Mnyika aibua tena uozo TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mnyika aibua tena uozo TANESCO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaga Michael, May 22, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  WAZIRI Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, kwa mara nyingine tena, ameibua suala zima la mikataba tata baina ya serikali na makampuni ya umeme nchini, akimtaka pia Waziri mpya wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ataje hadharani majina ya watendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) wanaotuhumiwa kufanya ubadhilifu mkubwa ndani ya shirika hilo.

  Katika taarifa yake kwa umma jana, Mnyika amemtaka waziri huyo mbali na kuwaumbua watendaji hao hadharani, ahoji vyombo vya uchunguzi vya kiserikali na mamlaka za nidhamu za watumishi hao ni hatua zipi zilichukuliwa tangu watendaji hao wahusishwe na ubadhilifu. Mnyika alisema ufisadi hauko TANESCO peke yake, bali umejikita zaidi ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na baadhi ya wataalamu kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, ambao wamesababisha nchi kuwa katika hali mbaya. "Baadhi ya majina yao yametajwa pia bungeni kwa nyakati mbalimbali, hivyo anachopaswa kufanya ni kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa maazimio yaliyobaki ya Bunge ya mwaka 2008 juu ya mkataba baina ya TANESCO na kampuni ya Richmond Development Company LLC na ya mwaka 2011, kuhusu uhalali wa utaratibu wa wizara kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti bungeni na kuhusu uendeshaji wa sekta ndogo ya gesi nchini," alisema.

  Mnyika akizungumzia mikataba hiyo, alisema ni miaka minne toka maazimio yapitishwe na Bunge, ambalo liliagiza kwamba mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC (uliorithiwa na Dowans Holdings S.A.) na ile kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals, ipitiwe upya mapema iwezekanavyo kama ambavyo mikataba ya madini ilivyopitiwa upya na serikali.

  "Iwapo azimio hili lingetekelezwa kwa ukamilifu wake, gharama za uzalishaji TANESCO na serikali kwa ujumla zinazotokana na matatizo katika mikataba zingepungua," alisema na kuongeza; "Pia, Azimio Na. 1 lilitaka serikali izihusishe kamati za kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya mikataba mikubwa ya muda mrefu ya kibiashara ili kuondokana na utaratibu uliopitwa na kwamba mikataba ya kibiashara ni siri hata kwa walipa kodi wenyewe." Alisema serikali imeshindwa kutekeleza azimio hilo na
  matokeo yake ni kwamba, kati ya mwaka 2008 mpaka 2012 kumeendelea kuwa na usiri katika hatua za awali za maandalizi ya mikataba, na pia mikataba mingi mikubwa haijafanyiwa mapitio.

  Aliongeza kuwa, utaratibu wa sasa kwa mujibu wa Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge ya mwaka 1988 pamoja na kanuni na taratibu za Bunge, ambao mbunge anaweza kuomba kwa serikali kupitia kwa ofisi ya Bunge nakala ya mikataba baada ya kusainiwa, hauliwezeshi Bunge kutimiza kikamilifu wajibu wa kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 63 ya kuisimamia serikali katika hatua zote muhimu.

  Hata hivyo, Mnyika alimuunga mkono Waziri Muhongo katika azma ya kutumia wataalamu wa ndani kabla ya wataalamu wa nje, na kumtaka aagize ukaguzi maalumu ili wataalamu na makandarasi waliohusika katika ufisadi dhidi ya TANESCO na mashirika mengine yaliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini waondolewe katika orodha (black listing).

  Alimtaka Muhongo mbali na kusimamia ongezeko la uzalishaji na usambazaji wa umeme, azingatie kuwa matatizo ya sasa ni matokeo ya udhaifu wa kisera na kiutendaji kuanzia wakati wa Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadaye kwa Rais Benjamin Mkapa ambapo TANESCO iliwekwa kwenye orodha ya mashirika ya kubinafsishwa na hivyo serikali kuacha kuwekeza kikamilifu katika uzalishaji wa umeme pamoja na matengenezo ya miundombinu ya usafirishaji na usambazaji.

  Aidha, alisema ni katika kipindi hicho hicho kuliibuka matatizo pia ya ufisadi kwenye uwekezaji katika sekta ya nishati kama ya IPTL, Kiwira, Net Group Solution nk. "Awamu ya nne ya Rais Kikwete nayo ikaongeza zaidi mzigo kwa TANESCO kupitia miradi mingine ya kifisadi kama ya Richmond na sasa kuna tuhuma mpya za ufisadi kuhusu utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme. "Mpango wa Dharura uliwasilishwa bungeni tarehe 13 Agosti 2011, ahadi ya serikali ilikuwa kuongeza MW 572 ifikapo mwezi Desemba 2011 na kuweka orodha ya mitambo ya kununua kabla ya Oktoba 2012.

  "Pamoja na kuwa na mpango wa gharama kubwa wa dharura ambao unahusisha kwa sehemu kubwa suluhisho la muda mfupi la kukodi mitambo, bado utekelezaji wa mpango wenyewe nao unasuasua hali inayodhihirisha kuendelea kwa uzembe na udhaifu katika serikali.

  "Hata mitambo iliyofungwa nayo haina uhakika wa kuwa na uwezo wa kuendeshwa wakati wote uliopangwa kutokana na madeni TANESCO ambayo inadaiwa, serikali kushindwa kutekeleza kikamilifu ahadi ilizotoa kwa TANESCO na pia upungufu wa gesi kwa ajili ya kuendeshea mitambo husika na kuwa tishio kwa nchi kuingia gizani katika siku za usoni. Kati ya miradi ambayo utekelezaji wake umesuasua kinyume na ahadi za serikali bungeni ni pamoja na kununua mtambo wa MW 150 wa NSSF na kununua mitambo ya MW 100 wa TANESCO Ubungo," alisema Mnyika. Kwa upande mwingine, Mnyika alisema udhaifu wa kutokutekeleza mipango ya uzalishaji wa gesi na makaa ya mawe kwa wakati umesababisha utegemezi mkubwa kwenye matumizi ya mafuta katika mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura.

  Alidai kuwa zaidi ya nusu ya umeme unaozalishwa nchini hivi sasa ambao ni sawa na takribani MW 660, unazalishwa kwa kutumia dizeli, mafuta ya ndege na mafuta mazito hali ambayo imeongeza mahitaji makubwa ya uagizaji wa mafuta toka nje ya nchi. "Hii imesababisha mahitaji makubwa ya fedha za kigeni kwa ajili ya kuagiza mafuta, na hivyo kuchangia katika kuporomoka kwa thamani ya shilingi. Aidha, ongezeko kubwa la uagizaji toka nje limeathiri urari wa biashara na hivyo kuchangia katika mfumuko wa bei, ambao umesababisha Watanzania kubeba mzigo wa kupanda kwa bei za bidhaa na gharama za maisha kwa ujumla kutokana na ufisadi kwenye mikataba, ubadhirifu katika matumizi, uzembe katika uongozi na upungufu katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya serikali kwenye sekta ya nishati," alisema.

  Hii ni mara ya pili ndani ya siku mbili kwa Mnyika kuwashukia mawaziri wapya. Juzi, mbunge huyo alimtaka Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe achukue hatua na kueleza bayana namna kilivyotumika kiasi cha dola za Marekani milioni 164 kwa ajili ya usambazaji wa miundomimbinu ya maji jijini Dar es Salaam ambayo imeshindwa kufanya kazi kikamilifu.
   
 2. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  wahusika wamekusikia
   
 3. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kila siku tunamsikia John Mnyika tu akiwatetea wananchi wa Dar kuhusu uwajibikaji wa serikali kwenye kila idara mara TANESCO, EWURA, AFYA, MIUNDOMBINU, AJIRA nk. Je, wabunge wengine wa Dar wako wapi? Au wapo likizo wanasubiri posho tu?

  Big up sana kamanda Mnyika. Usikate tamaa, songa mbele kamanda!

  - JACADUOGO (Mwenyekiti wa WANARORYA WOTE popote walipo!)
   
 4. A

  AZIMIO Senior Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Halafu unasikia mtu na akili zake anakaa chini kuandika upuuzi eti tuambie Mnyika umefanya nini katika jimbo lako?

  Wao kipimo cha mbunge kufanya kazi sjui huwa ni nini?mbunge wetu tunamuona jinsi anavyohangaika kupeleka matatizo yetu kwa wahuska tatizo wahusika hawatekelezi wajibu wao, mbunge gani wa ubungo alishawahi hata kubadilisha tu baadhi ya vipengele tu kwenye kamati za bunge na bunge zima kulidhia?

  BIG UP MNYIKA TUPO PAMOJA.
   
 5. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Halafu atanyang'anywa ubunge kesho kutwa.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kipimo cha mbunge mchapakazi siyo kuonekana mara kwa mara kwenye media. Ungekuja na taarifa ya utafiti unaoonesha Mnyika kafanya nini jimboni mwake na wenzake hawakufanya nini, kidogo ningeshawishika kuona logic ya thread yako.

  Inawezekana kabisa hao ambao hawasikiki wako kivitendo zaidi kuliko maneno.
   
 7. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Halafu huyo poyoy(Mnyika) hana hata hadhi ya kuongoza serikali ya mtaa.
  .
  "IT WAS GOD WHO CREATED MAN, MAN CREATED MONEY AND MONEY HAVE CREATED MAD, MAD, MAD AND MADNESS".
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumbe Mnyika unamsemea, huyu siku hizi tunamwita Mbunge mpenda sifa , na kwa taarifa yako huyu jamaa hafanyi kazi ni media tu zinampamba, nenda ubungo kaangalia watu wanavyolia jimboni kwake
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumbe Mnyika unamsemea, huyu siku hizi tunamwita Mbunge mpenda sifa , na kwa taarifa yako huyu jamaa hafanyi kazi ni media tu zinampamba, nenda ubungo kaangalia watu wanavyolia jimboni kwake
   
 10. Q

  Qixima mQiqa Senior Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 178
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata wewe hufai hata kuwa mwenyekiti wa mende wa chooni
   
 11. m

  mamajack JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hicho wanachofanya bila kusikika kinamnufaisha nani?acha mawazo ya ujima wewe.tunaona utekelezaji ndo maana tunasema.
   
 12. m

  mamajack JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  nyie mbimbu ndo mnamuita hivyo,wananchi wanamjua mtumishi wao.wewe si umezoea kupewa 10% msimu hii huna ndo maana huoni kazi yake.
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,029
  Trophy Points: 280
  Natamani sana kama ingewezekana majimbo ya Ubungo na Kawe yangeunganishwa ili mpambanaji John Mnyika awe mbunge wangu.
   
 14. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #14
  May 22, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kamanda Mnyika songa mbele, hakuna kulala mpaka kinaeleweka.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Source: Chuki binafsi. Myika anafanya kazi Ubungo, katika masuala mengi, na kero za wananchi, JJ amehusika kusaidia kutatua. Tuache ushabiki usio na maana. We taja kero na mpelekee uone.

  Mfano: Kituo cha mabasi yaendayo mikoani, hakiridhishi; Ndani ni kichafu, sakafu zimechakaa kiasi kwamba huwezi kuburuza sanduku lako. Makusanyo ni mengi, yanaenda wapi?

  Ubungo, Kimara, Mbezi NK hakuna masoko, je Mh Mbunge una mikakati gani. Hivi wote mpaka twende Kariakoo?

  Utaona atajibu haya.
   
 16. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Hemu tuwekee hapa mategemeo yako Mnyika anatakiwa kufanya nini? usiwe ukawa unaandika mambo usiyoyajua.
   
 17. F

  Froida JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ni maoni yenu lakini ukiniuliza mimi nitakuambiya ni mbunge aliyena dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo kwenye jimbo lake Bravo Mnyika
   
 18. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Ashughulikie matatizo ya jimbo lake Uhaba wa maji, foleni N.K sio UMEME hauwezi.
   
 19. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2012
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Mh Mnyika ni kweli yupo na wananchi, kazi yake inonekana hata mafisadi wakimtolea nje katika kesi yake bado atafanya kazi na wananchi kwa sababu anakublika. Ogopanguvu ya umma.
   
 20. k

  kitenuly JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haijalishi hata kama atanyang'wanywa sababu bado ni msemaji wa CHADEMA, hivyo akili yake itaendelea kufanya kazi na kutumika kikamilifu, kusema na kukosoa, upo hapo?!!!!! moto wa jua hauzimwi kwa fire extinguisher, au gari la zima moto.
   
Loading...