Mnh? Umasaini tena...!

Napenda kumshukuru mwandishi kwa uchambuzi wake kuhusu mila za jamii za kitanzania. Ila ningependa nitoe dosari chache tu katika uchambuzi huu kama ifuatavyo:
1. Kichwa cha habari kinapotosha kwa kiasi kikubwa kuhusu desturi aliyolenga kuzungumzia mwandishi. Kwa kawaida, kimila umasaini, mgeni hakaribishwi mke alale naye, bali, Mgeni hukaribishwa na hulala kwa mke. Lengo na nia siyo mgeni kulala na mke, ila ni ahifadhiwe kwa mke.
2. Binti ambaye bado hajafanyiwa tohara hawezi kamwe kuolewa hivyo swala la mahari ndogo halipo. Binti hufanyiwa tohara kwanza ndiyo apate kuolewa.
3.Ni makosa kwa mvulana ambaye hajafanyiwa tohara kuwa na mahusiano kumamiiana na binti ambaye hajafanyiwa tohara (mbaya zaidi kwa yule aliyefanyiwa tohara)kwa sababu mabinti wote ni wa morani.


Heee hii kali...
 
Back
Top Bottom