Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe

Mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe

Oscar M Lungu

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2016
Posts
480
Reaction score
743
Ni mwezi kama huu (July) miaka minne iliyopita nilienda katika mahakama moja katika mkoa fulani hapa Tanzania nikiwa katika pilika pilika zangu za kuomba mkopo kwa ajili ya elimu ya juu. Ilikuwa 2013 wakati huo Rais wetu alikuwa ni mh. Kikwete.

Nakumbuka nilifika katika viwanja hivyo vya mahakama majira ya saa tatu Asubuhi ili kuwahi foleni kutokana na uwingi wa wanafunzi kipindi hicho( tofauti na sasa maana nahisi elimu ya juu imekuwa ngumu kama kupata scholarship ya kwenda kusoma uingereza).

Lakini mungu si athumani nakumbuka siku ile hakukuwa na foleni kwa sababu tulikuwa wachache sana, hatukuzidi watatu, ila ilinibid nisubiri kwa masaa matano ili tu niweze kusikilizwa kabla ya kuhudumiwa na bado at all that time sikuweza kumuona hata receptionist ambae angeweza hata kunipa muongozo wa nini ninachotakiwa nifanye.

Nashukuru mungu wakati ofisi zinakaribia kufungwa niliweza kuonwa na mhusika na kusikilizwa shida yangu...kila karatasi moja ilinigharimu shilingi elfu 3 na mia 5 (x 6 ) with no bargaining ..hutaki toka. Kiasi hiki cha pesa hakikuwa tatizo sana kwa sababu kwenye Tigo Pesa na M pesa jumla nilikuwa na not less than Tsh:470k .

Baada ya miaka minne kupita ( I mean today) muda mfupi uliopita nilirejea tena kwenye mahakama ile ile na almost 85% ya wafanyakazi ni walewale waliokuwa wananishangaa miaka minne iliyopita lakini tofauti yake ni kuwa leo sipo na makaratasi ya loansboard Bali ni vyeti vyangu safi vya level zote na training mbalimbali nilizozipitia katika kipindi hiki chote cha miaka 4.

Nikiwa naelekea usawa wa geti lengo likiwa ni kumfuata mlinzi anipe utaratibu wa kuonana na wahusika , ghafla nikajikuta nashikwa mkono na kusalimiwa , kabla sijajibu salami nikaulizwa shida yangu ,nikajibu then akaniongoza mpaka reception napo sikukaa hata dakika moja nikapelekwa kwa mhusika.

KIPI KILICHONIPA FARAJA?
Ni kwamba leo nimerejea katika ofisi ile huku tigo pesa yangu ikiwa na deni LA shilingi elfu 29845 na M pesa yangu ikiwa imefungiwa kutokana na kutokuwa mwaminifu kwenye M-pawa yao.

Hivyo njia nzima nilikuwa nawaza itakuwa iwapo watahitaji the same amount kama kipindi kile au zaidi. Nilipokuwa nakabidhi vyeti huku nikiwa na wasiwasi ghafla yule mdada akaniuliza unafanya kazi wapi ,? Nikamjibu mie ndio kwanza nimemaliza chuo na am a jobless japo nimefanya bachelor ya education with ICT.

MUDA WA MUUJIZA
Yule mhusika akachukua vyeti na kuvipiga mhuri na sahihi na kunisihi kwamba nilitakiwa niwaeleze kwamba mie ni mwanafunzi hivyo sitakiwi kulipa gharama yoyote ile.

Akanikabidhi vyeti vyangu vikiwa tayari validated with bolded stamp and beautiful signatures to all 10 pages.

As longer as this is a forum for great thinkers basi nahisi nitakuwa nimeeleweka. Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo una maana awamu hii mambo yako vizuri kwenye utumishi wa umma tofauti na awamu zilizopita Kwa maana ya huduma Kwa wateja?
 
Me Nasemaga Kama Ningesoma Kwa Kupat Mkopo % Hata 80 Hv Kwel Nisinge Pata Tabu Kwenye Maswala Ya Ajira Koz Mkopo Ukiutumia Vzr Unaweza Kujiajili Mtu Asinibishie Kwa Mm Naweza Kuishi Maisha Yyt Ili Mlad Nakua Makin Na Future Yangu
 
Back
Top Bottom