Mloganzila kunani paleeee mbona...

Mloganzila kunani paleeee mbona...

MUSHEKY

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
2,812
Reaction score
2,765
Habarini wakuu,

Kwa nyakati tofauti ndani ya jiji la Dar nilikua nikisikia tuhuma mbali mbali zinazotupiwa kwa hii hospitali yetu kubwa ya kisasa na yenye sifa za kimataifa

Nimesikia mara kadhaa kwa watu kwamba ukimpeleka mgonjwa wako pale kama ni serious case basi ujue atapotea tu

Minong'ono hii inakuja kwa dhana kuu mbili ambazo serikali hasa wizara ya afya naomba ifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wake na kuleta ufumbuzi

Dhana ya kwanza ni kwamba madaktari wengi wa pale ni madaktari wanafunzi ambao hufanya mazoezi kwa vitendo kwa wangonjwa.......

Dhana hii imepelekea wagonjwa wengi wanaopewa rufaa ya kwenda kule kuikacha hospitali hiyo na kurudi majumbani

USHUHUDA: wiki kadhaa zilizopita nikikua pale muhimbili kumuuguza mgonjwa wangu ambaye hata hivyo aliamriwa na madaktari afanyiwe upasuaji tumboni ili kuondoa uvimbe aliokua nao

Jambo la kushangaza ambalo pia ndilo limenisukuma kuandika mada hii ni baada ya ndugu yangu huyo pamoja na wagonjwa wengine kama kumi na tano waliokua wodini hapo kupewa rufaa ya kwenda hospitali ya mloganzila

Wodi iligeuka kua uwanja wa mabishano kati ya aliyetoa maelekezo hayo na wagonjwa.....wengi walilalama kwamba hawawezi kwenda kule kufa

Ghafla niliona wagonjwa hao wanafungasha mabegi na kusepa bila kwenda walikoamriwa

Dhana ya pili ni gharama kubwa ambayo inalalamikiwa hospitalini hapo ambayo pia inawafanya wagonjwa wapakimbie

Kwa kua haya ni maneno yanazungumzwa kwa wingi, naiomba wizara husika ichunguze jambo hili kwa makini

Nawasilisha
 
yaani unafanya majaribio kwa mtu anayeumwa serious.....pumbafu mlonganzila
 
Ukishaona Afya na elimu vinakuwa vya gharama jue taifa hilo liko chini na duni kiuchumi na watu walio choka kabisa hawafai kabisa hawasikii la muwadhini Wala mnadi swala
 
Wodi iligeuka kua uwanja wa mabishano kati ya aliyetoa maelekezo hayo na wagonjwa.....wengi walilalama kwamba hawawezi kwenda kule kufa
Rip loving anko... Mloganzila has a story to tell
IMG_20190831_162306.jpeg
 
Hizi tuhuma inabidi serikali izifanyie kazi haraka,lakini cha kusikitisha maviongozi yapo bize na akina membe na musiba,uchaguzi wa serikali za mitaa,kuna jitu lingine juzi tu hapa limewaongopea watu waende uwanja wa taifa kuna mikopo ya riba nafuu,watu kufika uwanja wa taifa wanakutana na KONGAMANO LA NDOA agrrrrrrriii yaani wanakomaa na mambo ya kijingajinga tu nchi hii sijui tumerogwa
 
Habarini wakuu,

Kwa nyakati tofauti ndani ya jiji la Dar nilikua nikisikia tuhuma mbali mbali zinazotupiwa kwa hii hospitali yetu kubwa ya kisasa na yenye sifa za kimataifa

Nimesikia mara kadhaa kwa watu kwamba ukimpeleka mgonjwa wako pale kama ni serious case basi ujue atapotea tu

Minong'ono hii inakuja kwa dhana kuu mbili ambazo serikali hasa wizara ya afya naomba ifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wake na kuleta ufumbuzi

Dhana ya kwanza ni kwamba madaktari wengi wa pale ni madaktari wanafunzi ambao hufanya mazoezi kwa vitendo kwa wangonjwa.......

Dhana hii imepelekea wagonjwa wengi wanaopewa rufaa ya kwenda kule kuikacha hospitali hiyo na kurudi majumbani

USHUHUDA: wiki kadhaa zilizopita nikikua pale muhimbili kumuuguza mgonjwa wangu ambaye hata hivyo aliamriwa na madaktari afanyiwe upasuaji tumboni ili kuondoa uvimbe aliokua nao

Jambo la kushangaza ambalo pia ndilo limenisukuma kuandika mada hii ni baada ya ndugu yangu huyo pamoja na wagonjwa wengine kama kumi na tano waliokua wodini hapo kupewa rufaa ya kwenda hospitali ya mloganzila

Wodi iligeuka kua uwanja wa mabishano kati ya aliyetoa maelekezo hayo na wagonjwa.....wengi walilalama kwamba hawawezi kwenda kule kufa

Ghafla niliona wagonjwa hao wanafungasha mabegi na kusepa bila kwenda walikoamriwa

Dhana ya pili ni gharama kubwa ambayo inalalamikiwa hospitalini hapo ambayo pia inawafanya wagonjwa wapakimbie

Kwa kua haya ni maneno yanazungumzwa kwa wingi, naiomba wizara husika ichunguze jambo hili kwa makini

Nawasilisha
Unayosema yana ukweli kwani hata mimi nimewahi kuuguza mgonjwa pale na matokeo yakawa ni hayo. Sawa hata MNH tunawapeleka na wanakufa, lakini unaziona juhudi za Mafaktari na huduma na unakubali kuwa mgonjwa wako alistahili kufa.

Nadhani Awamu ya 5 imegeuza madhumuni ambayo Mloganzila ilianzishiwa. Nisipokosea ilikuwa iwe Traching Hospital ya MUHAS lakini kinyume chake imekuwa ni kitengo cha MNH.
Kuna mahali tunakosea, Tujisahihishe
 
Back
Top Bottom