Watuma salamu maarufu waliotamba kwenye vipindi mbalimbali vya Redio

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
5,940
23,177
Miaka imesonga sana, maisha yamebadilika Kwa kiasi kikubwa.Tofauti na sasa ambapo ukiwa na simu janja au tarakirishi unapata taarifa zote zilizotokea na zilizovunjika 'breaking news', Zamani redio ilikuwa chombo muhimu ktk kupata taarifa na burudani.

Leo nimewakumbuka wale watuma salamu maarufu enzi zile,ingawa hata sasa wapo baadhi ya watu ambao ni maarufu ktk vipindi mbalimbali ukisikiliza redio km Clouds mfano kuna heri dereva babaji, shangwe dereva babaji, Daudi wakota n.k

Enzi hizo ukisikiliza kipindi cha mirindimo asilia na Malima Nderema au salamu Kwa wagonjwa, kuna majina maarufu huwezi kuacha kuyasikia wakati wa kutuma salamu.

Kuna huyu jamaa wa kuitwa Wajadi fundi Wajadi binadamu mashaka, yeye kila siku yupo safarini kuelekea mahuta shimoni, fundi Khamisi full migebuka wa mwandiga fashion sokoni Kigoma.

Lawena Msonda Baba mzazi kutoka chunya Mbeya.

Ally Mrangi Gigiri Mresa yeye mar kila siku yupo safarini kuelekea mabibo Dar es Salaam.

Zakaria Ndemfoo, Issa Mzee wa urembo kutoka Moshi. Lupa tingatinga "mdau asiyechuja" ndiyo ilikuwa slogan yake bila kumsahau Chesko Mzee wa matunda kutoka Africa Sana.

Kuna mdau akiitwa Limonga Justine Limonga na kuna huyu mama Abuu wa majani mapana. Kuna jamaa aliitwa Fikiri Dario Gakala wa GGM Geita na Filbert Kyenshambi kutoka Muleba-Nshambi, wapo wengi sn na tulikuwa tunaenjoy sana Enzi hizo

Unawakumbuka baadhi? Unazikumbuka kauli mbiu zao maarufu zilizotamba?
 
Siku hizi Ukisikiliza Deutsch welle (DW) na BBC kuna jamaa mmoja maarufu sana anaitwa Jumanne mpenda Amani yeye kila akipiga simu kutoa maoni yake mwishoni lazima amalize na hii kauli mbiu "ni busara Urusi Waache vita haraka" anafurahisha Sn
 
Kuna mmoja huyo nimemsahau jina,anapenda kupiga sn simu DW na kutoa ushauri..mwamba anajikutaga mchambuzi nguli wa siasa..nikimkumbuka jina nitamtaja
Mtaje Sana mnk nasikiliza sna kipindi hicho au unamzungumzia basila bint kimario !
 
Back
Top Bottom