Acha Ufala,Mnyika kazi anayofanya ni kisayansi mno.Ameweza kuorganise Chama chote kimekuwa na Agenda Moja ya Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi pamoja na kumpigania Mwenyekiti wao.
Sasa hivi Kamati, Mabaraza na Makundi yote ya Chadema yanaongea Lugha moja Agenda moja na amejitahidi kuyapa Platform kila kundi sasa hivi kelele zinasikika vizuri na Chama kimeweka Historia nzuri ya kupigania Katiba Mpya na Tume huru ya Uchaguzi.
Huwezi kufananisha Perfomance ya Mnyika na Dk Slaa wakati Mazingira ya Kisiasa ni tofauti kabisa,Uhuru wa kufanya Siasa aliokuwa nao Dk Slaa kipindi cha Mnyika haupo,na huyu Dogo akitulia akafanikiwa kuivusha Chadema salama kwenye haya Mawimbi huenda akawa Katibu Mkuu bora kabisa katika Historia.