Mmwambie Rais nampongeza kwa kazi anayofanya lakini kura yangu 2025 hapati, mbunge wake anataka kunipora ardhi

NANCA

Member
Jun 23, 2023
92
100
Mimi chief nimpongeze Rais Samia kwa mzigo wa miradi anoopiga, kiukweli ukweli anapambana na kujitahidi sana, maua kwake ingawa 2025 simpi kura yangu maana kuna mbunge wake mmoja darasa la 4B tena failure anataka kunipokonya ardhi yngu kwa kutumia mamlaka yake.

Hivyo nimeamua kumjumuisha Rais Samia kwasababu ni mbunge wake na nimwambie tu hiyo mbunge kuwa mimi ni mwingine asitegemee kupata hata nukta ya ardhi yangu kwa kuitumia serikali, mkono wa Mungu kwangu una nguvu sana kuliko alivyowaahidi kuexperience kwa wengine aliodhurumu.
 
Umchague au usimchague Samia ndiye rais mpk 2030. Hata akipigiwa kura na mwanaye Abdul tu, bado atakuwa rais.

Kwann?
1. Tuna katiba baya halijawahi tokea popote duniani.
2. Tuna jeshi la hovyo lisilojitambua kama jeshi la Niger, Gabon, Burkina Faso, na Mali.
 
Hivi kama tunajua atakuwa rais tutake tusitake sasa tunapiga kura za nini?
 
Samia akuwekee mahakama, kila siku unaipita hapohapo, huendi kushtaki kudhulumiwa ardhi unakuja kulialia humu
 
Mimi chief nimpongeze Rais Samia kwa mzigo wa miradi anoopiga, kiukweli ukweli anapambana na kujitahidi sana, maua kwake ingawa 2025 simpi kura yangu maana kuna mbunge wake mmoja darasa la 4B tena failure anataka kunipokonya ardhi yngu kwa kutumia mamlaka yake.
Mkuu NANCA kosa afanye nani, adhabu apewe nani?!.
Hivyo sasa unataka kuitumia kura yako kama fimbo ya kumtishia Rais Samia ili aingilie kati mgogoro wako wa kiwanja na Waziri wake!, alikuambia 2025 anagombea?.

P
 
Back
Top Bottom