Mnyika, ubunge sio kujitolea pesa

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
Mnyika ubunge sio kujitolea pesa, haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutoa pesa. Kinachohitajika ni mbunge mwenye uwezo wa kuikaba serikali itumie kodi ya wananchi kuboresha elimu, maji,nk...tukijenga dhana kwamba uongozi unapimwa kwa mtu kuchangia fedha kusaidia watu tujue tunajenga mazingira mazuri kwa mafisadi kubaki madarakani. Kwani ni utaratibu huu ambao umefanikisha mafisadi wengi kuziteka hata nyumba za ibada kwakuwa wanachangia sana michango ktk nyumba za ibada. Mimi nilidhani pesa hizo mnyika ungezipeleka chuo kikuu ukalipie ada umalizie degree ili jimbo letu la ubungo liondokane na aibu ya kuwa jimbo linalo ongozwa na kihiyo...jamani ni aibu jimbo la mjini kuongozwa na form six tu..
 
Mkuu kwanza kabisa nataka kukuhoji kuhusu kauli yako ya kusema mtu wa form six ni kihiyo. Mtu wa form six si kihio. Pili ili serikali (nikimmanisha matawi yote ya serikali) iweze kuwa kilisha wananchi vizuri lazima viongozi wake wawe representative wa makundi mbali mbali ya jamii. Kwa hiyo kuwa na viongozi wote wenye degree siyo representative kwa maana siyo wananchi wote wenye degree. Pili akili ni muimu kuliko elimu. Hao "amdokta" na "maprofesa" wameifanyia nini nchi mpaka sasa?

Kisha nije kwenye hoya yako ya mchango. Mkuu kwa Tanzania hakuna system ya kuapprepriate funds kwenye majimbo na hela zinazo enda kwenye majimbo mbunge ana kuwa na control ndogo sana ya jinsi zinavyo tumika. Mkuu wa mkoa au wilaya ana kuwa na mamlaka zaidi ya kusimamia hizo pesa kwa ajili ana pokea maagizo direct toka serikalini. Kwa hiyo kwa Tanzania maendeleo laazima yaanzie kwa wananchi. Mfumo huu wa kuchangisha ina maana mbunge kafanikiwa kuhakikisha wananchi wana take a proactive instead of reactive role linapo kuja swala la maendeleo yao.
 
@sikulkifika kaka hebu think BIG then u re post hii thread kwan kwa sasa umekurupuka na ninahisi binafsi huamini ulicho andika?!Mnyika go mwanzo mzuri
 
Mnyika ubunge sio kujitolea pesa, haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutoa pesa. Kinachohitajika ni mbunge mwenye uwezo wa kuikaba serikali itumie kodi ya wananchi kuboresha elimu, maji,nk...tukijenga dhana kwamba uongozi unapimwa kwa mtu kuchangia fedha kusaidia watu tujue tunajenga mazingira mazuri kwa mafisadi kubaki madarakani. Kwani ni utaratibu huu ambao umefanikisha mafisadi wengi kuziteka hata nyumba za ibada kwakuwa wanachangia sana michango ktk nyumba za ibada. Mimi nilidhani pesa hizo mnyika ungezipeleka chuo kikuu ukalipie ada umalizie degree ili jimbo letu la ubungo liondokane na aibu ya kuwa jimbo linalo ongozwa na kihiyo...jamani ni aibu jimbo la mjini kuongozwa na form six tu..

Naomba mwenye elimu ya Makamba aweke hapa. pili Rais mstaafu wa zanzibar, bwana karume ambaye anatokea CCM naomba pia elimu yake iwekwe hapa,............... nasubili ndio nianze kuchangia.
 
Mwanafalsafa kajibu kwa akili contribution iliyokua ya kijinga. Pole na asante!
 
Siku ikifika,unatafuta wanaume Jf,umepima Kwanza akili na kipimo kikubwa? unaandika kama vile unataka kufa leo. Wenye digrii si ndio mafsadi na matapeli, .
 
Naomba mwenye elimu ya Makamba aweke hapa. pili Rais mstaafu wa zanzibar, bwana karume ambaye anatokea CCM naomba pia elimu yake iwekwe hapa,............... nasubili ndio nianze kuchangia.

Mkuu hoja hujibiwa kwa hoja.
Kabla ya elimu ya katibu mkuu wa ccm na rais mstaafu wa znz, ungeweka kwanza ya mwenyekiti wako mbowe na ya mgombea mwenza wa urais.
Ama sivyo jibu hoja
 
Tatizo ni kukurupikia mambo yasiyokuwa ya msingi. Kwanza nimuulize huyo anayesema form six kwamba katiba yetu inasema elimu gani kugombea ubunge?? Na je wakati ule walipokuwa na mbunge msomi nini cha maana kilichofanyika AMA alichokifanya. Na hapa kosa ni nini kutoa pesa mfukoni kuchangia maendeleo ya jimbo lake AMA alitaka aweke mfukoni pesa za maendeleo. Tafakari kabla hujachangia
 
MwanaFalsafa1

Mkubwa mfumo wa TZ hauko ivyo. Pesa zote za serikali za mitaa (local government) zipo under the control of mkurugenzi wa halmashauri ya jiji/manispaa/mji/mji mdogo/wilaya. Hapo kunakua na kamati ya wataalamu (central steering committee) ambayo inatoa vipaumbele kutokana na utaalamu wao,kisha wanaconsult Full Council (yenye madiwani,wataalamu na mbunge). Kisha kamati ya uchumi,fedha na mipango inakaa baada ya kupata mawazo ya kamati ya wataalamu na Full Council,na kuangalia namna ya kutekeleza ivyo vipaumbele. Ivyo mbunge ana control pia ya matumizi ya izo pesa kwani anaingia kwny Full Council yenye kupanga matumizi pamoja na wataalamu. Ila anakua na control kidogo kama ilo Full Council lina wajumbe (madiwani) wengi kutoka chama tofauti na mbunge,kwani watamzidi nguvu kwny kura za kuamua mambo mbalimbali. Asante.
 
Tatizo ni kukurupikia mambo yasiyokuwa ya msingi. Kwanza nimuulize huyo anayesema form six kwamba katiba yetu inasema elimu gani kugombea ubunge?? Na je wakati ule walipokuwa na mbunge msomi nini cha maana kilichofanyika AMA alichokifanya. Na hapa kosa ni nini kutoa pesa mfukoni kuchangia maendeleo ya jimbo lake AMA alitaka aweke mfukoni pesa za maendeleo. Tafakari kabla hujachangia

Mkuu hoja hii imesimama sana sema tu ndio hivyo mtu ukipenda sana chongo utaona kengeza.

sio kazi ya mbunge kutoa pesa yake mfukoni kwa maendeleo ya jimbo. matatizo haya wanayo wabunge wengi si mnyika pekee.
wananchi wa ubungo hawahitaji hata sent ya mnyika, dogo anapaswa kujua kazi yake nini
 
Mnyika ubunge sio kujitolea pesa, haiwezekani kuleta maendeleo kwa kutoa pesa. Kinachohitajika ni mbunge mwenye uwezo wa kuikaba serikali itumie kodi ya wananchi kuboresha elimu, maji,nk...tukijenga dhana kwamba uongozi unapimwa kwa mtu kuchangia fedha kusaidia watu tujue tunajenga mazingira mazuri kwa mafisadi kubaki madarakani. Kwani ni utaratibu huu ambao umefanikisha mafisadi wengi kuziteka hata nyumba za ibada kwakuwa wanachangia sana michango ktk nyumba za ibada. Mimi nilidhani pesa hizo mnyika ungezipeleka chuo kikuu ukalipie ada umalizie degree ili jimbo letu la ubungo liondokane na aibu ya kuwa jimbo linalo ongozwa na kihiyo...jamani ni aibu jimbo la mjini kuongozwa na form six tu..
Limbukeni mkubwa, hata kama angekuwa na elimu ya darasa la nne lakini akaweza kuongoza vizuri ni bora kuliko elimu ya chuo na Ph.d alafu uongozi unakushinda. John Major alikuwa waziri mkuu bora Uingereza na alikua na elimu ya sekondari tuu. Bill Gates hakumaliza shule na ameiongoza Microsoft vizuri, Steve Jobs hakumaliza shule pia ila nadhani Apple unaiskia inavyoendelea vizuri. George Washington hakuwa na elimu ya chuo na alikuwa kiongozi shupavu, mifano ipo mingi sana, ila unaonekana we ni mbumbumbu, au limbukeni usiejua maana ya uongozi. Tungekuwa tunawachagua viongozi kwa elimu zao, tungeenda mlimani kuwatafuta maprofesa ili watuongoze majimboni. Sokoine hakuwa na elimu hata ya Form 6 ila nadhani unakubali alikua kiongozi bora. Kabla ya kuandika upuuzi jaribu kutumia akili hata kidogo. Kama umeona jimbo la Ubungo linaaibika kwa kuwa na kiongozi asiyesoma inaonyesha akili huna. Alafu kwa kukusahisha kihiyo si mtu asiyekuwa na elimu, kihiyo ni mtu aliyegushi vyeti. Jaribu kwenda shule ndugu yangu, watu wanakucheka
 
Bro uliyetuma thread hii hata fisadi ana nafuu kuliko mawazo haya. Hii inaonesha una mambo yako binafsi katika hili.
 
Binafsi sijui elimu ya mnyika, ila niseme mnyika ana elimuu kubwa sana, atathibitisha kwa vitendo wachache ambao mmekuwa mkipiga kelele. Alishinda 2005 wakiba, maprofesor, wenye madgrii mlimani ndio wamempa ushindi na ujue serikali haikufungua vyuo nchini sababu ya myika, ndio utajua jaaamaa msomi, nimesoma hoja za mnyika hakika ni mweledi maana ana elimu ya hali ya juu na mtalaam wa uongozi tena wanaomuombea njaa kwa wivu wa kike wajua atafika sio hapo alipo bali atafika mbali
 
lakini ubunge ni kuhonga wananchi kanga, kanga,t-shirt na kofia,skafu na chumvi kabla ya kupiga kura! Maendeleo mgando!!
 
Jamani hili la elimu ya mnyika lisiwatoe roho tuangalieni hoja ya msingi je ni kazi ya mbunge kutoa pesa yake mfukoni kwa maendeleo ya jimbo?
 
Tatizo hawa sisiem bwana ni wepesi sana kusahau afu warahisi sana kuropoka....! kama uongozi/ubunge ni mpaka uwe professor ama uwe na Phd mbona walimbwaga prof Sarungi rorya na kumpa Lakairo ambaye ni std seven afu leo mnashangaa jimbo kuongozwa na form six liver this is ridiculous....!:whoo:
 
MODs ni vema mkatengeneza jukwaa la takataka yaani trash bin. Hizi mada zisizo na kichwa wala miguu zisogezwe huko
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom