Secret Star
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,829
- 2,001
Huu uzi nauandika kwa masikitiko makubwa sana! Tanzania Umeme Umekuwa ukikatika tangu miaka 60 iliyopita, hadi leo umeme bado unaendelea kukatika na natumai miaka 50 ijayo ukija Tanzania utakuta hali ni hii hii!. Leo sababu ni hii miaka 100 ijayo kutakuwa na sababu nyingine mbalimbali, ni kama sababu mbalimbali zilizokuwepo miaka 50 iliyopita.
Shida ni kubwa ila leo nitazungumzia Kero ya ubadilishwaji wa nguzo! Sababu hii inawafanya Tanesco wakate umeme hovyo. Ni kweli Tanesco wanashindwa kutumia akili ndogo ya busara kukata umeme usiku labda kuanzia saa sita usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi, ili watu wanavyoenda kutafuta mkate wa kila siku wasipate shida hiyo!
Tanesco mnawezaje kukata umeme mchana kwa siku tatu mfululizo!? Mnataka watu wale wapi!? Watu ambao ni masikini wa kutupwa wanaotegemea kipato cha kila siku ili wale chakula duni!. Tanesco mnashindwa kuwa na mitambo ya mwanga ili muwe mnafanya marekebisho ya miundombinu yenu usiku wa manane!
Yaani Tanesco nao wanataka Kwenda kazini saa mbili muda ambao raia nao wanaenda kazini, kisha Tanesco wakifika kazini wanakata umeme hadi jioni kisha wanarudisha na kurudi kutoka kazini!!! Nchi nyingine sio kwamba hawakati kabisa umeme ila wakitaka kifanya marekebisho wanatafuta muda ambao hautaathiri shughuli za wananchi!
😔😔Dah waTZ Hakyamungu tumekwisha!!!