Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,436
- 5,230
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameeleza kuwa mwenendo wa shauri la maombi ya marejeo ya mwenendo wa kesi ya mgawanyo wa mali za chama umeendelea kufichua ukweli kuhusu tafsiri sahihi ya amri ya zuio lililotolewa Juni 10, 2025.
Akizungumza mara baada ya kusikilizwa kwa shauri hilo leo Machi 24, 2026 katika Mahakama ya Rufaa jijini Dodoma, Mnyika amesema kuwa hoja iliyowasilishwa na Wakili wa upande wa kina Saidi Issa Mohamed, Saidi Marijani, mbele ya majaji wa rufaa, imethibitisha wazi kuwa zuio la Juni 10, 2025 lilikuwa na mipaka mahususi ambayo awali Chadema waliieleza umma.
Kwa mujibu wa Mnyika, Wakili Marijani ameiambia Mahakama ya Rufaa kwamba: Zuio la kufanya siasa lilimlenga Katibu Mkuu wa CHADEMA na Bodi ya Wadhamini pekee.
Soma Pia: Kesi ya Zuio CHADEMA kufanya shughuli za kisiasa yaahirishwa Hadi Agosti , 18, 2025
Pia Zuio la matumizi ya mali za chama lilihusu Katibu Mkuu, Bodi ya Wadhamini, wajiriwa walio chini ya Katibu Mkuu, mawakala wake na watu wanaofanya kazi kwa maelekezo ya Katibu Mkuu.
Amesema kilichotokea leo mahakamani kinawaongezea nguvu wanachama na viongozi wa chama nchi nzima kuendelea na shughuli za kisiasa kwa sababu hakuna zuio lolote kisheria linalowazuia wanachama au viongozi.