Mnaosafiri haya yanawahusu

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,675
Mnaosafiri na familia kwenye magari binafsi wakati huu wa sikukuu tafadhali muwe makini.

Tayari tumeshashuhudia ajali kadhaa zilizogharimu uhai na hata kusababisha majeraha makubwa.
Kumbuka kumiliki gari hakukufanyi automatically kuwa dereva wa masafa marefu! Kama huna stamina na huijiui barabara vyema basi epuka kuiweka familia yako katika hatari.

Ikibidi basi endesha mchana wakati mwanga ni wa kutosha pia pata muda wa kutosha kupumzika.

Wote waliopo kwenye gari wafunge mikanda na tabia ya kuwaacha watoto wakiwemo wakubwa kurukaruka na kucheza kwenye gari wakati wa safari ni hatari!
Pia hakikisha gari imefanyiwa ukaguzi na kujiridhisha kwamba inaweza kusafiri.
Je hali ya tairi, mfumo wa brake, usukani, ipo vipi? Pia acheni tabia ya kujazana sana kwenye magari kisa tu huyu ni mtoto wa Mjomba au shangazi hivyo hatuwezi kumuacha!

Pia tabia ya kusomba kila 'takataka' kutoka nyumbani au njiani - mahindi, mihogo, viazi, maharage, nyanya, vitunguu etc. mpaka kupitiliza uwezo wa gari acheni kabisa!

Pia endesha kwa mwendo wa tahadhari huku ukitilia maanani alama za barabarani. Ukifanya hivyo wewe na familia yako mnaweza kuuona mwaka mpya mkiwa wazima na wenye afya badala ya kuishia mortuary au kwenye vitanda vya hospitali!
 
Ni kweli kabisa na hii yote inaletwa na ile kwamba mtu kanunua gari na kazowea kuendesha safari za kazini na kurudi nyumbani baada ya muda mfupi anajiona keshakuwa dereva wa masafa marefu kumbe sivyo.
Na wakati mwingine udereva wenyewe hajasomea kajifunza juu juu, alama za barabarani hazijui ndio huo mwisho wake kunakuwa na ajali ambazo zingeweza kuepukika.
 
Umesema acheni tabia ya kujazana ndugu ni kitu cha msingi. Kuna kipindi nikienda home na gari ndugu wa karibu wakiomba lifti zaidi ya wawili niliwaambia tutapanda gari letu wawili wengine ninawapa nauli ya basi, siku za nyuma walikuwa hawanielewi lakini nimesimamia msimamo wangu na issue ya kuwapa nauli mpaka sasa wamenizoea ingawa busara inahitajika ili ndugu wakuelewe wengine wanaweza kuchukia
 
Back
Top Bottom