Mnyika, mbona huonekani jimboni?

Mnyika, mbona huonekani jimboni?

Natumain umzima na unaendelea vizuri na majukumu yakoo..mimi ni mpiga kura wangu kaka tena nilikuwa mbele kuona ukiingia madarakani lakini sasa mambo yamekuwa kinyume na sikuone tena huku jimboni kwako Maeneo ya manzese, kwamfuga mbwa na ukombozi....

Ukweli huku hali ni mbaya sana na hatuna pa kukimbilia, huduma ya maji ni kiama, miundo mbinu ni uchafu mtupu, takataka ndo usiseme spidi ya kukusanya hela ya taka ni kubwa kuliko huduma yake, barabara zimeekwa taa ila ziliwaka siku moja na nadhani zitawaka tena siku MH RAIS AKITEMBELEA MANZESE USIKU....! Yapo mengi ya kuongea na wewe kuhusu jimbo lako .........

WAKE UP GUY DON'T LET US DOWN

Hii kali sasa yaani kwa kuwa Mnyika ni Mbunge wenu mnataka mpaka taka awazolee Lol!!kweli Watanzani ani wavivu sana hata kufikiria pia mnakuwa wavivu hii ni hatari,Mijitaka mtupe wenyewe na wewe ukiwa mmoja wapo then Mbunge aje kwenye mkutano aongelee mambo ya usafi?Hivi wewe kama mwana Manzese ulifanya nini kwa mtaa wako au hata nyumba ya jirani zako kama tano tu,umewashauri vipi kuhusu utupaji wa takataka?Kuhusu maji hili ni la wote sio Mbunge tu kumbuka kilio cha wengi ni Sauti ya Mungu so komaeni nyie wote kwa usafi kwanza then Mbunge wenu anapambana na mambo ya maji.
Nini wasiwasi sana na wewe kaka kwani naona hata hufuatilii nchi yako inavyokwenda yaani umeshindwa hata kusikia kwa news au hata kufuaatili Bungeni ni juzi tu Mh Mnyika alikuwa anaongea habari za maji hususani Dar Es Salaam yote hata hili hujasikia mie niko mbali sana na home lakini nilisoma na nimesikia hata kupitia youtube nini kiliendelea Bungeni.Tusiwe wepesi wa kushabikia vitu ambavyo ni vya kusikia sikia tu kabla ya kusema au kuandika kitu jaribu kufuatilia kwanza.Kumbuka tu kama Dar Es Salaam yote itapata maji basi na Manzese basi yatapatikana kwa kuwa nayo iko Dar Es Salaam.
 
acha ujinga wewe.....kama angejua kubwa kura si angeomba mtaani kwake mbona kwetu alifika... kaa kimya lofa wewe

Mbona wewe umeanza tu kwa kubwatuka kwa matusi!!Unadhani usingeeleweka bila kutukana. Tunapoteza hadhi ya jukwaa. Hata hivyo kama una nia njema ya kumpa ujumbe Mnyika (maana naona kama sio swala la kujadili), kwa nini usimtumie ujumbe tu badala yake we unapost humu ndani wakati namba yake ya simu huwa ameitoa na ana account za wazi facebook na Tweeter? Mi nadhani unaweza usiwe na nia njema ya kutaka tu tatizo liishe, ila unataka Mnyika achafuke! Simtetei Mnyika wala viongozi wanaopuuza kuwatetea wananchi wao lakini napenda wananchi tuwe responsible na tunie katika kutatua matatizo yaliyopo kwa njia sahihi.
Nawakilisha!
 
wewe unakaa eneo gani la jimbo? na matatizo mengine yanahitaji msukumo ndani ya halmashauri mbunge ana kazi ya kuzungumza maswala ya kibunge na kuwasilisha hoja zetu bungeni tunatakiwa kujua kazi za mbunge na ikumbukwe mbunge si mtendaji sisi tunapoanza kuonekana kulaumu kuwa haya yamesababishwa na mbunge kutoonekana tunawapa mwanya hawa jamaa walioyasababisha haya matatizo kuona wamepata loop hall ya kuendelea kuhujumu tuwe makini tunapolalamika
mi nilidhani ungeanalyze matatizo na kero maeneo zilipo na kuziwasilisha kwa njia ya kumweleza mbunge ajipange wote tupambane si hivi kaka
 
Mnyika Tarehe 08-12-2012 Atashinda manzese kutwa mzima akifungua mashina na matawi jioni atafanya mkutano mtaa wa mnazi mmoja eneo la kwamfuga mbwa.njoo utowe maoni yako.
 
Na Bado.. Mtamsubiri sana muuza sura kutafuta umaarufu.. Si ndio hulka ya viongozi wa cdm wengi.. Porojo tuu, kazi hakuna... Poleni Sana.. Sisi watu wa Arusha tumeshakistukia kile kimeo chetu sasa we are fighting to do something for our city and not the other way round.. CDM full usanii
 
Back
Top Bottom