MNYIKA: Spika aunde kamati ya gesi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MNYIKA: Spika aunde kamati ya gesi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 15, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  WAZIRI Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, amemtaka Spika wa Bunge, Anna Makinda, kutumia madaraka na mamlaka yake kutangaza kwa umma kamati nyingine ya kudumu ya Bunge itakayoshughulikia masuala ya gesi asili kabla na wakati wa mkutano wa Bunge ujao mwishoni mwa mwezi huu.
  Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, alisema hatua hiyo ni kutokana na hali tete na tata kuhusu sekta ndogo ya gesi asilia nchini na kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.
  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mnyika alisema pamoja na mambo mengine, Spika Makinda aelekeze kamati hiyo kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge ya mwaka 2011 kuhusu sekta ndogo ya gesi asili ikiwemo juu ya hatua iliyofikiwa katika kushughulikia tuhuma za ufisadi.
  Madai mengine ni ya mapunjo ya fedha za mauzo ya gesi asili na hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya sera, mpango mkakati na sheria ya gesi asili.
  “Hatua hii ni muhimu kufuatia ukimya wa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo kuhusu kauli yangu ya Oktoba 4, 2012 ya kutaka taarifa ya ufafanuzi kuhusu utafutaji wa mafuta na gesi asili nchini iliyotolewa na wizara hiyo Septemba 21 mwaka huu ifutwe,” alisema.
  Alisema kuwa taarifa hiyo ya wizara ilieleza kuwa maandalizi ya sera ya gesi asili yapo katika hatua za mwisho wakati ambapo kamati mbalimbali za kudumu za Bunge hazijahusishwa katika mchakato huo muhimu pamoja na kuwa mamlaka ya kutunga sera kwa mfumo wa sasa ni ya Baraza la Mawaziri.
  “Kwa unyeti na upekee wake sera ya gesi, Spika wa Bunge anapaswa kuwezesha Kamati za Kudumu za Bunge zihusishwe ili pawepo mashauriano na maridhiano kwa mapana na marefu,” alisema.
  Mnyika alisema izingatiwe kwamba katika mkutano wa nane wa Bunge, Spika alitangaza kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imevunjwa na kwamba majukumu iliyokuwa ikishughulikiwa yatashughulikiwa na kamati nyingine kwa mujibu wa madaraka na mamlaka ya spika.


   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Watanzania kwa kauli moja tusimame na tuseme KAMATI ZA BUNGE SASA BASI kwa vile zimeonesha udhaifu wa wazi wa kuwabeba Wabunge hasa pale wanapotuhumiwa kwa rushwa. Kamati iliyoundwa kuchunguza tuhuma dhidi ya wabunge katika shirika la umeme TANESCO imedhihirisha wazi kuwa Wabunge bila kujali chama gani wanatoka wametanguliza mbele maslahi yao na kusahau kabisa maslahi ya Taifa. Kitendo cha kumtaka Waziri wa Nishati kuwaomba radhi Wabunge wakati humo humo ndani yao kuna wabunge waliojitokeza wazi wazi na kusema wana ushahidi wa Baadhi yao waliokula mulungula ni dhahiri sasa hatuna bunge bali majangili.
   
 3. w

  wikolo JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot] [FONT=&quot]SSRA Amendment Bill till next year – Govt
  [/FONT]


  [/FONT]

  [FONT=&quot] [FONT=&quot] Anyone waiting to hear the fate of contributions to any of the pension funds will have to hold their breath until next year when Parliament tables a Bill to amend the Social Security Laws (Amendments) Act 2012 in Dodoma. In April this year, Parliament passed the Social Security Regulatory Authority (SSRA) Amendment Bill, 2012 under which subscribers were barred from taking out their benefits until they attained retirement age. [/FONT][FONT=&quot][/FONT]


  [FONT=&quot]Soon after, workers across the country, notably those in the mining sector, rose in sporadic protests and called for an immediate review. Kisarawe MP Seleman Jafo then tabled a private motion in Parliament pressuring the government to review the Act. However, when tabling the 2012/2013 budget, the Minister for Labour and Employment, Gaudensia Kabaka promised MPs and the entire community of workers that the Bill to amend the Act would be tabled in the session that starts in Dodoma end of this month. But on a sudden turn of events, the government has this week told The Guardian on Sunday that workers would have to wait until early next year when the Bill comes up for review. [/FONT][FONT=&quot][/FONT]


  [FONT=&quot]Deputy Minister for Labour and Employment Dr Milton Makongoro Mahanga this week told this paper that his ministry couldn[/FONT][FONT=&quot]’[/FONT][FONT=&quot]t find sufficient time [/FONT][FONT=&quot]‘’[/FONT][FONT=&quot]to go through the various proposals[/FONT][FONT=&quot]’’[/FONT][FONT=&quot] but promised that a draft Bill could be finalized by next February. [/FONT][FONT=&quot]‘’[/FONT][FONT=&quot]We are still working on the proposals[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot] we need to collect views from the people before we can act,[/FONT][FONT=&quot]’’[/FONT][FONT=&quot] he said, adding that the ministry needs those views to present a better and more comprehensive bill.[/FONT][FONT=&quot][/FONT]


  [FONT=&quot]The Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA), which has followed the matter closely since April this year, has said it was first [/FONT][FONT=&quot]‘[/FONT][FONT=&quot]puzzled[/FONT][FONT=&quot]’[/FONT][FONT=&quot] by the sudden turn of events but has since expressed confidence that the ministry would work on it. TUCTA Secretary General Nicolaus Mgaya this weekend told The Guardian on Sunday that he had already sent in a 12-page report to the ministry, setting out a number of recommendations that called for immediate implementation. [/FONT][FONT=&quot][/FONT]

  [FONT=&quot]But as things stand now, the Union has little option but wait until the ministry clears its decks. [/FONT][FONT=&quot]‘’[/FONT][FONT=&quot]We are not worried so about the slow pace[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot] we are more concerned over the contents of the final draft[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot] it[/FONT][FONT=&quot]’[/FONT][FONT=&quot]s the promise we want fulfilled,[/FONT][FONT=&quot]’’[/FONT][FONT=&quot] he said, during an exclusive interview. He added the workers were anxious to know the fate of their contributions, and that the issue was [/FONT][FONT=&quot]‘[/FONT][FONT=&quot]sensitive[/FONT][FONT=&quot]’[/FONT][FONT=&quot] because it touched on their rights of access to their benefits. [/FONT][FONT=&quot][/FONT]

  [FONT=&quot]Following the recent announcement by the fund[/FONT][FONT=&quot]’[/FONT][FONT=&quot]s regulatory Authority, many workers said during random interviews that they worried the sudden policy changes could disrupt their life plans[/FONT][FONT=&quot],[/FONT][FONT=&quot] saying they held high expectations of financial gains to support their families.[/FONT]


  [/FONT]
  [FONT=&quot]Soerce: The Guardian on Sunday[/FONT][FONT=&quot]
  [/FONT]


  [FONT=&quot][/FONT]
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  wakipenda waisogeze hadi 2015
   
 5. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hi hawa viongozi wetu mbona wanatuchezea akili zetu?withdraw benefit lazima iwe isiwe irudishwe watanzania amkeni tupiganuie haki zetu mbona tumelala kiasi hiki?aghhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,
   
 6. MchukiaUonevu

  MchukiaUonevu JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35

  Kwa mtazamo wako unaona ilikuwa sahihi kujiridhisha na maelezo ya Waziri kuwa kuna wabunge wamepokea rushwa bila kuunda tume ya kuchunguza tuhuma? Kama tume ime-establish kuwa hakuna mbunge aliyepokea rushwa definitely walifanya uchunguzi ikiwemo kuwahoji waliotoa tuhuma na waliotuhumiwa. Tena haitoshi kumtaka Waziri awaombe radhi wabunge bali anatakiwa afukuzwe kazi kwa kusema uongo. Hivi unajua ni damage kiasi gani ilisababishwa na uongo wa Prof.Sospeter,hadi kupelekea wabunge kupitisha bajeti mbovu ya wizara yake kwa kisingizio cha wabunge kupokea rushwa ili kukwamisha bajeti!!
   
 7. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  SWALI ninalojiuliza, Je itakuwaje kwa watumishi ambao watafukuzwa kazi, mikataba ya kazi zao itakuwa imekwisha, mashirika/NGOs kufungwa kwa kufilisika/kazi zao kufikia mwisho. Wakati watumishi hao hawajafikisha miaka 55 kuanzia sasa hadi Februari mwakani wakati ambapo muswaada utapelekwa Bungeni?
   
 8. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wanajaribu kutikisa akili za Watanzania waone kama zinafanya kazi au la.Mimi naomba jamani
  viongozi wa hii nchi msijaribu kucheza na maisha yetu kiasi hicho ohoo.....hamtaamini kuwa ni
  sisi walewale ambao mmekuwa mkijidanganya kwa misemo yenu"hili nalo litapitaaa"...mjue hili halitapita
  kamwe mpaka kieleweke.
   
 9. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #9
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  deleted by Aweda
   
 10. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Hawa wapumbavu wasituletee ujinga wao hapa, ni nini wanachosubiri? wanakusanya maoni ya nani? maana so far sijaona wakikusanya maoni kwa mtu yeyote ninayemfahamu, au wafanyakazi kwao ni nani?

  Kitu kimoja wakae wakijua: HATUPIGI KURA 2015 HADI HII SHERIA IMEBADILIKA NA KURUHUSU MFANYAKAZI ACHUKUE PENSION YAKE 6 MONTHS AFTER AKIACHA KAZI KAMA MWANZO, KWANI SASA TUNATAKA ACHUKUE MIEZI 2 S6 NI MINGI SANA. WATAKE WASITAKE, HII SHERIA LAZIMA IBADILIKE LA SIVYO WAHAME NCHI WATUACHE TUJITUNGIE SHERIA SISI WENYEWE, COZ WE CAN DO IT.
   
 11. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hii serikali inacheza na akili zetu sisi wafanyakazi. Hapa wafanya kazi wasipokuwa makini mwezi wa april 2013 watajadili halafu JK atasaini 2015 kabla hajaondoka. Huu ni uzembe wa hali ya juu na dharau,hujuma na wizi kwa fedha za wafanyakazi - haukubaliki.
   
 12. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hakuna shida,wapeleke mbele hadi 2015.
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  huu ndo upuuzi tusioutaka wa serikali ya ccm, wafanyakazi mbona tumelala hivi hawa wanasiasa uchwara wanacheza na maisha yetu!
   
 14. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ndicho wanachofanya. Wameshatuona mabwege.
   
 15. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ee Mungu tuangalie sisi tunaotaabika. Nataka kuanza masomo mwakani mwezi wa kumi na fund ninayotegemea hasa ni kaakiba nilikohifadhi huko. Hii ni baada ya kukosa mkopo. Naamini Mungu atajibu maombi yangu.
   
 16. w

  wikolo JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ajabu kabisa ni kwamba Mgaya ambaye anatakiwa asimame na kuwasemea wafanyakazi kwa kuupinga kabisa usanii huu wa serikali ndo anakuwa wa kwanza kusema ana imani serikali itatua tatizo hili!! Hivi kama kiongozi yuko hivyo, hao wafuasi wake watakuwaje? Ina maana yeye Mgaya hajui kwamba mpaka sasa kuna watu wamepoteza ajira zao na hawawezi kuchukua hizo pesa na kwa maaana hiyo wanaendelea kuhangaika wao na familia zao? Anaongoza wafanyakazi gani huyu? Inaudhi kwa kweli.
   
 17. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali yetu inacheza na hili fao la kujitoa. Nawaambieni hakika, hili suala linaweza kuwa very pivotal kwenye uchaguzi kwa chama au wagombea watakaolibeba kupata kura za wafanyakazi na dependants wao.
   
 18. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Spika wa Bunge Anna Makinda ndani ya wiki moja atumie madaraka na mamlaka yake kutangaza kwa umma kamati nyingine ya kudumu ya Bunge itayoshughulikia masuala ya gesi asili kabla na wakati wa mkutano wa tisa wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 30 Oktoba 2012 kufuatia hali tete na tata kuhusu sekta ndogo ya gesi asilia nchini na kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.

  Pamoja na mambo mengine aelekeze kamati hiyo kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge ya mwaka 2011 kuhusu Sekta Ndogo ya Gesi Asili ikiwemo juu ya hatua iliyofikiwa katika kushughulikia tuhuma za ufisadi, madai ya mapunjo ya fedha za mauzo ya Gesi asili na hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya sera, mpango mkakati na sheria ya gesi asili.

  Read More...
  SOurce:Mnyika Blog
   
 19. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  [h=2]MONDAY, OCTOBER 15, 2012[/h][h=3]TAARIFA KWA UMMA: Madini, Mafuta na Gesi[/h]  Spika wa Bunge Anna Makinda ndani ya wiki moja atumie madaraka na mamlaka yake kutangaza kwa umma kamati nyingine ya kudumu ya Bunge itayoshughulikia masuala ya gesi asili kabla na wakati wa mkutano wa tisa wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 30 Oktoba 2012 kufuatia hali tete na tata kuhusu sekta ndogo ya gesi asilia nchini na kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.  Pamoja na mambo mengine aelekeze kamati hiyo kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge ya mwaka 2011 kuhusu Sekta Ndogo ya Gesi Asili ikiwemo juu ya hatua iliyofikiwa katika kushughulikia tuhuma za ufisadi, madai ya mapunjo ya fedha za mauzo ya Gesi asili na hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya sera, mpango mkakati na sheria ya gesi asili.


  Hatua hii ni muhimu kufuatia ukimya wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kuhusu kauli yangu ya tarehe 4 Oktoba 2012 ya kutaka Taarifa ya ufafanuzi kuhusu utafutaji wa mafuta na gesi asili nchini iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini tarehe 21 Septemba 2012 ifutwe kwa kuwa italinda ufisadi na kukwaza utetezi wa rasilimali za taifa.


  Taarifa hiyo ya Wizara ya Nishati na Madini ilieleza kuwa maandalizi ya sera ya gesi asili yapo katika hatua za mwisho wakati ambapo kamati mbalimbali za kudumu za Bunge hazijahusishwa katika mchakato huo muhimu pamoja na kuwa mamlaka ya kutunga sera kwa mfumo wetu wa sasa ni ya Baraza la Mawaziri hata hivyo kwa unyeti na upekee wake sera ya gesi Spika wa Bunge anapaswa kuwezesha Kamati za Kudumu za Bunge zihusishwe ili pawepo mashauriano na maridhiano kwa mapana na marefu.


  Taarifa hiyo ya Wizara ya Nishati na Madini ilieleza kuwa mikataba 26 ya TPDC ni sehemu ya nyaraka muhimu za kuboresha utayarishaji wa sera ya gesi asili, hata hivyo mikataba hiyo imeendelea kuwa siri hivyo Spika aingilie kati kuziwezesha Kamati za Kudumu za Bunge kuisimamia serikali kurekebisha mikataba ya sasa na kuboresha mikataba ijayo kwa Serikali kutekeleza mwito wangu wa toka mwaka 2011 wa kutaka mikataba hiyo iwasilishwe bungeni na iwekwe wazi kwa umma.


  Izingatiwe kwamba katika Mkutano wa Nane wa Bunge Spika alitangaza kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imevunjwa na kwamba majukumu yaliyokuwa yakishughulikiwa na kamati hiyo yatashughulikiwa na kamati nyingine kwa mujibu wa madaraka na mamlaka ya Spika.


  Irejewe kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 116 na Kanuni ya 114 fasili ya 14 Spika ana mamlaka na madaraka ya kukabidhi mambo mengine yashughulikiwe na Kamati ya Kudumu ya Bunge nyingine kama atakayoelekeza.


  Ikumbukwe kuwa Julai 2011 na Julai 2012 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani nilieleza namna nchi yetu ilivyojaliwa utajiri wa gesi asilia katikati ya lindi la umasikini wa wananchi na kwamba taifa letu lina fursa ya kuwa nchi kiongozi katika gesi Afrika na kushindana kimataifa ikiwa tutaweka mstari wa mbele upeo, umakini na uadilifu katika sekta ya nishati kuepusha laana ya rasilimali.


  Hata hivyo, mapitio ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2011/2012 yanaonyesha bado serikali haichukui hatua thabiti kushughulikia ufisadi na udhaifu wa kiuongozi katika sekta ndogo ya gesi asili hivyo hatua za haraka zisipochukuliwa katika mwaka wa fedha 2012/2013 na kuendelea rasilimali inaweza kuwa chanzo cha migogoro na kuhatarisha pia usalama wa nchi.


  Kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani nilieleza bungeni tarehe 15 Julai 2011 kuhusu tuhuma za ufisadi na ukiukwaji wa mikataba katika sekta ndogo ya gesi inaoihusu pia Kampuni ya Pan African Energy Tanzania (PAT) na kutaka kuundwa kwa kamati teule ya bunge kuchunguza suala hilo.


  Badala yake Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini uliunda kamati ndogo ya iliyofanya uchunguzi uchunguzi wa masuala husika na taarifa kuwasilishwa bungeni mwaka 2011 ; hata hivyo mpaka sasa maamizio ya bunge kufuatia taarifa hiyo hayajatekelezwa kwa ukamilifu.


  Tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani niliitaka Serikali kueleza ni kwanini mpaka sasa kiasi cha dola milioni 20.1 zilizopunjwa kifisadi hazijareshwa na kuitaka serikali iache kutumia kisingizio cha kuundwa kwa Timu ya Majadiliano (GNT) kuchelewesha utekelezaji wa maazimio, suala ambalo Wizara ya Nishati na Madini itapaswa kueleza hatua iliyofikiwa iwapo Spika atazingatia mwito huu na kuchukua hatua za haraka.


  Ifahamike pia kwamba mwaka 2011 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini niliitaka serikali ambazo kuweka wazi bungeni na kwa umma mikataba ya madini, mafuta na gesi asili katika nchini ili kuongeza tija na uwajibikaji.


  Aidha nilitoa mwito mwito kwa wananchi na wabunge kuongoza marekebisho ya kikatiba na kisheria ili kuweka vifungu vya kulazimisha uwazi katika mikataba katika hizo muhimu kwa uchumi na usalama wa nchi.


  Uwazi katika mikataba utadhibiti pia mianya ya ufisadi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa serikali kwa kuwa mikataba hiyo itajadiliwa na umma na hivyo kupunguza uwezekano wa viongozi kutanguliza maslahi binafsi na kuwa na mikataba bora ya baadaye yenye kuzingatia maslahi ya umma.


  Usiri katika mikataba ni tatizo kwa sababu masharti kama ya kushughulikia madhara ya kimazingira na kuchangia katika huduma za jamii pamoja na kulipa kodi zinazokusudiwa yanaweza yasitekelezwe kwa ukamilifu kama hayatafahamika kwa wabunge na umma. Aidha, ipo mikataba yenye vifungu ambavyo vinakinzana na sheria nyingine ama vinalinda kupindukia makampuni dhidi ya sheria nyingine za nchi zinazotungwa masuala ambayo yanaingilia mamlaka ya bunge ya kutunga sheria na kuisimamia serikali.


  Sheria mpya ya madini Tanzania ya mwaka 2010 ina kifungu kinachotaka uwazi hata hivyo kimejikita katika uwazi wa rekodi na ripoti hakijaweka bayana mfumo wa uwazi katika mikataba ya madini, sheria ya mafuta nayo haina kifungu cha uwazi katika mikataba na sheria ya gesi haipo kabisa; hali ambayo inahitaji kurekebishwa.


  Pamoja na mapato uwazi katika mikataba utachangia katika kupata tija ya ziada katika uchimbaji kwa kulinda maslahi ya wafanyakazi na kuweka mfumo mzuri zaidi wa makampuni kununua bidhaa za ndani kwa majibu wa vifungu vya mikataba hali ambacho itawezesha rasilimali kunufaisha wananchi wengi zaidi.


  Uwazi katika mikataba utawezesha wabunge na wadau wengine kusimamia ipasavyo taasisi za kiserikali kuhusu mifumo ya kifedha na kibenki ambayo itaongeza mchango wa sekta za nishati na madini katika kuimarisha uchumi kwa kudhibiti mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu wakati huu ambapo thamani ya mauzo imeongezeka duniani lakini mzunguko umejitika katika masoko na mabenki ya nje. Kwa ujumla, uwazi katika mikataba utapanua pia uwajibikaji wa kuongeza umiliki wa nchi na wananchi wa michakato ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili.


  Pamoja na kuwa ibara ya nne ya katiba inasema kwamba rasilimali na mali asili zote ziko chini ya usimamizi wa serikali; na ibara ya 63 inaeleza kwamba bunge ndicho chombo kikuu cha kuisimamia serikali kwa kutunga sheria na kupitisha mipango, katiba haijalazimisha mikataba ya madini, mafuta na gesi kuridhiwa na bunge hivyo katika kipindi cha sasa mikataba hiyo iwasilishwe kwa rejea na mapitio.


  Katika muktadha huo, tarehe 4 Oktoba 2012 nilimtaka Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo afute taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuwa lengo la agizo lake la kupitiwa kwa mikataba yote 26 ya utafutaji mafuta na gesi asili ni "kuhakikisha kwamba endapo kuna mapungufu katika mikataba hiyo, mapungufu hayo yasijirudie tena katika mikataba mipya ya baadaye" kwa kuwa ikiachwa ilivyo italinda ufisadi na kukwaza utetezi wa rasilimali za taifa.


  Nilieleza kwamba ufafanuzi uliotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini unatoa mwanya kwa mikataba mibovu kulindwa wakati ambapo kuna madai tuliyotoa toka mwaka 2011 kwamba baadhi ya mikataba hiyo imeingiwa kifisadi na mwaka huu wa 2012 zimeibuka tuhuma za vigogo wa serikali kuingiziwa fedha kifisadi katika akaunti zao za nchini Uswisi na makampuni ya nje ya utafutaji mafuta na gesi asili.


  Aidha, pamoja Serikali kuwasilisha bungeni mikataba inapaswa pia kuwasilisha mipango kabambe (master plan) ya mafuta na gesi asili yenye kuzingatia mabadiliko ya kisera na kimfumo yenye kuwezesha nchi na wananchi kunufaika na rasilimali husika.


  Kauli hii nimeitoa leo tarehe 14 Oktoba 2012 ikiwa ni Siku ya Kumbukumbu ya Hayati Julius Nyerere ambaye alipinga ufisadi na kutaka rasilimali za nchi zitumike kwa manufaa ya maisha ya wananchi:


  John Mnyika (Mb)
  Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
   
 20. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]

  --
  Spika wa Bunge Anna Makinda ndani ya wiki moja atumie madaraka
  na mamlaka yake kutangaza kwa umma kamati nyingine ya kudumu ya Bunge
  itayoshughulikia masuala ya gesi asili kabla na wakati wa mkutano wa tisa wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 30 Oktoba 2012 kufuatia hali tete na tata kuhusu sekta ndogo ya gesi asilia nchini na kwa kuzingatia umuhimu na unyeti wa sekta hiyo katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi.  Pamoja na mambo mengine aelekeze kamati hiyo kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge ya mwaka 2011 kuhusu Sekta Ndogo ya Gesi Asili ikiwemo juu ya hatua iliyofikiwa katika kushughulikia tuhuma za ufisadi, madai ya mapunjo ya fedha za mauzo ya Gesi asili na hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya sera, mpango mkakati na sheria ya gesi asili.


  Hatua hii ni muhimu kufuatia ukimya wa Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo kuhusu kauli yangu ya tarehe 4 Oktoba 2012 ya kutaka Taarifa ya ufafanuzi kuhusu utafutaji wa mafuta na gesi asili nchini iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini tarehe 21 Septemba 2012 ifutwe kwa kuwa italinda ufisadi na kukwaza utetezi wa rasilimali za taifa.


  Taarifa hiyo ya Wizara ya Nishati na Madini ilieleza kuwa maandalizi ya sera ya gesi asili yapo katika hatua za mwisho wakati ambapo kamati mbalimbali za kudumu za Bunge hazijahusishwa katika mchakato huo muhimu pamoja na kuwa mamlaka ya kutunga sera kwa mfumo wetu wa sasa ni ya Baraza la Mawaziri hata hivyo kwa unyeti na upekee wake sera ya gesi Spika wa Bunge anapaswa kuwezesha Kamati za Kudumu za Bunge zihusishwe ili pawepo mashauriano na maridhiano kwa mapana na marefu.


  Taarifa hiyo ya Wizara ya Nishati na Madini ilieleza kuwa mikataba 26 ya TPDC ni sehemu ya nyaraka muhimu za kuboresha utayarishaji wa sera ya gesi asili, hata hivyo mikataba hiyo imeendelea kuwa siri hivyo Spika aingilie kati kuziwezesha Kamati za Kudumu za Bunge kuisimamia serikalikurekebisha mikataba ya sasa na kuboresha mikataba ijayo kwa Serikalikutekeleza mwito wangu wa toka mwaka 2011 wa kutaka mikataba hiyo iwasilishwe bungeni na iwekwe wazi kwa umma.


  Izingatiwe kwamba katika Mkutano wa Nane wa Bunge Spika alitangaza kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imevunjwa na kwamba majukumu yaliyokuwa yakishughulikiwa na kamati hiyo yatashughulikiwa na kamati nyingine kwa mujibu wa madaraka na mamlaka ya Spika.


  Irejewe kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 116 na Kanuni ya 114 fasili ya 14 Spika ana mamlaka na madaraka ya kukabidhi mambo mengine yashughulikiwe na Kamati ya Kudumu ya Bunge nyingine kama atakayoelekeza.


  Ikumbukwe kuwa Julai 2011 na Julai 2012 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani nilieleza namna nchi yetu ilivyojaliwa utajiri wa gesi asilia katikati ya lindi la umasikini wa wananchina kwamba taifa letu lina fursa ya kuwa nchi kiongozi katika gesi Afrika na kushindana kimataifa ikiwa tutaweka mstari wa mbele upeo, umakini na uadilifu katika sekta ya nishati kuepusha laana ya rasilimali.


  Hata hivyo, mapitio ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha 2011/2012 yanaonyesha bado serikali haichukui hatua thabiti kushughulikia ufisadi na udhaifu wa kiuongozi katika sekta ndogo ya gesi asili hivyo hatua za haraka zisipochukuliwa katika mwaka wa fedha 2012/2013 na kuendelea rasilimali inaweza kuwa chanzo cha migogoro na kuhatarisha pia usalama wa nchi.


  Kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani nilieleza bungeni tarehe 15 Julai 2011 kuhusu tuhuma za ufisadi na ukiukwaji wa mikataba katika sekta ndogo ya gesi inaoihusu pia Kampuni ya Pan African Energy Tanzania(PAT) na kutaka kuundwa kwa kamatiteule ya bunge kuchunguza suala hilo.


  Badala yake Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini uliunda kamati ndogo ya iliyofanya uchunguzi uchunguzi wa masuala husika na taarifa kuwasilishwa bungeni mwaka 2011 ; hata hivyo mpaka sasa maamizio ya bunge kufuatia taarifa hiyo hayajatekelezwa kwa ukamilifu.


  Tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani niliitaka Serikali kueleza ni kwanini mpaka sasa kiasi cha dola milioni 20.1 zilizopunjwa kifisadi hazijareshwa na kuitaka serikali iache kutumia kisingizio cha kuundwa kwa Timu ya Majadiliano (GNT) kuchelewesha utekelezaji wa maazimio, suala ambalo Wizara ya Nishati na Madini itapaswa kueleza hatua iliyofikiwa iwapo Spika atazingatia mwito huu na kuchukua hatua za haraka.


  Ifahamike pia kwamba mwaka 2011 kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini niliitaka serikali ambazo kuweka wazi bungeni na kwa umma mikataba ya madini, mafuta na gesi asili katika nchini ili kuongeza tija na uwajibikaji.


  Aidha nilitoa mwito mwito kwa wananchi na wabunge kuongoza marekebisho ya kikatiba na kisheria ili kuweka vifungu vya kulazimisha uwazi katika mikataba katika hizo muhimu kwa uchumi na usalama wa nchi.


  Uwazi katika mikataba utadhibiti pia mianya ya ufisadi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa serikali kwa kuwa mikataba hiyo itajadiliwa na umma na hivyo kupunguza uwezekano wa viongozi kutanguliza maslahi binafsi na kuwa na mikataba bora ya baadaye yenye kuzingatia maslahi ya umma.


  Usiri katika mikataba ni tatizo kwa sababu masharti kama ya kushughulikia madhara ya kimazingira na kuchangia katika huduma za jamii pamoja na kulipa kodi zinazokusudiwa yanaweza yasitekelezwe kwa ukamilifu kama hayatafahamika kwa wabunge na umma. Aidha, ipo mikataba yenye vifungu ambavyo vinakinzana na sheria nyingine ama vinalinda kupindukia makampuni dhidi ya sheria nyingine za nchi zinazotungwa masuala ambayo yanaingilia mamlaka ya bunge ya kutunga sheria na kuisimamia serikali.


  Sheria mpya ya madini Tanzania ya mwaka 2010 ina kifungu kinachotaka uwazi hata hivyo kimejikita katika uwazi wa rekodi na ripoti hakijaweka bayana mfumo wa uwazi katika mikataba ya madini, sheria ya mafuta nayo haina kifungu cha uwazi katika mikataba na sheria ya gesi haipo kabisa; hali ambayo inahitajikurekebishwa.


  Pamoja na mapato uwazi katika mikataba utachangia katika kupata tija ya ziada katika uchimbaji kwa kulinda maslahi ya wafanyakazi na kuweka mfumo mzuri zaidi wa makampuni kununua bidhaa za ndani kwa majibu wa vifungu vya mikataba hali ambacho itawezesha rasilimali kunufaisha wananchi wengi zaidi.


  Uwazi katika mikataba utawezesha wabunge na wadau wengine kusimamia ipasavyo taasisi za kiserikali kuhusu mifumo ya kifedha na kibenki ambayo itaongeza mchango wa sekta za nishati na madini katika kuimarisha uchumi kwa kudhibiti mfumuko wa bei na kuporomoka kwa sarafu wakati huu ambapo thamani ya mauzo imeongezeka duniani lakini mzunguko umejitika katika masoko na mabenki ya nje. Kwa ujumla, uwazi katika mikataba utapanua pia uwajibikaji wa kuongeza umiliki wa nchi na wananchi wa michakato ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili.


  Pamoja na kuwa ibara ya nne ya katiba inasema kwamba rasilimali na mali asili zote ziko chini ya usimamizi wa serikali; na ibara ya 63 inaeleza kwamba bunge ndicho chombo kikuu cha kuisimamia serikali kwa kutunga sheria na kupitisha mipango,katiba haijalazimisha mikataba ya madini, mafuta na gesi kuridhiwa na bunge hivyo katika kipindi cha sasa mikataba hiyo iwasilishwe kwa rejea na mapitio.


  Katika muktadha huo, tarehe 4 Oktoba 2012 nilimtaka Waziri wa Nishati na Madini Prof.Sospeter Muhongo afute taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo kuwa lengo la agizo lake la kupitiwa kwa mikataba yote 26 ya utafutaji mafuta na gesi asili ni “kuhakikisha kwamba endapo kuna mapungufu katika mikataba hiyo, mapungufu hayo yasijirudie tena katika mikataba mipya ya baadaye” kwa kuwa ikiachwa ilivyo italinda ufisadi na kukwaza utetezi wa rasilimali za taifa.


  Nilieleza kwamba ufafanuzi uliotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini unatoa mwanya kwa mikataba mibovu kulindwa wakati ambapo kuna madai tuliyotoa toka mwaka 2011 kwamba baadhi ya mikataba hiyo imeingiwa kifisadi na mwaka huu wa 2012 zimeibuka tuhuma za vigogo wa serikali kuingiziwa fedha kifisadi katika akaunti zao za nchini Uswisi na makampuni ya nje ya utafutaji mafuta na gesiasili.


  Aidha,pamoja Serikali kuwasilisha bungeni mikataba inapaswa pia kuwasilisha mipangokabambe (master plan) ya mafuta na gesi asili yenye kuzingatia mabadiliko ya kisera na kimfumo yenye kuwezesha nchi na wananchi kunufaika na rasilimalihusika.


  Kaulihii nimeitoa leo tarehe 14 Oktoba 2012 ikiwa ni Siku ya Kumbukumbu ya HayatiJulius Nyerere ambaye alipinga ufisadi na kutaka rasilimali za nchi zitumike kwa manufaa ya maisha ya wananchi:


  John Mnyika (Mb)
  Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
   
Loading...