Mnyika kuwasha moto mwingine Arusha

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454

MNYIKA HAELEZA SABABU ZA NASSARI KUAMISHWA NA KUWATAJA WANAUSALAMA WALIO KUWA WANATISHIA MAISHA YAKE - YouTube


WAKATI Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ikiendelea kumsaka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema,Mbunge wa Ubungo John Mnyika kesho atawasha moto mwingine wa maombolezo uliotawanywa kwa mabomu jana.Mnyika atakuwa msatari wa mbele kuongoza wafuasi wa Chadema kuaga miili ya watu watatu waliouawa katika shambulio la kigaidi Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Soweto.


Mbali na Mnyika zoezi hilo pia litasimamiwa na wabunge wanne wa Chadema walioachiwa huru kwa dhamana leo kwakua upelelezi wa kesi zao hazijakamilika.

wabunge hao waliachiwa huru kwa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoani hapo kabla ya kufikishwa Mahakamani na kutakiwa kurudi Polisi Julai 22 mwaka huu .


Wabunge hao Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu), walipewa dhama hiyo majira ya saa nane mchana.Kabla ya Wabunge hao kuachiwa huru kwa dhamana, maelfu ya wafuasi wa Chama hicho walijazana katika Mahakama hiyo wakisubiri msafara wa wabunge hao, na mara baada ya kupewa taarifa kwamba wabunge hao wameachiwa huru wakiwa Polisi,maandamano makubwa yakaelekea katika Kituo cha Polisi.

Akizungumza baada ya dhamana hiyo Tundu Lissu alisema kwamba, Jeshi la Polisi limempa hasara kubwa baada ya kuvunja mawani yake na kwamba hivi sasa hawezi kufanya kazi yoyote mpaka atakapo pata mawani mapya.


Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliyefika jijini Arusha kwa ajili ya kuwawekea dhama wabunge hao alisema kwamba, Chama hicho bado kitaendelea na mipango yake ya kuomboleza na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu waliouawa kwa shambulio la bomu katika mkutano wa kisiasa wa Chama hicho Juni 15 mwaka huu katika Uwanja wa Soweto, marehemu hao ni pamoja na Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally, waliofariki kwenye mlipuko wa bomu.


Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutoka Polisi Mnyika alisema, "Kesho tutaendelea na zoezi la kuwaaga wenzetu waliofariki dunia katika mkutano wetu, na watazikwa kwa heshima zote za Chama,zoezi litaanzia kanisani kabla ya kwenda katika eneo maalum ilipoandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho".

Hata hivyo Mnyika alikataa kujata jina la kanisa muda wala eneo iliyopangwa kwa madai kwamba ni mapema sana.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe aliyevaa nguo nyeusi pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema aliyevaa skafu shingoni wakiwa nyumbani kwa wazazi wa mmoja wa marehemu (Ramadhani) eneo la Mianzini kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao,katika shambulio la kigaini jijini Arusha

 

Attachments

  • Arusha lema na Mbowe kwa wafiwa wa bomu.jpg
    Arusha lema na Mbowe kwa wafiwa wa bomu.jpg
    28.9 KB · Views: 1,542
Hizi sheria za bunge kweli ni za kizembe sana, watu wanacheza kule Arusha wakijua mishahara na posho zipo palepale.
 
Hizi sheria za bunge kweli ni za kizembe sana, watu wanacheza kule Arusha wakijua mishahara na posho zipo palepale.

Hivi wanaposhughulikia majeruhi na kuwazika waliokufa wewe unaona wanacheza? Kinywa cha mtu hunena kilichojaza moyo. Siyo hilo tu. Ni kwamba uzima na mauti viko kwenye uwezo wa ulimi. Utavuna ulichopanda. Umepanda chuki, utavuna chuki.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Nitakuwepo, navaa tyt zangu 3... halaf nione vijibwa koko, vipolisi toka ccp, na hvyo vya moshi na meru vinaleta ubazaz, lazma ning'oe mbavu kamoja. Yaan sis tunahuzuni vyenyewe vinatuvamia kwa mabomu. Ngoja pakuche
 
Nitakuwepo, navaa tyt zangu 3... halaf nione vijibwa koko, vipolisi toka ccp, na hvyo vya moshi na meru vinaleta ubazaz, lazma ning'oe mbavu kamoja. Yaan sis tunahuzuni vyenyewe vinatuvamia kwa mabomu. Ngoja pakuche

Safi sana kwa UJASIRI. Hakika wewe ni Mwanamke SHUJAA.
 
Polisi bado wanawatafuta akina mbowe?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Big up Mnyika we will be there fear will not paralyze us because we believe the more secure we are, the more safe we are the less alive we will be, life is too short we love to live it to the fullest because we will die anyway.
 
Nendeni mkajadili bajeti bungeni mambo ya kuwasha moto kila siku yametuchosha hayana tija zaidi ya kutupotezea muda
 
Back
Top Bottom