Mmiliki wa gari ambalo Lissu alilitaja kwa kutumia plate number zake amewahi kulalamika?

Mkuu;
Aksante sana kwa andiko lako safi. Kwangu mimi nimekuelewa kuwa; Kama ni kweli hao watu walimfuatilia, naamini hawakuwa na ujuzi wa kutosha. Niliandika kuwa; Aliyekuwa anamfuatilia, alidhani anamfuatilia jinga fulani lisilo hata na uwezo wa kugundua kuwa linafuatiliwa. Ndo maana nikasema, basi huyo askari wetu, hajui kazi yake.
Ila unaposema kuwa; Acheni kujitafutia cheap public sympth I hope it is "sympathy". Sijui kama nimekuelewa hapo. Ni nani anatafuta hiyo kitu?? Lisu alimtaja/wataja wakuu wa idara fulani. Je, wewe ndio mmoja wa waliotajwa unamjibu?? Ukiona kimyaaa!! Ni nini maana ya kimya yako??
si hekima kumrushia mawe kila Mbwa anayekubwekea
 
Katika hali kama hizi matumizi sahihi ya akili yana kuwa chini sana....ni mihemko inakuwa juu sana...........

Hivyo ni vyema kila mtu kuwa makini na kila anachokinena......
 
Kufuatwa na Gari ndio kutishiwa kuuwawa??
Mawazo mengine bana, yamekaa Ki-Lumumba Lumumba....!!!!!!!!!!
Ni kweli Ma Lumumba yanapima upepo unaendaje humu kwa kile walichokifanya. Plate namba huwa zinachongwa tu, watu wa usalama leo wanaweka plate namba hii kwenye gari, kesho wanaweka nyingine. Mfumo wa utoaji wa plate namba za magari uko kiholela sana, utakuta plate namba ina jina la mtu, ina maana mfumo huu umewekwa makusudi ili kuwapa nafasi watu kujitengenezea plate namba zao kama vile majambazi au hawa watu wa usalama wa ccm. Huu mfumo wa utoaji plate namba za magari ni vema tuuangalie kwa jicho la tatu
 
NANUKUU.... ni heri Slaa awe raisi kuliko Tindu Lisu awe mbunge.. BY JK..... MWISHO WA KUNUKUU
Slaa agombee kwa tiketi ya ccm kwani yeyeni mwana ccm. TL ndio Chadema halisi na hamuwezi kumuua kama ambavyo mmeshindwa, aibu juu yenu. Mungu ndiye mwenye maamuzi ya mwisho juu ya uhai wa mtu sio ccm. Labda niwakubushe au kuwajulisha ambao hawajui maandiko matakatifu yanasema "Mtu anayetenda haki Mungu anamstawisha kama mtende" hivyo mungu atamstawisha TL kama mtende. Katika hili lililotikea Mungu atamponya na ataendelea kustawi kama mtende. Habari ndio hiyo.
 
Tulianza na tukio la Ben Saanane, akapotezwa na watu wasiojulikana na hadi leo hii hajulikani yuko wapi.

Likafuatia tukio la studio ya Clouds kuvamiwa na watu wasiojulikana na watu wenye silaha za moto, hadi leo hii watu hao "wameshindikana" kukamatika!

Likafuatia tukio la Nape Nnauye kuchomolewa na bastola mchana kweupe pale Hoteli ya Protea na mtu huyo kuonekana kwenye camera na huyo mtu hadi leo hajakamatwa!

Tulishuhudia pia tukio la IMMMA advocates wakivamiwa usiku wa manane na ofisi hizo kulipuliwa na hadi leo hajamatwa mtu yeyote!

Tumeshuhudia pia tukio baya kabisa la kushambuliwa kwa mwanasiasa wetu shujaa wa Taifa letu Tundu Lissu mchana kweupe na silaha za moto na watu hao hadi muda huu hawakakamatwa!

Kwa hiyo kwa matukio hayo ni dhahiri kutokana na tukio la hivi karibuni kwa Tundu Lissu kueleza kuwa alikuwa akifiuatwa na gari nyeupe ya Premio lenye namba T460CQV, ni vyema jeshi letu la Polisi likawakamata hao wenye gari hilo na kueleza sababu za kumfuatilia Tundu Lissu.

Na kama hao watu wasipokamatwa tutajua a Taifa letu limegeuka Taifa la ki-MAFIA ambalo haliwezi kurudi nyuma ambamo kuna baadhi ya watu wamekuwa UNTOUCHABLES ambao hawakamatiki tena kwa sheria za hapa kwetu, na wanasubiri kwenda The Hague wakajibu makosa yao makubwa sana!
 
Lissu huwa hakosei, CCM wanataka atoweke duniani hata leo ana wanyima raha sana.
Kwenye matukio kama haya ndo tunagundua akili finyu za watz wengi kama wewe mkuu!
Kama mmiliki wa gari ambalo Lissu alitaja hdharani namba zake za usajili alisingiziwa kuwa gari yake ndio ilikuwa inatumika kufuatila movement za Lissu, bila shaka mmliki husika angeshajitokeza hadharani na kukana na pengine kulalamika na hata kutaka kuchukua hatua za kisheria.

Maswali:
Je,muhusika(mmiliki wa gari husika) amejitokeza na kukana madai ya Lissu?

Kama hajajitokeza,kwanini tusiamini Lissu alikuwa sahihi kwa asilimia 100 kuwa anafuatiliwa na aliowatuhumu?

Je,watu hawa wameacha kumfuatilia au wamebadili mbinu?

Tuko salama kweli?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lissu alishatoa angalizo kwa igp na mkuu wa usalama wa taifa kuwa kuna watu wanamfatilia.

Mwenyekiti wa bavicha nae aliongeza kwenye press kuwa lissu anatishiwa na kuna comments na mtu mmoja ambaye wanamtilia shaka wanazo print out zake za social media.

Lkn pia huyo mtu jana pia facebook alifadhaishwa kutokana na lissu kuendelea kuwa hai. Leo kwenye profile yake ametoa picha yake akifikiri kuwa watu hawana picha zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amani iwe nanyi, naomba kila mtanzania mwenye uwezo na utaalam wa kuangalia usajili wa magari atusaidie kuangalia jina la mmiliki wa gari ambalo lilitajwa na tundu kumfatilia tangu dar na akilipata atuwekee hapa jf, tutakua tumeisaidie police kumkamata
Binafsi naamini polisi wanajua kila kitu, tabu ni kwamba Lisu yupo upande mwengine. Tuhuma hizo zingetolewa na upande wa pili polisi ingekuwa pro-active.sasa hivi mtahimizwa kuipelekea polisi taarifa.
 
Hivi ulitegemea kila upuuuuzi aongeao huyo kamanda wenu utolewe maelezo?? Yeye TL aitishe press tena kisha aongelee, hapa hapati airtime, apambane na hali yake tu!
Kuna wakati tuwe na akiba ya maneno. Alichokilalamikia ndicho kimedhihirika kweli kilivyo.
Get well soon hon. TL!
 
Back
Top Bottom