Mnyika, ubunge sio kujitolea pesa

MODs ni vema mkatengeneza jukwaa la takataka yaani trash bin. Hizi mada zisizo na kichwa wala miguu zisogezwe huko

Hahahahahahahaahhahha nimeipenda hii kaka,kwaiyo kukiwa na jukwaa la takataka tunakua tunapeleka pumbaa huko kma comments si ndio?nimecheka sana aise
 
Mnyika ubunge sio kujitolea pesa, haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutoa pesa. Kinachohitajika ni mbunge mwenye uwezo wa kuikaba serikali itumie kodi ya wananchi kuboresha elimu, maji,nk...tukijenga dhana kwamba uongozi unapimwa kwa mtu kuchangia fedha kusaidia watu tujue tunajenga mazingira mazuri kwa mafisadi kubaki madarakani. Kwani ni utaratibu huu ambao umefanikisha mafisadi wengi kuziteka hata nyumba za ibada kwakuwa wanachangia sana michango ktk nyumba za ibada. Mimi nilidhani pesa hizo mnyika ungezipeleka chuo kikuu ukalipie ada umalizie degree ili jimbo letu la ubungo liondokane na aibu ya kuwa jimbo linalo ongozwa na kihiyo...jamani ni aibu jimbo la mjini kuongozwa na form six tu..

"Wasomi "mkipata degree mnadhani watanzania wengine ni wajinga, huo ni mtazamo potofu! Ebu pina Point aliyoeleza hapo juu na fikiria ni wabunge wangapi wana Phd lakini wanabaki kuwa ndiyo mzee. Kasome sifa za mbunge (elimu inayotakiwa) kabla ya kuhukumu kiwango cha elimu ya form six.


Kwenye bold unaongelea ukihiyo hapa ningependa kujua unamaana gani!


For the record, nafikiri ni wazo zuri ajiendeleze kielimu ili kuongeza maarifa kama ilivyo kwa mtu yeyote yule! Mnyika ni miongoni mwa wabunge wachache wanaojua kuwa kazi ya mbunge ni uwakilishi na si kutatua matatizo ya jimbo lake kwa pesa zake binafsi.
 
Hongera Mnyika kwa kuonesha kuguswa na maendeleo ya Elimu jimboni kwako. Hongera kwa kutokua mchoyo na mbinafsi. Kitendo chako kilistahili kupigiwa mfano na siyo kubezwa.

Nasukumwa kuamini kuwa aliyekushambulia siyo bure ana lake jambo linalokusuma. Anasema 'Ubunge siyo kutoa fedha?' kwa mawazo yake ni nini? .. Fursa ya kufisadi na kujinufaisha au kusinzia? Com' on acha hizo! Pamoja na kuwakilisha watu wake kudai kupewa huduma stahili na serikali yao unafikiri kujenga moyo wa wanaubungo kuchangia elimu ni kosa? Ulitaka ahimize nini kuchangia kitchen party au ubarikio? Ama kweli wewe wa kizamani. Songambele ndugu yetu usikatishwe tamaa kitendo chako cha kutoa katika kile ulichopata kihalali si cha kawaida mshambulizi wako amezoea michango ya makombo ya ufisadi.
Kwa bahati mbaya huyu jamaa anajichanganya, sijui kama anajua utaratibu na sifa za ubunge. Yeye anatamani bunge la vyeti! Kwa taarifa yako bunge letu kwa miaka ya karibuni limekua moja ya mabunge yanayoongoza kwa idadi kubwa ya 'wasomi' lakini sisi wote ni mashaidi wa michango yao, kama ipo inayofanana na 'usomi' wao ni ya kutafuta kwa darubini. Ila upande wa pili tumeshuhudia hoja nzito na michango mingi mizuri yenye maslahi na mwananchi mtanzania ikitoka kwa wabunge wenye elimu ya kawaida tu.

Nasukumwa kuomba mjadala mahsusi wa "kiwango cha elimu kama kigezo cha mafanikio ya mbunge" ili tutende haki kwa hoja hiyo.

HONGERA MNYIKA, HONGERA WANAUBUNGO KWA KUTUPATIA MBUNGE MAKINI! Nataraji kuona wengine wakijifunza kwako...KAMA KIJANA UMEONESHA NJIA...


Sungurampole
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom