Mnapenda wanaume wenye ndevu au vipi?

Mnapenda wanaume wenye ndevu au vipi?

Quinton Canosa

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2012
Posts
1,228
Reaction score
1,264
Wanaume wamekuwa wakijiuliza je, ni vizuri kunyoa ndevu kipara kabisa au kuziacha zikue na kuwa mzee madevu?.
Je, nitaonekana navutia nikiwa nimenyoa ndevu au sijanyoa ndevu?

Utafiti huko Uingereza unaonesha kwamba wanawake wengi (si wote) huvutiwa sana na wanaume wenye videvu vyenye ndevu kidogo (Stubble) kuliko wale wasio na ndevu kabisa (clean shaved) au wenye vichaka vya ndevu (full beards) kwa ajili ya sex, mapenzi na ndoa.
Njia rahisi ya kuvutia wanawake ni mwanaume kuwa na kidevu chenye ndevundevu na si kuwa kipara au nyingi kama akina Osama.

Kuwa na ndevu (kwa mwonekano wa aina hiyo) hudhihirisha uwezo kinguvu, uimara, ukomavu kijamii na mvuto (best romantic partners)
Kuwa na ndevu ni kiungo cha nguvu kijamii na kimapenzi kwani ni alama ya kuonesha ukomavu kibaolojia.
Wale wasio na ndevu kabisa huonekana hawajakomaa na wale wenye vichaka vya ndevu huwa na sura inayotisha mno au kuonekana wababe na hawavutii sana.

Je, huu utafiti una ukweli wowote? labda wanawake wanaweza kutoa maoni!

Source: British newspaper the Sunday Telegraph,
India times newspaper.
Women prefer men with stubble - The Times of India
 
Kwe mwenye hela ndevu ni urembo, kwa masikini ni uchafu! Hutaki unaacha!!
 
kufuga ndevu ni sunnah katika uislam, hivyo ukitaka fuga (lakini zitunze ziwe safi) upate thawabu, ukitaka acha kufuga wala hupati dhambi.
 
haaaaa.jpg
 
Back
Top Bottom