GE2025 Mluya: Serikali yangu itakuwa na wajibu wa kuwatunza mama mjamzito na mtoto kwa kumpa lishe bora kwa muda wa miezi mitatu

GE2025 Mluya: Serikali yangu itakuwa na wajibu wa kuwatunza mama mjamzito na mtoto kwa kumpa lishe bora kwa muda wa miezi mitatu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Democratic Party (DP), Abdul Juma Mluya, akiambatana na Mgombea wake mwenza Sadoun Abrahman Khatib, leo Agosti 13, 2025, wamechukua fomu za uteuzi katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Njedengwa jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu, Mluya alisema huu ni wakati wa kuwakomboa Watanzania kwa kumaliza malalamiko ya muda mrefu kwenye huduma za kijamii, ikiwemo sekta ya afya, kuboresha maisha ya watumishi wa umma, na kuinua maslahi ya Jeshi la Polisi na Magereza.

“Serikali yangu itakuwa na wajibu wa kuwatunza mama mjamzito na mtoto kwa kumpa lishe bora kwa muda wa miezi mitatu,” amesema Mluya.

 
Mgombea wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Democratic Party (DP), Bw. Abdul Juma Mluya akiambatana na mgombea Mwenza Bw. Sadoun Abrahman Khatib wamejitokeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuchukua fomu ya kuomba uteuzi wa kugombea Urais Katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 huku akibainisha kuwa vipaumbele vyake ni afya, kilimo na maslahi kwa watumishi wa umma




Chanzo: ITV DIGITAL
 
Chadema hawatak watu wenye sera
Huyu angemtukana rais saiv angekua na wafuasi wengi tuh
 
Back
Top Bottom