Mnyika: Serikali itoe msimamo uchaguzi Uganda. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika: Serikali itoe msimamo uchaguzi Uganda.

Discussion in 'International Forum' started by nngu007, May 16, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  May 16, 2011Habari Mchanganyiko


  Na Hellen Ngoromera


  MKURUGENZI wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, ameitaka serikali kueleza msimamo wake kuhusu uchaguzi wa nchini Uganda ambao umeelezwa na asasi mbalimbali ikiwemo Mtandao wa Mtandao wa Asasi za Kiraia za kuangalia Uchaguzi Tanzania (TACCEO) kutokuwa huru na wa haki kutokana na kuingiliwa na vyombo vya dola.

  Amemtaka pia Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta kueleza Tanzania inakemea vipi vitendo hivyo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hasa kuhusiana na matumizi makubwa ya vyombo vya dola katika kuzuia matembezi yanayofanyika ndani ya nchi hiyo kama ishara ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta na chakula.

  Katika taarifa yake kwa nyombo vya habari aliyoitoa jana, Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Ubungo(CHADEMA) alilaani vitendo vya ukiukwaji wa haki za kisiasa na uvunjaji wa demokrasia vinavyofanywa na Serikali ya Uganda kwa vyama vya upinzani na makundi mengine yanaounga mkono mabadiliko nchini humo.

  "Katika muktadha huo Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa ya CHADEMA imeshangazwa na Rais Jakaya Kikwete kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni hivi karibuni bila ya Tanzania kutoa kauli ya kina kuhusu uchaguzi wa Uganda na vitendo vilivyofuatia baada ya uchaguzi huo," alisema Mnyika.

  Alieleza ofisi yake inautafsiri ukimya huo kuwa ni ishara ya nchi kupoteza nafasi yake iliyokuwa nayo katika diplomasia ya Afrika ya kukemea vitendo vinavyokwenda kinyume na haki za msingi kama ilivyokuwa wakati wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

  Alieleza pia wadadisi wa mambo wanaweza kutafsiri kuwa ukimya huo ni ishara ya rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupoteza uhalali wa kimaadili kutokana na yaliyojiri kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 nchini Tanzania na yaliyotokea baada ya hapo hususani kuhusu maandamano ya CHADEMA ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha.

  Alimtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa Benard Membe, kueleza umma sababu za marais wengi wa Afrika kuacha kwenda kushuhudia kuapishwa kwa Rais Museveni isipokuwa marais wachache akiwemo wa Tanzania kwa kuwa safari hiyo imetumia fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kuelekezwa kwenye huduma nyingine za msingi za kijamii.

  Aliutaka umma kufahamu kuwa kati ya nchi 54 za bara la Afrika wakuu wa mataifa 32 pekee ndio waliolikwa na kati yao ni marais wanane ndio waliohudhuria.

  "Kurugenzi ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kimataifa inalaani vitendo hivyo vinavyofanywa na vyombo vya dola nchini Uganda na kwa nyakati tofauti vimehusisha kushambulia viongozi wa upinzani, baadhi ya wanahabari na wafuasi wa vyama hivyo na kuwafungulia kesi mbalimbali," alisema Mnyika.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Mnyika unashishushia heshima sasa, hivi unataka serikali itoe tamko gani wakati rais wetu ameenda kushuhudia kuapishwa kwa Yoweri Museveni. Hivi akiri yako haijapata jibu ya hoja yako ya kutaka serikali itoe tamko?
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  safi sana cdm najua kwa sasa watajibu tu wameambiwa waropoke...ivory coast uliwataka watoe tamko sikumbuki kama walifanya hivyo hata wakitoa watatoa la kinafiki kwani kilicho fanywa na museven na yule wa ivory coast ni mwendelezo wa yaliyofanywa na ccm..
   
Loading...