Mnyika kuwasilisha hoja binafsi bungeni

Mkuu,

Jopo halipashwi kuundwa na serikali ya CCM kwani bado jopo litakuja na katiba yenye kulalia kwa watawala. Ni vizuri ikaundwa kamati ya bunge ambayo itakuwa na composition ya wapinzani ili tuje na mapendekezo ya katiba yenye kukidhi matakwa ya watanzania wote. Hilo jopo unalolizungumzia wewe kitakuwa ni kiini macho na linaweza kufika mahali likasema muda ni mfupi hivyo kuja na mapendekezo baada ya kuipitisha katiba baada ya uchaguzi wa 2015.

Tiba

Buchanan, tuko pamoja hapa. Sijawahi kuona uncoordinated governement kama huyu mheshimiwa. Waziri mkuu anasema yake baada ya waziri kuzumgumza utumbo siku chache kabla ya tamko la Pinda. Nafikiri suala la katiba mpya ni zito na lilipashwa lijadiliwe katika baraza la mawaziri na kuja na msimamo wa serikali kwa umma lakini sio kila mmoja anasema vyake. Hii ni aibu kwa serikali na inaonyesha ni jnsi gani wasivyokuwa makini kwa masuala mazito!!!!

Tiba

Tiba,

Nilifikiri uliupata ule ujumbe wa mwanzo kutoka kwangu..............maneno niliyo-highlight red...........ondoa herufi "h" iliyo mbele ya herufi "s"......yataleta maana uliyokusudia

Kumradhi wakuu wengine kwenye hii mada...........
 
Mkuu kama umemsikiliza vizuri Pinda kasema kuundwe jopo la katazama katiba irekebishwe vipi? Hilo jopo ndio litatowa mapendekezo. Kuna nchi zina katiba leo inazidi miaka 150 hufanyiwa marekebisho kuendana na wakati na si lazima kuunda katiba mpya, lakini, ikiwa hilo jopo litaloundwa likiona kuwa kurekebisha katiba iliyopo kwa manufaa yua umma waTanzani ni kuwa na katiba mpya, basi sidhani kama kuna ubaya hapo.

The point is, kwa nini tupoteze wakati kuongelea katiba wakati its the thing of the past, sasa ni wakati muafaka wa kuongelea na kupendekeza jopo la kupitia katiba liwe vipi.

Nna uhakika kuwa kabla Mnyika hajafikisha hoja yake bungeni jopo litakuwa limeshaundwa na akiifikisha hiyo hoja yake bungeni itakuwa ni kichekesho na itatupiliwa mbali. Kama jopo likisha undwa, hiyo hoja yake itakuwa na faida gani? Au ni chokochoko za kutaka kuleta vurugu?

Mheshimiwa Dar es salaam, ninaamini hujui mazingira ya serikali Tanzania ya CCM.. nakuhakikishia suala la uundaji wa hiyo kamati halitatokea katika siku za karibuni.. kumbuka jinsi suala la hukumu ya mgombea binafsi lilivyocheleweshwa makusudi hadi karibu na uchaguzi.. mimi naamini ni lazima tutumie njia mbalimbali kudai katiba mpya.. kwa hiyo Mh. Mnyika kuandaa hoja binafsi ni kitu kizuri. Naamini bungeni tutaweza kujua nani anaunga na nani anapinga..

Dar es salaam, nakumomba sana urudi nyuma na kusoma between the lines maelezo ya Mh. Pinda.. binafsi nayaona yalikuwa ni ya kisiasa zaidi maana yeye alisema kumshauri rais kuhusu katiba mpya.. na Rais anaweza kuyakataa vilevile na hakuna atakayemfanya kitu kwa sababu katiba inampa madaraka makubwa.
 
NINAOMBA MNYIKA ASOME COMMENT YANGU HII:

Mh. Mnyika nakuomba sana, utushirikishe makundi mbalimbali katika kuandaa hoja hiyo.. tafadhali tafuta wataalamu wa masuala ya katiba, sheria, bunge na serikali ili kuweza kutengeneza hoja binafsi iliyo nzuri sana.. kuna makundi mbalimbali yameshafanya tathmini na research kuhusu masuala ya katiba (bila kusahau ripoti za kamati za kina Nyalali na wenzake). Chonde chonde shirikisha wengine!!
hoja iliyokamilika ikipelekwa bungeni, hapo ndo tutaona sababu gani zitatumika kuitupilia mbali.. aidha kwa kipindi hiki napendekeza ufanyike utaratibu (kadri itakavyowezekana) kutafuta support ya wabunge wa CCM (tukubali tukatae their support ni muhimu).

pia si vibaya kutafuta mtu au kikundi cha watu kupitia michango iliyotolewa hapa JF na kuyazingatia kwa sababu kuna michango mizuri ambayo huwezi kuipata sehemu yoyote ile.

nawasilisha!!
 
Kuna thread ilikuwa hapa wiki iliyopita, kwamba hii siyo hoja ya upinzani tena. Imetekwa nyara. Kinachotakiwa sasa siyo hoja ya katiba mpya bali kuelimisha wananchi mapungufu ya katiba iliyopo na nini kiingie kwenye katiba mpya. Kupigana ili ccm wasiturudishie katiba ya sasa katika ganda jipya
 
Mnyika mbona umechelewa sana? Kwa taarifa yangu sahihi aliyewahi kuweka ombi la hoja binafsi ni Kafulila david na alianza wakati nyie mnazungumza tu yeye akawahi kuweka ombi lake. Kwa hiyo nadhani mtafute msaidiane kuboresha kwa kuwa hutakuwa na nafasi ya kupewa hoja wakati umechelewa kuwasilisha kusudio.
 
Kila mtu sasa hivi amerukia treni ya katiba mpya bila kufafanua huo "upya" wanaoutaka. Ubungo tunataka maji, barabara bora, usafiri, umeme, shule. Mijadala ya katiba isifunike umuhimu wa kuhakikisha kuwa serikali inatekeleza mahitaji ya kila siku ya mwananchi wa kawaida.

Katiba YA SASA NI NZURI. Inahitaji tu marekebisho machache. katiba mpya SIO ufunguo wa kupata uongozi wa nchi.

tEROBURU
 
Mbona kachelewa sana, Mheshimiwa Pinda kisha Tangaza kuunda tume ya Katiba, sasa hoja binafsi ya Mnyika na hoja ya Serikali iliotangazwa na Waziri Mkuu ipi yenye nguvu? Anataka kupoteza muda wa kujadili mambo muhimu, hili tayari linafanyiwa kazi. Mijitu mingine hata sijui huwa ina fikiri kinyume-nyume, siielewi.

We Dar es Salaam,
Usiwe mjanja kwa kudandia hoja za watu. CCM wana miaka 49 sasa wako madarakani ndio mwaka huu wanaona umuhimu wa katiba mpya au ni wamazidiwa tu kwa wananchi kuelimishwa na Upinzani hasa Chadema ndio wenye hii agenda ya katiba mpya kwa hiyo hakuna cha Wazir mkuu wala Celina combani ni waTZ wameamua.

Kila jambo ,kizidiwa mnasema ni lenu hata la kushughulikia mafisadi naona mnasema ni agenda ya CCM, mbona hamkuwatosa kwenye chama hadi wananchi wawakatae baadae mnasema hii agenda yenu ya kuwaondoa.

Tuwe makini hii nchi ni yetu.

Peoples power.
 
Mnyika mbona umechelewa sana? Kwa taarifa yangu sahihi aliyewahi kuweka ombi la hoja binafsi ni Kafulila david na alianza wakati nyie mnazungumza tu yeye akawahi kuweka ombi lake. Kwa hiyo nadhani mtafute msaidiane kuboresha kwa kuwa hutakuwa na nafasi ya kupewa hoja wakati umechelewa kuwasilisha kusudio.

Kafulila ameanza ubunge lini alishawahi kuzungumza issue za wananchi hata siku moja kabla hajawa mbunge? Nachojua huyu bwana kazungumzia ishu ya umeme, hawezi kuzungumzia katiba mpya. Kaa kimya uelewe kinachoendela TZ ndo uchangie mada.
 
Mnyika mbona umechelewa sana? Kwa taarifa yangu sahihi aliyewahi kuweka ombi la hoja binafsi ni Kafulila david na alianza wakati nyie mnazungumza tu yeye akawahi kuweka ombi lake. Kwa hiyo nadhani mtafute msaidiane kuboresha kwa kuwa hutakuwa na nafasi ya kupewa hoja wakati umechelewa kuwasilisha kusudio.

Kaka....Kafulila yupo anaandaa hoja ya kwenda kumsulubu waziri ngeleja bungeni..
 
.

Katiba YA SASA NI NZURI. Inahitaji tu marekebisho machache. katiba mpya SIO ufunguo wa kupata uongozi wa nchi.

tEROBURU

Huo uzuri wa katiba ya sasa ambao kina Mkapa,pinda,john tendwa,warioba,augustino ramadhani,sumaye.....na wanannchi wengine hawajauona ni upi?????......are you serious kweli...
kama watanzania kama wewe ndio wengi ...tena angalau weewe unaweza papasa na kudonoa keyboard za kompyuta ndio wengi ...basi we get a long way to goo..kweli!!!
katiba mpya is inevitable!

Kila mtu sasa hivi amerukia treni ya katiba mpya bila kufafanua huo "upya" wanaoutaka. Ubungo tunataka maji, barabara bora, usafiri, umeme, shule. Mijadala ya katiba isifunike umuhimu wa kuhakikisha kuwa serikali inatekeleza mahitaji ya kila siku ya mwananchi wa kawaida.

Katiba YA SASA NI NZURI. Inahitaji tu marekebisho machache. katiba mpya SIO ufunguo wa kupata uongozi wa nchi.

tEROBURU

Yaani kweli akili ni Nywele! uwezo wako wakufikili umeishia hapo mkuu. Hii katiba haiiitaji marekebisho, katiba mpya ni lazima! mkuu hata kuangalizia kwa wenzio unashindwa (ZANZiBAR)
 
Mbona kachelewa sana, Mheshimiwa Pinda kisha Tangaza kuunda tume ya Katiba, sasa hoja binafsi ya Mnyika na hoja ya Serikali iliotangazwa na Waziri Mkuu ipi yenye nguvu? Anataka kupoteza muda wa kujadili mambo muhimu, hili tayari linafanyiwa kazi. Mijitu mingine hata sijui huwa ina fikiri kinyume-nyume, siielewi.
yani hii comment yako tu ndo iko tofauti na wengine wote, hebu jifanyie uchunguzi.
 
Kwa hili mh. Mnyika watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu wako nyuma yako; maana bila kuwa chonjo kuna uwezekano mkubwa suala hili likapotoshwa kama ilivyofanyika mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili ambapo kilio cha watu ilikuwa kupunguza madaraka makubwa anayopewa rais chini ya katiba, na badala yake ikaandikwa white paper iliyomwongezea madaraka zaidi kwa kumpa uwezo wa kuteua wabunge kumi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom