wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,931
- 4,550
Kwa mara ya kwanza kabisa katika maisha yangu najuta kabisa kuwa mtanzania, taifa la watu wajinga, taifa lisilo na mbele wala nyuma, jambo ambalo hata mtoto mdogo haliwezi kumsumbua eti majitu mazima yanapiga yowe kuwa dola imepanda. Mnataka shilingi ya Tanzania ipande kwenda wapi? Wasomi gani nyie msiojua uchumi? Sh ya Tanzania ipande kwa lipi? Mnazalisha nini hapa Tanzania ili kuinua uchumi?
Kila kitu watanzania mnanunua nje ya nchi, wewe unayesoma hapa hebu jikague umevaa mavazi ya wapi? Kuanzia viatu, suruali, chupi,soksi, shati hadi saa vyote ni nje ya nchi, magari yote, pikipiki na vipuri ni nje ya nchi hadi sindano, stick za meno na sukari mnaagiza nje, wakulima wa machungwa Muheza wanakufa njaa nyie mnaagiza machungwa kutoka South africa na juice kutoka Kenya, taifa gani hili? More imports than exports halafu eti shilingi ipande, watanzania mnapenda kuishi kimiujiza kuliko uhalisia, ndio maana wengi wenu ni washirikina wa kutupwa, viwanda mmeua halafu shilingi ipande, tena ngoja sasa hivi dola moja itakuwa sh 5,000 tuone mtafanyaje.