uchaguzi ,chama kilimchukulia hatua gani mwenyekiti huyo ilihali akijua fika kuwa mgombe wake yupo kwenye mchuano mkali wa chama chake kushika dola!?

  Chama cha CUF kule Zanzibar kiliwekewa pingamizi na mwenyekiti huyu huyu wa upinzani kiasi cha wagombea wake kuzuiliwa na tume ya uchaguzi kushiriki uchaguzi,chama kilimchukulia hatua gani!?Tunashindwa kuamini kama kweli ni chama cha upinzani kweli chenye kutaka kuleta mabadiliko ya kweli ikiwa ni pamoja na kukiondoa kushika dola chama tawala.

  Mifano ni mingi tu,hata kitendo cha kumpinga mpinzani mwenzake kwenye matokeo ya ubunge ni usaliti mkubwa katika nafasi ya wapinzani kukiondoa madarakani chama tawala.kwanini NCCR hawakuliona hili kama ni ushahidi tosha kumuajibisha mwenyekiti huyu nguli katika siasa za NCCR hapa nchini.

  Tuwe wa kweli na kukubali kuwajibika pale inapoonekana uwezo wa kuongoza umefika kikomo.Zile zama za zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama zimekwisha kupitwa na wakati.Hata waasisi wa kauli mbiu hizo waliziona haziendani na wakati ulipo na ndo maana waliziondoa.Kitendo cha kumfukuza Uanachama Mh. Kafulila mimi nasema ni unafiki na uzandiki unapaswa kupigiwa kelele si tu na wananchi wa Kigoma Kusini bali na wapenda maendeleo wote nchini.

  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.Mpeni haki ya kuchaguliwa na wana wa jimbo lake.Kuwanyima haki zao wananchi wa kigoma za kuletewa maendeleo ni usaliti mkubwa.Shime wana wa Kigoma ni wakati wenu tena kufanya maamuzi ya kina kwa kipenzi chenu,kwani mlimuamini anaweza,japokuwa juhudi zake zimefikishwa ukingoni na chama chenye kuamini fikra sahihi za mwenyekiti wa chama chake.Mkiipoteza nafasi hii ya kumtetea mtumishi wenu deni la usaliti litakuja daiwa na vizazi vyenu.Ule mfumo wa umangimeza ukomo wake umefika.

  Tahadharini wana wa nchi hii,ukombozi unapokaribia ikatoke mmoja wenu wakawasaliti,basi huyu si mwenzenu,mkataaeni kwa vitendo bila kumuonea haya.Pia naulaani mfumo dume wa uchaguzi na sheria kandamizi inayokinzana na katiba juu ya mgombea binafsi.Tanzania bila vyama uchwara inawezekana.Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Afrika.
   
 2. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #2
  Dec 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu afadhali wewe umeliona hilo maana wengine humu wanashabikia adhabu ya Kafulila kwa kufuata mkumbo tu bila kufahamu Kafulila alikuwa anapambana mapambano halali na ya haki!
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  halafu vinapata ruzuku kutoka kwenye kodi zetu.....yet kuna watu hawalioni hili
   
 4. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Well said... ila lazima tutambue chama ni taaasisi na lazima taratibu za uendeshaji wa taasisi husika ziheshimike. Hakuna taasisi inayoweza kuendeshwa bila taratibu hivyo kama taratibu hazifuatwi lazima hatua madhubuti zichikuliwe kwa wanaozikiuka. Kinacho mhukumu huyu ndugu, ni ukiukwaji wa taratibu za chama na kutoa siri za vikao hadharani. majadiliano ya vikao ni siri ya chama na ndio medani za usindani. Ukiweka kila kitu hadharani kwa kila mtu unategemea usindeje ktk ushindani? Hili haliko nccr tu lipo kwa vyama vyote na hata makampuni ya biashara, lazima tulinde siri za taasisi.

  Ni vema pia ifahamike kwamba kuwa wapinzani wamoja haina maana kupoteza haki za kidemokrasia na kisheria. Kama kuna swala la ukiukwaji wa haki au taratibu lazma hatua stahiki zichukuliwe. Hii ndiyo inayofanyika kawe, ndio iliyofanyika zanzibar kwenye uchaguzi wa marudio na ndio inayofanyika kwingineko kote katika kuhakikisha misingi na taratibu zindemokrasia zinalindwa na kugeshimiwa. Kuinyima nccr fursa ya kudai haki yake ni sawa na kumfumania ndugu yako na mtoto wako uache kumshtaki na kumfungulia kesi kwakua tu kufanya hivyo utakua umemshtaki ndugu yako. Huu ni mtizamo potofu. Nccr wana haki ya kudai haki zao popote na dhidi ya yeyote bila kuwekewa mipaka na bila kutafsiriwa vinginevyo.

  Kama kiongozi.. Aliekua mh Kafulila alielewa fika taratibu za chama chake. Alitambua nini kitamkuta iwapo ataenda kinyume cha taratibu, maana taratibu na kanuni za adhabu ziko wazi katika katiba za vyama. Hivyo analipa alilikula na anavuna alichopanda.

  Pamoja na uchanga wake ktk nccr si mchanga sana ktk siasa. Tunakumbukumbu yake ktk chadema, historia pia inatengeneza ushawishi wa kimaamuzi hivyo alipaswa kujitambua, kuheshimu taratibu za chama ili chama na wanachama wenzake waheshimu na kuzingatia maoni yake atakayo toa kwa taratibu muafaka. Hoja nzito nzuri na yenye mashiko inaweza potenza nguvu tu kwakua imetolewa nje ya taratibu. Alipaswa tambua hilo.

  Kafulila amepewa haki yake na amepimiwa kikombe anachostahili. Nifursa sasa kwake kuangalia wapi amejikwaa ajipange upya, bado ananafasi na fursa za kuwatumikia watanzania kama mtanzania mwanasiasa wa kawaida na bado ana nafasi ya kuomba ridhaa ya wananchi wake tena, kupitia chama atakachokimbilia na wakampokea . Kwa kutumia mtandao na mahusiano aliyojenga pia anauwezo wakujenga ushawishi ktkt hoja na maeneo mbali mbali hii pia itakua mchango wake ktk siasa za nchi hii.

  Ubunge ni moja ya mlango mzuri wa kutoa maoni na mchango, ila wigo wa mchango wa maendeleo ya kiuchumi na kisiasa ni mpana na hivyo bado ananafasi yakutimiza malengo. Kama malengo yake nikuleta mabadiliko kwa jamii na si vinginevyo.
   
 5. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Nccr=ccm c
   
 6. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,918
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Binafsi sishabikii adhabu ya kafulila, ila namlaumu kwa kutokusoma alama za nyakati na kupangilia mapambano yake kisayansi zaidi..!
  Kufukuzwa kwa Kafulila NCCR ni pigo kwa wapenda mabadiliko na ni ushindi kwa kikundi kidogo cha mafisadi wa Madaraka.. Ila kwamba amekosea mahesabu ni lazima tukiri. alirusha ngumi nyingi sana hewani kabla ya hata kumfikia adui..
   
 7. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  mapambano gani bila mpango ,hata yeye alikuwa anapambana na wapizani wenzake hata kabla hajapata ubunge ...baada ya kupata unakumbuka aliungana na hamadi rashidi kupindisha kanunu za bunge kuhusu kambi rasmi ya upinzani bungeni ,wote walikuwa na uroho wa madaraka kumbuka maneno aliongea baada ya cdm kutoka nje bungeni huku akishangiliwa na wabunge ccm aah masikini hakujuwa alichokuwa anakipanda yeye na rafiki yake lakini sio mbaya arudi akiatumikie degree yake kujenga nchi kuliko kukaa tu kupiga soga na kula pipi mjengoni

   
Loading...