Mnyika ataka Waziri Kawambwa awajibike

Serayamajimbo

Senior Member
Apr 15, 2009
191
38
na Irene Mark


amka2.gif

MKURUGENZI wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amemtaka Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, kuwajibika kwa kushindwa kueleza wazi hatma ya mkataba tata wa uendeshaji wa reli ya kati baina ya serikali na kampuni ya Rites kutoka nchini India.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Mnyika alisema bila kuvunjwa kwa mkataba wa TRL, hakuna sababu ya kuendelea kuwepo kwa waziri wa miundombinu kwa maelezo kuwa mkataba huo ni mzigo kwa serikali.
Mnyika, alisema kauli mbili tofauti zilizotolewa na viongozi wa juu wa wizara moja ni dalili za kushindwa katika utendaji wao.
“Utofauti wa kauli kati ya waziri na katibu wake ni ishara kwamba kimaadili hatuna serikali. Najua kusema hakuna serikali ni uhaini lakini ni muhimu Watanzania wajue ukweli huu.
“…Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema mkusanyiko wa mawaziri na watendaji wasiokuwa na kauli moja ni dalili ya kutokuwa na serikali,” alisisitiza Mnyika. Mnyika alisema, anaielewa India kuwa ni moja ya nchi zenye mitandao mipana ya reli, lakini kati ya makampuni yanayoheshimika kwa uwekezaji nchini humo kampuni ya Rites si mojawapo.
 
Mapungufu mazito sana haya kwenye sekta ya reli, na kwa mtu makini alitakiwa kujiuzulu fasta!..

Ni mkataba gani huu wenye sura mbili, then waziri yuko na furaha tu?..

Je huku si kuwaabudu cum kuwaogopa wageni, huku ukiwaponda blood-brodas?

Utumwa wa Fikra!
 
Back
Top Bottom