Mmiliki halali wa mtoto ni mama au ni baba?

Mallia

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
437
1,532
Eti kwanini wanaume ndio huwa wanapewa asilimia kubwa kama wamiliki wa watoto wanao zaliwa? Ikitokea mimba mwanaume ndio anapewa lawama za kwanza na majukumu yote ya kulea mtoto kama mhusika mkuu na watoto huwa tunawaambia wanaume kwamba tuna mimba zao.

Lakini kibaolojia inasemekana kuwa yai la baba linapokutana na yai la mama na kuungana ndio hupatikana mtoto so mtoto kumbe ni wa watu wawili baba na mama sasa kwa nini watoto majina yao ya mwisho huwa ni ya wazazi wao wa kiume na sio wa kike? Kwanini watoto wengine huwa wanafanana na mama zao kuliko hata baba zao je nani ni mmiliki halali wa mtoto?

Mama na mtoto
7c7d28457efb671e4d2bde2ff87c8f8f.jpg
 
Sasa umeuliza kumbe unajua ??? Suala LA majina limekaa kitamaduni zaidi na inatofautiana mahali namahali.

Kuna nchi wanatumia Jina LA mama kama jina LA mwisho !!.

Lkn pia Baba anapewa heshima iyo kwaajili tu yakulinda Existence yake maana tinaamin mwanamme ndio mwamzishaji Wa familia mpaka kua ukoo!!.
 
Baba ndiye mmiliki, ndio maana hata majina tunaitwa kupitia baba.
kwa nyie mnao amini mungu, naona pia mnamwita baba.

Baba ndio mashine,
 
Inategemea na mfumo wa jamii husika,kama ni ya kimama(matrilineal) au ya kibaba(patrilineal). Kwa jamii nyingi za kiafrika ni za kibaba,yaani mtoto anakua ni mwanaukoo wa ukoo wa babaye moja kwa moja halikadhalika kwa jamii za kimama.
Kibayolojia mtoto anaweza kua ni 51% wa mama na 49% wa baba.Sababu baba akishatia mbegu yake hapo ndio basi tena hausiki tena na ukuaji wa hyo mbegu yake ila inakua ndani ya mwili wa mwanamke,lakini cha ajabu ni kua mtoto hufwata kundi la damu la babaye.
 
.......Ndiyo umejibu nini sasa?hapa sio Facebook mtu anapokuuliza anataka kupata idea kwamba ulichokiuliza unakijua japo kidogo but unajibu kama uliuliza kujifurahisha.jifunze!!!
23
 
kabla sijajibu uzi wako unazungumzia wazungu au wazungu au wa africa maana swala hili lazima tuzungumzie wa africa pamoja na mila na desturi zao zinasemaje
Eti kwanini wanaume ndio huwa wanapewa asilimia kubwa kama wamiliki wa watoto wanao zaliwa? Ikitokea mimba mwanaume ndio anapewa lawama za kwanza na majukumu yote ya kulea mtoto kama mhusika mkuu na watoto huwa tunawaambia wanaume kwamba tuna mimba zao.

Lakini kibaolojia inasemekana kuwa yai la baba linapokutana na yai la mama na kuungana ndio hupatikana mtoto so mtoto kumbe ni wa watu wawili baba na mama sasa kwa nini watoto majina yao ya mwisho huwa ni ya wazazi wao wa kiume na sio wa kike? Kwanini watoto wengine huwa wanafanana na mama zao kuliko hata baba zao je nani ni mmiliki halali wa mtoto?

Mama na mtoto
7c7d28457efb671e4d2bde2ff87c8f8f.jpg
 
Wote ila upande wa baba nakuwa na nguvu ndo mana hata ukiulizwa we mtoto wa nani lazima utaje jina la ukoo wa baba yako upande wa mama hauna nguvu ndo mana hata watu wanadiliki kuoa au kuolewa na binamu zao upande wa mama
 
Mmliki halali wa mtoto ni mwanamke hasa ukizingatia mwanamke anaweza kuzaa bila mwanaume - asexual reproduction mfano mzuri Yesu kuzaliwa na bikira Maria.
 
Back
Top Bottom