Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Majority ya wana JF ni wa age kati ya late 1960's up to early 1980's.

Mwanakijiji ni wa late 1960's, karibu utapata wajukuu na umri wa kugombea urais karibu utatimia.

Punguza michezo.

he kumbe kazaliwa 1960's bado kijana kabisa ..
mie nikajua atakuwa wa mwaka 1940-1950 teteteteteh
 
Hahaaaaaaaaaa,ukweli ni kwamba sijawahi kutuma salamu redioni hata siku moja mkuu,sema nilikuwa nikipenda sana Muziki,na kama unakumbuka zamani wakati wa Idhaa ya Taifa ya RTD Muziki ulikuwa ukipigwa zaidi kwenye vipindi vya Salamu vya Jambo na Mchana mwema/Pokea Salamu(na baadae jioni njema japo kilikuwa kifupi cha nusu saa) na vipindi kama Kijaruba,So ukitaka kusikiliza Muziki ilikuwa sharti usikilize vipindi vya kutakiana salamu....Sana sana kulikuwa na vipindi maalumu(mara moja kwa wiki) vya Muziki kama Misakato,Club Raha Leo Show,Starehe na BP,Disco Show,Chaguo la Msikilizaji,Mambo Mpwitompwito,Kombora n.k..

So sikuwa mtuma salamu mkuu,bali najivunia kwamba nina kumbukumbu ya vitu vingi sana vilivyotokea kipindi cha nyuma hasa katika nyanja za Michezo,burudani na Siasa kwa mbaaaaali

Ebu weka thread ya tuziimbe huku nakumbuka kwenye DHB kulikuwa na mdau mmoja anaitwa TZ boy alikuwa na collection ya nyimbo nyingi za zamani.. na mdau mwingine yupo hku pia aitwa Babadesi nadhan ukiweka thread wadau watamwaga nyimbo za zaman zenye burudani mwanana!!
 
FL, Balantanda ana photographic memory!

Hahaaaa,inawezekana aisee...Maana hata mimi huwa kuna kipindi najishangaa,naweza nikaanza kuandika kitu let say about muziki,nashangaa vitu vyaniijia tu naanza kuvidondosha...Hata rafiki zangu hushangaa kwa hilo..May be ni photographic memory kama unavyosema mkuu
 
Ebu weka thread ya tuziimbe huku nakumbuka kwenye DHB kulikuwa na mdau mmoja anaitwa TZ boy alikuwa na collection ya nyimbo nyingi za zamani.. na mdau mwingine yupo hku pia aitwa Babadesi nadhan ukiweka thread wadau watamwaga nyimbo za zaman zenye burudani mwanana!!

Thread mbona zipo nyingi tu mkuu...angalia hapa: https://www.jamiiforums.com/sports-...bushane-wimbo-bora-wenye-jina-la-kike-26.html na hapa: https://www.jamiiforums.com/sports-...ane-nyimbo-bora-zenye-majina-ya-kiume-ii.html
 
Imma,Emmanuel Kulaya,huyu kijana alikuwa ananifurahisha sana anaweza kutaja ukoo wao wote akipata nafasi ya kutumia watu watatu,alikuwa mwanasanaa tosha!!
 
kbc ya kenya kuna jamaa alikuna anaitwa francis kadenge omwana wa lea, huyu naye alikuwa kiboko, akina wajadi fundi wa mahuta shimoni newala, kuna mtu namkumbuka akiitwa makungu wa tabora toka 1980 namsikia redio ujerumani akituma salamu
 
zamani watanzania walikuwa wanapendana,wanajaliana katika raha na shida na ilikuwa ukimsalimia mtu kupitia redio pekee ya taifa,RTD huyo alietumiwa salamu anajisikia na kama watu walisikia jina lake watamtafuta na kumwambia na nikumfata alipo maana simu ya kiganjani ilikuwa bado kipindi hiko .Wewe angalia watu walivyokuwa wastaarabu unaweza ukatuma barua kwa mzee wako labda huko Rombo mkuu kwa kumpa mtu anaesafiri na bus na akipita maeneo hayo anaidondosha huku bus linakwenda itapodondokea inaokotwa na lazima ifike kwa mlengwa salama ,jaribu sasa uone.
I have had quite a stressful day today, lakini hii nani yako hapo juu (in red) imeni-massage mpaka ndani ya roho....it sounds so funny! thx.
 
...kwenye kipindi cha "from me to you" external service ya Radio Tanzania DSM, kulikuwa na mtuma salaam machachari aliyefahamika kama Alphonce Majiyapwani.
 
Duu, umenikumbusha mbali,
Enzi hizo miaka ya mwanzo ya 90, nilikuwa na rafiki wa karibu, mtangazaji RTD, alinihadithia mambo mengi.
Siku hizo mshahara wa Mtangazaji RTD akianza kazi ilikuwa ni Shilingi,
3,660.65.
Kikombe cha chai ya maziwa canteen yao pale Pugu Rd. ilikuwa Sh. 20, chapati, 20, andazi 10, mayai mawili ya kukaanga 40. Kipande cha kuku wa kukaanga ni sh.60.

Hao mabingwa wa salamu, walikuwa kila ukisoma kadi yake, kuna mahali unapita, anakupiga na Sh. 100. ukimaliza kipindi cha salaam, ukishuka canteen, hiyo 100, unapata chai, chapati 2 na mayai mawili ya kukaanga, kipande cha kuku na soda juu.

Jioni ukipita maeneo fulani, sio vi offer vinafululuza, akina dada ndio usiseme, enzi hizo redio yenyewe ilikuwa moja.

Hawa mabingwa wa salamu, ndio walikuwa wakiongoza kumwaga hizo 100, wakifuatiwa na wanamuziki wanaotaka nyimbo zao zipigwe, hawa walikata fungu kubwa zaidi,

Enzi hizo, Mghanii wetu akiwa 'Mzee Athumani Khalfani' akilipwa Sh.100 kughani kipindi cha nusu saa.

Jameni watu wametoka mbali!. Wee acha tuu!.
Mungu awarehemu watangazaji wote waliotangulia, na walibakia mpaka sasa, wapewe pongezi nyingi, na hata wazuri waliochipukia na wanaoendelea kuchipukia pia pongezi, ukiondoa wale wachache wana vamia fani.

kumbe rushwa ya kupaishwa ilikuwepo tangu enzi hizo?leo twalia ufisadi kumbe mliulea tangu dahari??mafisi mafisadi wakubwa nie
 
I have had quite a stressful day today, lakini hii nani yako hapo juu (in red) imeni-massage mpaka ndani ya roho....it sounds so funny! thx.

Thats why there z a JF for refreshing your mind..pole sana kwa majukumu Mbeba box..i mean M-Mbabe
 
Hahaaaaaaa,Mwanakijiji..Umenikumbusha mbali sana ndugu yangu,umenikumbusha vipindi vya Jambo na Mchana Mwema(Pokea Salamu) pale Radio Tanzania bila kusahau kipindi cha usiku cha Kijaruba cha Abdallah Mlawa,hivi vilikuwa ni vipindi maarufu sana vya salamu...Ilikuwa ukisikiliza vipindi hivi ni lazima utakutana na majina haya

1.Issa Hasssan Madjeshi

2.Chidi Chidi Chitenda

3.Chivalavala wa Chivalavala

4.Limonga Justin Limonga

5.Duwa Wajadi

6.Wajadi Fundi

7.Mohammed Kassim Saibaba

8.Jai Sikinde

9.Maalim Shabani Uledi

10.Boko Man Mwana wa Mkongoman
wow, nimejihisis niko darasa la saba enzi zile

yaani hapo umemuacha Amos Nyang'uye bingwa salamu RTD kwa miaka kadhaa
 
hapo bado chivalavala M chivalavala, rama j sauniga wa ngarenaro, chidi chidi chitenda, justnine limonga, juma shaaban kesi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom