BABA E's
JF-Expert Member
- Dec 25, 2012
- 354
- 136
Sisi tunaoishi maeneo ya kimara hali sasa imeshakuwa mbaya sana. Ipo siku tutakapoona gari la Dawasco linapita tutachoma Moto. Hivi kama kweli kuna shida mahali ni kitu gani kinashindikana kutoa taarifa zinazoeleweka kwa wananchi. Kila mtu anajua maji ni kila kitu. Tumekuwa tukiuziwa maji ya chumvi ambayo nayo pia yanapatikana kwa shida na hata hatujui yanatoka wapi, sijui kwa mwarabu, huyu jamaa akiamua kutumaliza si tutakwisha wote. Kama kweli kuna tatizo mahali hasa linalochukua muda mrefu kwanini serikali isitafute njia mbadala ya kusaidia watu wanaoishi maeneo hayo!!. Ni kwamba huku hakuna viongozi wanaona hili. Haiwezekani watu hampati maji miezi miwili halafu mtu aseme eti wanatengeneza mitambo au njia za maji kwa muda wote huo. hii haiingii akilini.
Zimeni huo umeme wenu hatuutaki tupeni Maji.
Zimeni huo umeme wenu hatuutaki tupeni Maji.