Patupetu Shekiu
Member
- Nov 25, 2010
- 38
- 0
Hata Kikwete alisema kama kuna mazuri kutoka kwa upinzani kwa nini tusiyatimie. Kama ipo kwenye ilani ya chadema basi pia si jambo jipya kwani ipo kwenye ilani ya CUF tokea mwaka 2000. Wala hakuna ubaya wa kuwepo tena kwenye ilani ya Chadema, na kama Waziri Mkuu katangaza kushughulikia sual la katiba, huoni kuwa ni jambo jema na sifa kwa Chadema kwa kuwa ni ilani yao imepewa kipaumbele? Tatizo ni nini hapo?
Tatizo ni kuwa wao ni mahodari wa kudandia hoja halafu mwisho wa siku wanatekeleza kwa manufaa yao si ya walalahoi wa nchi hii. Mara moja hii umesahau walivyo idandia vita zidi ya mafisadi na wakaipigana kivyaovyao si mliona matokeo ya vita hiyo. Sasa na katiba ndio hiyo wanaidandia tusipochukua tahadhari itawekewa vilaka vya jeans wakati yenyewe ni kaniki tena iliyochakaa.