Mnyika ubunge sio kujitolea pesa, haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutoa pesa. Kinachohitajika ni mbunge mwenye uwezo wa kuikaba serikali itumie kodi ya wananchi kuboresha elimu, maji,nk...tukijenga dhana kwamba uongozi unapimwa kwa mtu kuchangia fedha kusaidia watu tujue tunajenga mazingira mazuri kwa mafisadi kubaki madarakani. Kwani ni utaratibu huu ambao umefanikisha mafisadi wengi kuziteka hata nyumba za ibada kwakuwa wanachangia sana michango ktk nyumba za ibada. Mimi nilidhani pesa hizo mnyika ungezipeleka chuo kikuu ukalipie ada umalizie degree ili jimbo letu la ubungo liondokane na aibu ya kuwa jimbo linalo ongozwa na kihiyo...jamani ni aibu jimbo la mjini kuongozwa na form six tu..
Naomba mwenye elimu ya Makamba aweke hapa. pili Rais mstaafu wa zanzibar, bwana karume ambaye anatokea CCM naomba pia elimu yake iwekwe hapa,............... nasubili ndio nianze kuchangia.
Tatizo ni kukurupikia mambo yasiyokuwa ya msingi. Kwanza nimuulize huyo anayesema form six kwamba katiba yetu inasema elimu gani kugombea ubunge?? Na je wakati ule walipokuwa na mbunge msomi nini cha maana kilichofanyika AMA alichokifanya. Na hapa kosa ni nini kutoa pesa mfukoni kuchangia maendeleo ya jimbo lake AMA alitaka aweke mfukoni pesa za maendeleo. Tafakari kabla hujachangia
Limbukeni mkubwa, hata kama angekuwa na elimu ya darasa la nne lakini akaweza kuongoza vizuri ni bora kuliko elimu ya chuo na Ph.d alafu uongozi unakushinda. John Major alikuwa waziri mkuu bora Uingereza na alikua na elimu ya sekondari tuu. Bill Gates hakumaliza shule na ameiongoza Microsoft vizuri, Steve Jobs hakumaliza shule pia ila nadhani Apple unaiskia inavyoendelea vizuri. George Washington hakuwa na elimu ya chuo na alikuwa kiongozi shupavu, mifano ipo mingi sana, ila unaonekana we ni mbumbumbu, au limbukeni usiejua maana ya uongozi. Tungekuwa tunawachagua viongozi kwa elimu zao, tungeenda mlimani kuwatafuta maprofesa ili watuongoze majimboni. Sokoine hakuwa na elimu hata ya Form 6 ila nadhani unakubali alikua kiongozi bora. Kabla ya kuandika upuuzi jaribu kutumia akili hata kidogo. Kama umeona jimbo la Ubungo linaaibika kwa kuwa na kiongozi asiyesoma inaonyesha akili huna. Alafu kwa kukusahisha kihiyo si mtu asiyekuwa na elimu, kihiyo ni mtu aliyegushi vyeti. Jaribu kwenda shule ndugu yangu, watu wanakuchekaMnyika ubunge sio kujitolea pesa, haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutoa pesa. Kinachohitajika ni mbunge mwenye uwezo wa kuikaba serikali itumie kodi ya wananchi kuboresha elimu, maji,nk...tukijenga dhana kwamba uongozi unapimwa kwa mtu kuchangia fedha kusaidia watu tujue tunajenga mazingira mazuri kwa mafisadi kubaki madarakani. Kwani ni utaratibu huu ambao umefanikisha mafisadi wengi kuziteka hata nyumba za ibada kwakuwa wanachangia sana michango ktk nyumba za ibada. Mimi nilidhani pesa hizo mnyika ungezipeleka chuo kikuu ukalipie ada umalizie degree ili jimbo letu la ubungo liondokane na aibu ya kuwa jimbo linalo ongozwa na kihiyo...jamani ni aibu jimbo la mjini kuongozwa na form six tu..