Mnyika: CHADEMA haitasusia uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba, amuomba Rais Magufuli kupeleka muswada wa Tume huru ya uchaguzi kwa hati ya dharura!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,821
141,732
Katibu mkuu wa Chadema mh John Mnyika amemuomba Rais Magufuli kupitia serikali kupeleka bungeni kwa hati ya dharura muswada wa kuanzisha Tume huru ya uchaguzi.

Hata hivyo Mnyika amesema Chadema haitasusia uchaguzi mkuu wa mwezi October ila amewataka wananchi wote kupaza sauti zao kuidai Tume huru ya uchaguzi kupitia mitandao ya kijamii.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!


Dar es Salaam. Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema kimewataka wanachama wa chama hicho wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 waandike barua za kuonyesha nia.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Januari 29, 2020 na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika wakati wa mahojiano maalum yaliyorusha Kituo cha Televisheni cha ITV.

Mnyika amesema hayo baada ya kuulizwa na mtandazaji kwenye mahojiano hayo kama Chadema wanatarajia kumsimamisha aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao.

“Waswahili wanasema linalosemwa lipo, ni kweli kwamba mnataka kumsimamisha Lissu kugombea nafasi ya urais mwaka 22020?” alihoji mtangazaji wa kipindi hicho, Farhia Middle

Akijibu swali hilo, Mnyika amesema, “mimi ni msimamizi wa uchaguzi na uteuzi wa mgombea ni sehemu ya uchaguzi, naomba kwa sasa niseme chama kinalenga kumsimamisha nani kugombea urais na katiba ya chama chetu inasema kamati kuu ndiyo yenye mamlaka ya kutafiti jina la mgombea urais.”

“Ila watanzania wawe na uhakika, Chadema itasimamisha mgombea wa urais ambaye ana uwezo wa kushinda na kuleta mabadiliko ya kweli.”

Amesema kwa sasa chama kinawaalika wanachama na wasio wanachama wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu ujao waandike barua kuonyesha nia zao.

“Katika hatua ya sasa nitoe wito sio tu kwa wenye dhamira ya kugombea urais, wanaotaka kugombea udiwani, ubunge, popote pale kwenye maeneo ya nchi yetu wajitokeze kwa kuandika barua za kuonyesha nia,” amesema Mnyika

“Kila mwana Chadema na hata ambaye sio mwana Chadema lakini anataka kugombea kupitia Chadema aandike barua sasa ya kuonyesha nia kuwa anataka kugombea kata gani, jimbo gani au nafasi gani, hatutasubiri badaye, sisi tutaingiza kwenye michakato yetu ya kichama na baadaye michakato mingine itaendelea.”

Mnyika alisema, “tunataka kufanya mkakati thabiti wa kuwaandaa watu wetu kwa mabadiliko, na kati ya watu tunaowaandaa ni wagombea, lazima tuwafundishe misingi ya chama, falsafa, itikadi ya chama ili ukiingia kwenye uongozi uwe kiongozi wa tofauti.”

“Lakini kwa mazingira tuliyonayo kwa sasa hivi, unapaswa vilevile kufundishwa mikakati, unajiandaaje kushinda? Ili yote haya yafanyike ni lazima wagombea wajulikane mapema na muda pekee wa wagombea kujulikana natoa rai kwa Watanzania wote wenye dhamira ya kugombea kupitia chadema waandike barua za kuonyesha nia” amesema

Pia, alipotakiwa kuelezea suala la Makamu Mwenyekiti Bara wa Chadena, Tundu Lissu kuchaguliwa kwenye wadhifa huo wakati yuko nje ya nchi, Mnyika amesema , “kila Mtanzania ana haki ya kuchaguliwa na Chadema ya sasa mtu anaweza kuwa nje ya nchi lakini akashiriki kwenye vikao vya kikatiba vya chama kwa kuwa katiba inaruhusu na Lissu alihudhuria mkutano na akaomba kura na wanachama waakamchagua,” amesema Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba
 
Kabisa kabisa, kwa vile AMEJITAPA kwamba atahakikisha kunakuwa na "UCHAGUZI HURU & HAKI" mwezi Oktoba 2020, basi na aanze na hilo la TUME HURU kama kweli alikuwa serious na kauli yake ile.
 
Kama CHADEMA wako serious hawakupaswa kushiriki UCHAFUZI huo,

Walitakiwa kuanzia January hii agenda Kuu iwe Demonstration for free And Fair election kwa kudai TUME HURU kuanzia now,

Hii imenifungua Macho kwamba CHADEMA na vyama vya upinzani Vipo after Ruzuku tu,

Why?? kwasababu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao hauna Ulaji wa Ruzuku walisusia lakin huu wa October hawawezi

Lakin wamesahau kwamba UCHAGUZI UJAO KWA MAZINGIRA YANAYOTENGENEZWA HATA MBOWE ANAWEZA AKAUKOSA UBUNGE,

naishia hapa

Britannica
 
Aaah! Hata uchaguzi wa serikali za mitaa CHADEMA, tena kupitia kwa mwenyekiti, waliahidi kushiriki lakini baadaye wakasusa. Wana sifa ya kinyonga kama ilivyokuwa kwa Lowasa.
 
Nchi bado ina sheria mbovu sana mpaka Serikali ipeleke mswada ila sio matakwa ya bunge ambalo ndio wananchi wenyewe?
Nadhani hujui Kanuni za Kudumu za Bunge!

Bunge linaruhusu Muswada Binafsi ina maana kuwa Mbunge yeyote anaweza kupeleka bungeni Muswada binafsi na kama akipata majority inakuwa ni sheria.

Kanuni ya 81(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge imeeleza utaratibu wa kuwasilisha Muswada Binafsi.

Kwa mantiki hii, Mnyika kama Mbunge anaweza kuwasilisha Muswada Binafsi kuhusu Tume ya Uchaguzi.

Mnyika anajua vizuri ndio maana alishawahi kupeleka bungeni Muswada Binafsi wa kuundwa kwa Barala za Vijana na ukapitishwa na wabunge kuwa sheria.

Mnyika anachofanya ni populist politics!
 
Back
Top Bottom