omtiti
JF-Expert Member
- Jun 19, 2019
- 1,022
- 1,590
Kuna wimbi limeibuka la kuanzisha thread kila uchao,zisizo na mashiko,za kipuuzi,zenye lengo la kumdhihaki na kumtukana rais Magufuli,zikiwa na lengo la kumvunja moyo na kumtisha.nasema halitafanikiwa.
Napenda kuwafahamisha wale wanaoanzisha thread hizo ,ya kwamba hawamtukani Rais Magufuli pekee ,bali wanadhihaki na kuikejeri taasisi ya urais,ambayo ina muundo wake mkubwa ,ikiwa imejaa watumishi wa taaluma mbalimbali,na wenye weledi wa hali ya juu sana.
Taasisi hii haiwezi kukubali idhalilishwe na kutukanwa kwa kisingizio cha uhuru wa kutoa maoni,na haikubaliki popote pale duniani.
Natoa onyo kwa wale ambao hawaamini katika kukosoa na kutoa njia mbadala kama njia ya kujenga taifa ,bali wao huamini katika matusi na dhihaka kwa wengine,waache mara moja,kwani hiyo ni jinai ina vifungu vya adhabu kwa mujibu wa sheria za nchi.
Hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ,popote pale walipo bila haya wala hiyana..
Ni wajibu wako wewe raia kuchuja aina ya maelezo unayoyaleta mbele ya hadhara(jamii),
Ukidharau na kufanya kwa kuiga ili mradi uonekane ni shujaa,usije blame mtu yoyote,bali blame yourself
Dawa inachemka,lengo ni kujenga nidhamu ya watanzania,iliyomomonyoka kwa kushindwa kutumia utandawazi kiistarabu kujiletea maendeleo.