Mmmh hivi hii ni haki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mmmh hivi hii ni haki

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kitunguunyanya, Mar 18, 2011.

 1. K

  Kitunguunyanya Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wandugu wa jf! Juzi boss we2 kamfukuza mfanyakazi mwenze2 kazi ni sawa? Kwa kifupi huyu mfanyakazi alimpigia sm mume wa mwenzake wanaofanya kazi secta 1 ofis 1 na kumwambia kwamba et mke wake anatembea na mume wake. Maskini jamaa akapatwa na hasra na kumpiga mkewe mpaka akazimia na kulazwa hospto. Mwanaume ndo akastuka na kufanya uchunguzi na kubaini ni uongo ndo hayo mambo yakafika ofisin na baada ya kikao boss akaamua kumfukuza kazi akisema ninanukuu" 2mekaa kikao 2meona 2kufukuze kazi kw sababu hizi zifuatazo 1. Fahari wawili hawakai zizi moja. 2meamua wewe uondoke mwenzako akipona 2tamrudisha kazini. 2. katika kampuni yangu sitaki wa2 waongo isije siku ukampelekea mke wangu manen0 ya uongo ukanivunjia heshma 3. kwanza utendaji wako hauridhish nilikua nafikiria kukufukuza kazi siku nying ila sikua na sababu ya msing. Chukua mshahara wako wa mwenzi huu ingawa bado mwenz haujaisha. nakutakia mafanikio mema" hivi wanajf ni haki? Si angemuhamisha2 secta? Au nyie munaunaje? Mimi binafsi imeniuma kufukuzwa kwake
   
 2. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kumfukuza mtu kazi ni mpaka hatua zifuatwe
  1. Je alikwisha kupewa onyo mara ngapi?
  2. Je alipewa nafasi ya kujitetea? n.k n.k..

  Kama hatua hazikufuatwa ana haki ya kwenda kwenye vyombo vya haki (kama vyama vya wafanyakazi) akasaidiwa...(ila mshauri awe anachunguza vitu kwanza apate uhakika)
   
 3. LD

  LD JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Na yeye, kwa nini amchonganishe mke wa mtu kwa mume wake.
  Vyovyote tu, lakini kitendo cha kumfanya mwenzake apigwe na mume wake, kinamtosha kupata hiyo adhabu, hana utu.
  Kuna siku atamwambia mke wa Bosi, Bosi anamtaka kimapenzi kumbe uongo.

  Muache akajifunze.
   
 4. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Huyo bosi anaona mbali, hata wewe ungekuja pata kichapo, mshukuru bosi
   
 5. K

  Kitunguunyanya Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaaa bosi alishawahi kumuonya lakini alimuambia kwamba nitakubadilishia nikupe ya kufukuza izi ofsini kama hiyo huwezi. Sijui ataanzia wapi kwenye vyombo vya sheria maana baada ya kumwambia mume wake kwamba amefukuzwa kazi mume wake amemfukuza nyumbani sasa anaish kwa ndugu zake
   
 6. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Haki kabisa mie sipendi wambea kabisa
   
 7. super thinker

  super thinker JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama kuna UHAKIKA wa sababu zilizo tumika bora afukuzwe tu,umeumia lakini fikiria kiundani aliyofanya na implications zake mbeleni........
   
 8. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  c mnafik ulitaka mkuu afanye nini tena
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Huyo jamaa cha umbea atakuwa anatoa hata siri za ofisini.
  Anadeserve kufukuzwa ukizingatia utendaji wake ulikuwa haumridhishi boss.
  Kwani utaratibu wa kumfukuza mfanyakazi hapo kwenu ukoje? Usilalamike kitu kumbe mambo yote yalishaelezewa kwenye contract.
   
 10. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hata mimi ningemfukuza.
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Acha tu afukuzwe!
   
 12. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  aende pale CMA(baraza la usuluhishi wa mambo ya kazi) huyu boss hana haki ya kumfukuza kazi kwa kisingizio kama hicho.Sheria ya kazi hairuhusu,huo ni uhuni.Lazima kuwe na sababu ya msingi ndani ya kazi na awe emeshapewa onyo,apewe haki ya kujitetea nk si kukurupuka tu,Huyu ana haki zote za kudai fidia na pia haki ya kurudishwa kazini au kulipwa kiasi cha mshahara ambao itaamriwa na hawa waamuzi(CMA).akipelekwa huyu boss hatakuwa na ushahidi wa kujitetea nae ni mhuni tu.Huyu dada aandae mkataba wake wa kazi,salary slip nk.....
   
 13. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Makubwa!
   
 14. triza

  triza Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo ni muuwaji kwanini amchonganishe mwenzake kwa mumewe alitaka amtake yeye? boss alifanya uamuzi wa busara sana kumfukuza kazi anaweza akasingizia tena wengine ata ukimuamisha idara nyingine ataenda tena kuchonganisha huko wengine. bora alivyofukuzwa kazi.
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  ni sahihi kabisa bosi alichofanya ....narudia tena kwa sauti kubwa NI SAHIHI KABISA.......

  unajua muongo anaua haraka sana kuliko mchawi?!!.......safi sana.....ufanisi wa kazi uko chini...kazi kupiga domo na kuua ndoa za watu.........

  huku kwenye makampuni hakuna sijui vikao....kuna njia mbili tu nazo ni summary dismisal na consultation hii ya pili huwa ni mara chachesana na hata huwa ikifanyika then ukabaki huwezi kudumu sana...... vikao ni huko serikalini......
   
 16. K

  Kitunguunyanya Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa lokisa lakini watakaaje tena ofisi mmoja? si watakua hawapatan na mwenzake? Isitoshe shughuli zao zinaingilia si wataharibu utendaji wa kazi?
   
 17. m

  mohamedswaleh New Member

  #17
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siku hizi, mambo ni kinagaubaga, hakuna kufichana au kuhurumiyana, iwapo bosi hakumuachisha kazi, angejenga ukuta, ndiposa bosi akatumia hikma ya kumuachisha kazi. Winter.jpg
   
 18. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Na ww akifukuzwa kazi kwa kuleta umbea humu jf atakua amekuonea? ....
   
 19. s

  shosti JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  umbea si kazi kazi kusutwa,sasa kalipwa kwa umbea wake:lol:
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  1) Tuichambuwe hii habari kama ni "Kitunguu" au "Nyanya".

  2) Hili ni shirika binafsi au Serikali au shirika la uma au si shirika?

  3) Wewe ni kitunguu au nyanya? Au kachumabari?

  4) Inakuhusu nini wewe hii habari?

  5) Yes, ni haki ya boss kupata sababu ya kumfukuza amtakae. Elewa kwamba hakuna anaekuajiri kama hakuhitaji kazini na hakuna anaekufukuza kama anakuhitaji kazini.
   
Loading...