Mmachinga kaniuzia kanyanga,nimfanyeje?

Columbus

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
2,002
650
Alikuja ofisini kwangu akanitangazia biashara yake ya vitu mbalimbali ikiwemo ya power bank. Kwa kweli nilikuwa na mpango huo ndipo nilipomuagiza aniletee power bank yenye uwezo mkubwa kwa ajili ya tablet yangu.

Nilipomkunbushia aniletee aliomba nimfuate alipo ndipo aliponikabidhi hiyo power bank ambayo baada ya kuichaji niliitumia kwa dakika 5 tu ikawa imeisha chaji. Nimempigia simu kumjulisha na akaahidi kuniletea nyingine lakini kama siku 2 hivi ameamua kuzima simu yake kabisaa.sasa najiuliza nimfanyeje nikimuona?

Watanzania inabidi tuwe wakweli na sio wababaishaji!
 
Daah pole sana kwa hilo, usimchukulie kama mtu mbaya, inawezekana na yeye amechukua sehemu bila kuelewa, kama tayari unajua yuko wapi basi wewe unachobidi ufanye ni kujaribu kuongea nae kwanza, hamna haja ya "kumfanya" chochote kwanza, kama vipi mpe muda kwa sababu inawezekana ameogopa kukwambia kwamba anatafuta njia ya kupata power bank nyingine ya kukurudishia.Huu ni mtazamo wangu mimi tu kwa sababu napenda sana kujaribu kwa kiasi nnachoweza kuwa mpole na kuelewa kwamba sio kila mtu anapofanya kitu kibaya alikuwa na nia kama hiyo tangia mwanzo
 
Nimejaribu kufuatilia nikagundua aliniuzia power bank hiyo kwa sh. 40 elfu na kumbe kuna mchina fulani anaziuza kwa kati ya sh. 5 na 10 elfu tu,nimeamua kununua nyingine kwa sh.30 elfu.
 
kweli magari yanaingia kila siku kutoka mtwara,..
yakibeba watu wanachungulia madirishani kuangalia newyork ya TZ i.e Dsm,..
unauziwa power bank mbovu,..
 
kweli magari yanaingia kila siku kutoka mtwara,..
yakibeba watu wanachungulia madirishani kuangalia newyork ya TZ i.e Dsm,..
unauziwa power bank mbovu,..
Kwahiyo watu wa Mtwara ndiyo washamba? Jiulize hao wanaouza hizo bidhaa wengi wao wanatoka wapi kama siyo Mtwara na Lindi!
 
Alikuuzia sh ngapi? Pale unaponunua kitu cha bei rahisi ambayo ni below the market price inabidi ujiandae kwa vyote. Kisheria huna la kumfanya maana sheria inaonya, 'buyer be ware'!
 
Kwahiyo watu wa Mtwara ndiyo washamba? Jiulize hao wanaouza hizo bidhaa wengi wao wanatoka wapi kama siyo Mtwara na Lindi!
Na inawekana wapo mjini kabla yake huyo anadhani wenzie washamba, moja ya siri ya kutepeliwa ni pamoja na kujiona wewe ni mjanja unajua sana.
 
Hiyo itakuwa uonevu tu kwa hustler wa kimachinga kumbuka yeye ananunua hiyo bidhaa sehemu Fulani ili auze!
Hata ukimchukulia hatua umkamate itakuwa unamkomoa tu,
Ilaumu serikali yako kwa kuruhusu kuingiza bidha feki alafu na watu kama nyie mnapenda slope(virahisi)mkiletewa original mnalalia bei
 
hehehehee mkuu yani unanunua power bank kwa chinga wa kitaa??!! vijana wa mjini tunasema 'ushapigwa'.

Kizazi cha Dude hicho ktk ubora wao. teh teh teh

Pole mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom