Line moja kila mtandao ni wazo zuri lakini kuna mapungufu.
Mfano ndugu X ana kampuni kubwa ya kimataifa ambayo iko nchi mbali mbali Africa.
Ana line ya voda hii ni kwa ajili tu ya kuwasiliana na wakurugenzi wake wa kanda za nchi za kusini mwa Africa kuliko na coverage nzuri ya voda.
Ana line ingine ya pili ya voda ajili ya kuwasiliana na ma manager wake walio mikoani Tanzania.
Ana line ya tatu ya voda ajili ya wakurugenzi wake walioko Africa mashariki.
Ana line ya nne ya voda ajili ya kuwasiliana na wanachama wa club yake vile yeye ni mfadhili mkuu na mwenyekiti wa club.
Ana line moja ya airtel kwa ajili ya kuwasiliana na ndugu zake tu na baba yake kijijini kwao kuliko na coverage nzuri ya airtel.
Ana line moja ya tigo kuwasiliana na mtu mshikaji kama wewe na washikaji wengi wa Dar kuliko na watumiaji wengi vile tigo wakazi wa dar wanaipenda sana.
Ana line ingine ambayo huitumia only for international calls kuongea na matajiri wenzake na hata maraisi mambo ya kuwekeza.
Kwa vyovyote mtu kama huyu akiwa na line moja kutatokea msongamano mkubwa mno taarifa zingine atazikosa.
Kumbuka mtu kama huyu ni jicho la taifa kwa kodi zake anazolipa na idadi kubwa ya watanzania amewaajiri nyuma yake kuna maelfu ya familia wanaishi kwa ajili yake.
Hapo hapo asubuhi akifika akifungua computer yake anakuta email 700 na zote anatakiwa azijibu.
Wazo lako ni zuri la kizalendo.Wazo langu watu kama hawa kuwe na utaratibu maalum kuwatambua.Kama ilivyo TANESCO mwenye kiwanda rate ya kulipa haiwezi kuwa sawa na mwenye bulb moja.
Sent using
Jamii Forums mobile app